Ndivyo ilivyo hadi sasa na haya majina mawili ndio yanaipasua kichwa Kamati Kuu ya CCM.

Kwa pamoja tuiombee CCM jamani bila kujali itikadi zetu.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Tuna taka katiba mpya
Screenshot_20220118-142702.jpg
 
Chenge ni fisadi. Unaiba 1.5 bilion ya serikali kwa mikataba ya hovyo wakati wa ununuzi wa Rada halafu unasema ni vijisenti?

Leo hii akikaa bungeni so ataiba 1 Trilioni , ataitaje hii sasa?

Chenge ametumika kipindi cha nyerere, mwinnyi, mkapa, na jk. Experience yake ni old school kwa sasa.

Taifa hili kwa sasa linahitaji speaker kijana wa umri wa kati na msomi ambaye ataendana na mabadiliko ya dunia/ global changes na kisha ku-relate na hali halisi ya nchi yetu in making decision katika bunge letu.

Huyo mzee na hiyo experience ya miaka 90's imepitwa na wakati. Watanzania tunataka kusonga mbele na kurudishwa nyuma na mauzoefu yaliyopitwa na wakati eti kisa masters ya havard ya mwaka 1975 wakati leo ni 2022 = miaka 48 imeshapita. Hii ni aibuu kubwa.

Chenge apumzike akalee wajukuu wake na vitukuuu

Wanataka kuleta speaker mlugaluga wa enzi za mwalimu
 
Kamati kuu ikimpitisha Betina itajihithirisha kwamba Ni team mwendakuzimu hivyo nayo inahitaji kuwa overhauled.
Betina Ni chaguo la aliyeko kuzimu na sababu za kumchunuku anazijua aliyeko kuzimu hapana mwingine mwenye pumzi anayezijua.

Masele is the right guy..
Vote for masele


Wanaonea wivu wa mafanikio hawawezi kumpa Masele

Masele anagesongesha Taifa mbele kisasa na si kikoloni
 
Ndivyo ilivyo hadi sasa na haya majina mawili ndio yanaipasua kichwa Kamati Kuu ya CCM.

Kwa pamoja tuiombee CCM jamani bila kujali itikadi zetu.

Mungu wa mbinguni awabariki sana!
Si kweli , kuna majina yatapigiwa kura na kamati ya wabunge wa ccm,,
Hivyo kamati kuu wala haiitaji kupasuka vichwa,
Acha propaganda
 
Hiyo kamati kuu wakimpitisha Tulia itadhihirisha ilivyo muhimu kupata katiba mpya.

Tulia ni batili kwa sababu haja jiuzulu unaibu spika. Hivyo hastahili kujadiliwa kwenye nafasi ya uspika.
Kwenye ngazi ya chama ruksa,, jina likienda bungeni ndiposa atajiuzulu
 
Si kweli , kuna majina yatapigiwa kura na kamati ya wabunge wa ccm,,
Hivyo kamati kuu wala haiitaji kupasuka vichwa,
Acha propaganda
Kamati kuu ikishateua, basi huyo ndiye Spika.

Pale bungeni ni utaratibu tu wa kikanuni.

Hakuna mbunge wa kupinga jina lililopelekwa na Kamati kuu.
 
Hakuna anayeridhika na kidogo, hiyo kanuni ya kuwa chini siku zote haipo,kujiuzulu au kutokujiuzulu hakufanyi asiwe na sifa na nia ya kujaribu Uspika.
Kwa hiyo ulikuwa unaunga mkono katiba ibadilishwe ili shujaa aendelee kusalia madarakani atake asitake??
 
Back
Top Bottom