Si kweli , kuna majina yatapigiwa kura na kamati ya wabunge wa ccm,,
Hivyo kamati kuu wala haiitaji kupasuka vichwa,
Acha propaganda
Watapigia kura majina yote 71 lazima wachuje kwanza kamati kuu
 
Tulia ndio spika ajaye
1.Anatosha(kwa kigezo cha elimu)
2.Mwenzetu
3.Umri una wastani mzuri
4.Gender equality
5. Hajawahi kutuhumiwa popote
Tulia ana ghubu sana na anakosa ukomavu. Chenge ndio best candidate wa hii nafasi. Kuhusu kachfa siyo kigezo, hazijathibitishwa popote, ila akina rizimoko waliokuwa na tuhuma za sembe tuliona wakipewa nafasi za uteuzi.
 
Chenge ni fisadi. Unaiba 1.5 bilion ya serikali kwa mikataba ya hovyo wakati wa ununuzi wa Rada halafu unasema ni vijisenti?

Leo hii akikaa bungeni so ataiba 1 Trilioni , ataitaje hii sasa?

Chenge ametumika kipindi cha nyerere, mwinnyi, mkapa, na jk. Experience yake ni old school kwa sasa.

Taifa hili kwa sasa linahitaji speaker kijana wa umri wa kati na msomi ambaye ataendana na mabadiliko ya dunia/ global changes na kisha ku-relate na hali halisi ya nchi yetu in making decision katika bunge letu.

Huyo mzee na hiyo experience ya miaka 90's imepitwa na wakati. Watanzania tunataka kusonga mbele na kurudishwa nyuma na mauzoefu yaliyopitwa na wakati eti kisa masters ya havard ya mwaka 1975 wakati leo ni 2022 = miaka 48 imeshapita. Hii ni aibuu kubwa.

Chenge apumzike akalee wajukuu wake na vitukuuu
Kwa wakati tofauti nimekuwa nikifuatia Chenge akiendesha mikutano ya bunge, ni mzuri sana kwa kuwa na uvumilivu.Huwezi mlinganisha na akina Tulia na comp. Kuhusu weledi wake,bado ni mzuri sana kwenye Sheria. Pamoja na umri alionao, uwezo wake wa kusoma na kuelewa unazidi kwa mbali vijana wengi. Kama kuna hoja nyingine zitolewe ila siyo kutumia kigezo cha umri na uwezo wa kazi ambavyo siyo halisia katika suala hili.
 
Chenge ni fisadi. Unaiba 1.5 bilion ya serikali kwa mikataba ya hovyo wakati wa ununuzi wa Rada halafu unasema ni vijisenti?

Leo hii akikaa bungeni so ataiba 1 Trilioni , ataitaje hii sasa?

Chenge ametumika kipindi cha nyerere, mwinnyi, mkapa, na jk. Experience yake ni old school kwa sasa.

Taifa hili kwa sasa linahitaji speaker kijana wa umri wa kati na msomi ambaye ataendana na mabadiliko ya dunia/ global changes na kisha ku-relate na hali halisi ya nchi yetu in making decision katika bunge letu.

Huyo mzee na hiyo experience ya miaka 90's imepitwa na wakati. Watanzania tunataka kusonga mbele na kurudishwa nyuma na mauzoefu yaliyopitwa na wakati eti kisa masters ya havard ya mwaka 1975 wakati leo ni 2022 = miaka 48 imeshapita. Hii ni aibuu kubwa.

Chenge apumzike akalee wajukuu wake na vitukuuu
Aibu kubwa ni darasa la nne wa mwaka 1975 aliweza kuongea kiingereza fasaha..
Kuliko pro ndalichako aliyekuwa waziri wa elimu.
 
Kamati kuu ikishateua, basi huyo ndiye Spika.

Pale bungeni ni utaratibu tu wa kikanuni.

Hakuna mbunge wa kupinga jina lililopelekwa na Kamati kuu.
Kamati kuu inateua jina zaidi ya moja, part caucus ndo wanateua jina moja la kwenda bungeni
 
Aliyekuwa katibu wa bunge kwa takribani zaidi ya muongo mmoja, Thomas Kashilila ndiye spika ajaye wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Aliyekuwa katibu wa bunge kwa takribani zaidi ya muongo mmoja, Thomas Kashilila ndiye spika ajaye wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
images (4).jpg
 
Kamati kuu inateua jina zaidi ya moja, part caucus ndo wanateua jina moja la kwenda bungeni
Hahahaaaa......hahahaaaa.........!

Kwahiyo party caucus ndio ilimwambia Sitta ile ni zamu ya mwanamke?

Kamati kuu iwe ya CCM au Chadema ndio huamua kila kitu!
 
Tulia ana ghubu sana na anakosa ukomavu. Chenge ndio best candidate wa hii nafasi. Kuhusu kachfa siyo kigezo, hazijathibitishwa popote, ila akina rizimoko waliokuwa na tuhuma za sembe tuliona wakipewa nafasi za uteuzi.
Chenge wako hapati u spika
 
UJASIRI wake wa kubainisha kwa uwazi kwa nini anaomba Uspika tofauti na wengine ambao hawajaweza kueleza kinagaubaga ukiacha wachache sana waliojaribu kidogo.

Usimamizi wake wa Kijasiri wa sheria juu ya Uvuvi Namba 22 ya mwaka 2003 katika kupambana na Uvuvi haramu Nchini uliowezesha ongezeko kubwa la samaki na kuwezesha mauzo ya samaki nje ya nchi kupaa kutoka Tsh Bilioni 379 hadi kufikia Tsh Bilioni 692 karibu Bilioni 700 mwaka 2020 fedha ambazo zilikwenda mfuko Mkuu wa Serikali kutekeleza majukumu mbalimbali ya kitaifa.

Mpina hajui kujipendekezapendekeza kwa misingi iliyosimama
lakini pia anaujua umaskini wa watu wa Chini,hivyo basi,Atawabana Mawaziri kufanya kazi kwelikweli, vinginevyo majibu na taarifa za Serikali zisizojitosheleza Bungeni chini ya Spika Mpina hazitapita.

Mpina kwa kuwa amefanya kazi katika Wizara ya Muungano atakuwa pia msikivu kwa upande wa Tanzania Zanzibar hasa ukizingatia nafasi anayoiomba ni ya Muungano.

Pia tunakumbuka kuwa Trillion zetu 360 ambazo aliziibua yeye Bungeni tutamdai hadi zipatikane hata kama ni kumikumi kila mwaka kwani anajua zilipo.

Tulishuhudia akiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi kwa namna alivyokuwa amejitahidi kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji na katika kipindi alichoongoza Wizara hiyo hatukuwahi kusikia

Wafugaji, Wavuvi na Wakulima ni sehemu ya Watanzania walio wengi watakuwa wamempata msimamizi wa Muhimili sahihi kwani historia yake na uzoefu wake ameyaishi maisha haya hivyo Mawaziri katika Wizara hizi zote itabidi wafanye kazi zaidi kulifafanulia Bunge juu ya maendeleo na changamoto za ukweli bila blaa blaa.

Uzoefu na mambo makubwa aliyosimamia na kuonekana matokeo dhahiri kabisa yapo kwenye CV yake
 
.... hivi yule profesa wa shahada 9 mbona kayeyuka kama umande wa asubuhi? Yu wapi yule gwiji au vitisho tayari?
 
Sukuma gang nani ampe usupika, enzi zenu zilishapita, hatutafuti wazuri tunatafuta watiifu wa chama kama ndugai alivo kua kwa mwendazake, wakati kichwa ni empty.
 
Back
Top Bottom