Nani anafaa kupeperusha bendera ya CHADEMA 2020 kwenye kinyang'anyiro cha Urais? | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani anafaa kupeperusha bendera ya CHADEMA 2020 kwenye kinyang'anyiro cha Urais?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Lizaboni, Dec 5, 2017.

 1. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2017
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,796
  Likes Received: 13,809
  Trophy Points: 280
  Wadau, amani iwe kwenu.

  Nimekaa nikafikiria na kuwaza kwa kweli nimebaini CHADEMA wana hali mbaya sana kisiasa. Wamepoteza dira na hawana mwelekeo. Sioni wa kukinusuru hiki chama angalau kisimamishe tu mtu wa kuweza kukimbizana na Rais Magufuli 2020.

  Mtaji wao wa mwaka 2015, Edward Lowasa hajapanga kugombea tena 2020 bali anajipanga kugombea 2025 bila shaka kwa tiketi ya CCM kama atakubaliwa kurejea chamani. Sasa najiuliza, nani mbadala wa Lowasa 2020?

  Nimejiuliza peke yangu nimekosa jibu. Nisaidieni wadau kunipa jibu la swali langu hili
   
 2. P

  Pohamba JF-Expert Member

  #41
  Dec 5, 2017
  Joined: Jun 2, 2015
  Messages: 16,518
  Likes Received: 25,654
  Trophy Points: 280
  Si kweli!

  Sifa ya Shahada kwa Mgombea Urais ni Kanuni ya Chama cha Mapinduzi sio Katiba ya Jamhuri
   
 3. madalleh

  madalleh Member

  #42
  Dec 5, 2017
  Joined: Feb 26, 2017
  Messages: 72
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 15
  Mnyika
   
 4. BILLY ISISWE

  BILLY ISISWE JF-Expert Member

  #43
  Dec 6, 2017
  Joined: Feb 10, 2014
  Messages: 1,113
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Awezi. Hana elimu ya chuo kikuu.
   
 5. 1000 digits

  1000 digits JF-Expert Member

  #44
  Dec 6, 2017
  Joined: Oct 16, 2012
  Messages: 2,849
  Likes Received: 1,378
  Trophy Points: 280
  Chadema ina watu wengi Makini.

  Sumaye ni Bora zaidi
  Nyarandu
  Heche
  Makongoro Mahanga.
  Meya Kalisti.
  Lisu.
  Juma Mwalimu.
  Prof. Safari
  Nyarandu.

  Hata watakao toka CCM kwa imani ya kujenga Demokrasia watafaa mana ni watanzania wenzetu.

  Vyama vyote ni sawa Hata Zito Kabwe akirudi Chadema itapendeza zaidi.

  Ila cha msingi kabisa ni Katiba ya Warioba ije kabla ya huo uchaguzi.
  Ili tuwe na uchaguzi wa kupiga kura kwa wagombea wa uongozi sio vita ya madaraka!

  Bila Katiba ya warioba uchaguzi wa 2020 itakua ni vita ya madaraka sio uchaguzi.
  Mana wenye madaraka hawataki kusikia suala la kushindwa kwenye majimbo.

  Sijui woga ni wa nini wakati hata ikija tume huru bado rais aliyepo atashinda japo hata kama ni kwa kura chache lakini atashinda kwa hali ya upinzani ilivyo na imani kubwa ya wananchi kwake.

  Kwa hiyo ni bora pawe na tume huru ili uchaguzi ufanyike kwa haki na huru na wenye ushawishi na sera nzuri wanyakue viti vingi vya ubunge na udiwani.

  Ingekua ni bora kabisa Wapinzani wakamsimaisha mgombea mmoja kwa ajili ya kupata viti vingi vya udiwani na ubunge.
  Suala la kushinda urais halina tija sana.
  Tukiwa na katiba ya Warioba suala la urais sio la muhimu sana kwa wapinzani na watanzania bali suala la muhimu ni utawala bora wenye kuwapa wananchi nguvu ya kushiriki katika ujenzi wa maisha yao na taifa kwa ujumla wakati huo huo haki za kila mtu zikilindwa kikatiba.

  Wapizani Suala la Urais lisiwape kiwewe.
  Tunaye Rais wa Awamu ya Tano.
  Na awamu ya Tano inaishia 2025. Tusipoteze muda kuwaza urais wa 2020.
  Wakati huo anaweza akawekwa hata Prof. Safari. Akaleta ushindani lakini kwa lengo la kukamata halmashauri Nyingi zaidi na kuwa na mameya wengi zaidi wa ulinzani.
  Ikiwezekana miji yote ichukuliwe na mameya wa upinzani.

  Mbowe angalia mbali zaidi ushindi ikulu sio mahali pa kukimbilia bila mipango ya kidola.
  CCM ina wazee wengi ndani ya vyombo vyote na mihimili yote.
  Subiri wapungue kiasili mpaka watajikuta wamebaki vijana wasioijua CCM. Hapo Ikulu itakua inamkaribisha yeyeyote.

  2020 wapinzani Anzieni chini kushika madaraka kuanzia kwenye mitaa.
  Mizizi ikikatwa mti hunyauka wenyewe kuliko kukata matawi.
   
 6. Boniphace Kichonge

  Boniphace Kichonge Verified User

  #45
  Dec 6, 2017
  Joined: Jul 31, 2017
  Messages: 1,059
  Likes Received: 1,317
  Trophy Points: 280
  Lissu Alikuwa na Sifa na Uwezo wa kugombea
   
 7. K

  Kennedy kidenda Member

  #46
  Dec 6, 2017
  Joined: Oct 28, 2017
  Messages: 14
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 5
  Bado atujapata mtu anaye sitaili kukalia hicho kiti au tusubili
   
 8. kanali mstaafu

  kanali mstaafu JF-Expert Member

  #47
  Dec 7, 2017
  Joined: May 17, 2015
  Messages: 2,379
  Likes Received: 1,969
  Trophy Points: 280
  Tundu Lissu
   
 9. M

  Makuti Malubu JF-Expert Member

  #48
  Dec 7, 2017
  Joined: Jul 22, 2017
  Messages: 339
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Pray 4 TL
   
 10. kasulamkombe

  kasulamkombe JF-Expert Member

  #49
  Dec 7, 2017
  Joined: Oct 3, 2017
  Messages: 2,268
  Likes Received: 2,377
  Trophy Points: 280
  KWANI BADO KITAKUWEPO
   
 11. Mkwaju Ngedere

  Mkwaju Ngedere JF-Expert Member

  #50
  Dec 7, 2017
  Joined: Oct 15, 2016
  Messages: 976
  Likes Received: 808
  Trophy Points: 180
  Wale waliomfanyia MAZISHI YA HESHIMA BOBI aka MH.MBWA, mmoja wao anafaa kupeperusha bendera !!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...