Nani anaestahili kuchukua nafasi ya IGP kumrithi Sirro endapo mabadiliko yakitokea?

Iwapo Raisi Samia ataridhia kufanya mabadiliko katika Jeshi la Polisi kwa kumuondoa IGP Sirro, unadhani ni nani atafaa kukabidhiwa mikobo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini?

Inawezekana tunaona wengi wao ni tatizo, ila ukweli ni kwamba kuna mmoja,wawili au watatu miongoni mwao wanaweza kuwa na afadhali au hata kufaa kabisa kwa nafasi hiyo.

Hivyo, wadau kupitia hapa JF, tutoe mapendekezo ya nani anafaa kumrithi Sirro iwapo ataondoka, ataondolewa au kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Kwa mnaowajua vizuri vigogo wa hili Jeshi, msaidieni Mama kujua ni yupi anafaa kuwa IGP baada ya Sirro(tumshauri).

Karibuni kwa mapendekezo (vetting isiyo rasimi).
Kamanda Heche angefaa sana hiyo nafasi akishirkiana kwa karibu na kamanda Lema.
 
Watu mnasahau haraka Sana
Kipindi Cha said mwema si ndio akina zombe walikuwa wanauwa wafanyabiashara, mwangosi alipigwa bomu na Askari, maandamano ya chadema kule Arusha n.k
Kifupi polisi wote wanafanana
Kipindi salama nafikiri ni kipindi cha Ernest Mangu ila na yeye ndipo lilipoibuka kundi la Al shabab kula Tanga na Kibiti.
 
Bashite makonda alikuwa akimtesa sana, sasa Dua la kuwabambikia kesi wapinzani na Dua la kuitesa familia ya Hamza kuwakamata hovyo watu wasiohusika ndilo linamtafuna IGP
Acha tu limtafune maana sasa hivi hekima na busara zimempita kushoto
 
Kipindi salama nafikiri ni kipindi cha Ernest Mangu ila na yeye ndipo lilipoibuka kundi la Al shabab kula Tanga na Kibiti.
Yes, hata kipindi Cha Mangu yalikuwa yaleyale tu
Tena katika IGP waliokuwa wakionekana dhaifu basi Ni Mangu, maana kipindi chake ndio ulianza uvamizi wa vituo vya polisi.
Polisi wwlivamiwa vituoni, waliuliwa na kuporwa bunduki.
Moja ya tukio lisilosahaulika ni lile la kituo kikubwa cha Ukonga Stakishari
 
John John Mnyika naona atafaa sana. Ile kauli yake ya ushujaa aliyo mwambia Mkwere kuwa dhaifu ina onyesha utimamu na Ushujaa wake. Mnyika na Jamhuri ya JF OYEEEEEE.
 
Ni muda muafaka wa kuwa na IGP mwana mama.
Kumradhi kinababa makamanda wametamalaki sana katika majeshi yetu na tunawashukuru kwa mchango wao, ila kwa sasa ni muda muafaka wa kuwapisha kina mama kwenye sekta hizi nyeti za taifa.
Mama tuanze na IGP mwanamke.
Then utuletee mkuu wa TISS mwanamke, kisha Chief of diffence mwanamke, na ikikupendeza magereza, JKT,nk....
Wanawake wanauwezo zaidi wa kuongoza hizi taasisi nyeti kama ulivyoonyesha njia.
Mamwavi Nkabasia (@Joeselasini) Tweeted:
Huyu kamanda awe IGP mnasemaje. Tena tutaandika historia ya kuwa na IGP wa kwanza mwanamke nchini. https://t.co/isHUUGYjIW
 
Ungelikuwa wewe ni IGP yapi ungefanya. Tatizo la sisi binadamu ni kujiona wakamilifu, tusio na mapungufu hata chembe huku tukiwaona wengine hawafai. Hesabu mapungufu yako kwanza kabla hujaangalia ya mwingine. Ikibidi angalia mapungufu katika familia na ukoo wako, zaidi jitathmini kama umeleta mabadiliko chanya.
Camillus Wambura
 
Kuna Jamaa anaitwa Njeera Nadhani ni RPC Mtwara Jamaa ana utulivu sana anaweza..
 
Iwapo Raisi Samia ataridhia kufanya mabadiliko katika Jeshi la Polisi kwa kumuondoa IGP Sirro, unadhani ni nani atafaa kukabidhiwa mikobo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini?

Inawezekana tunaona wengi wao ni tatizo, ila ukweli ni kwamba kuna mmoja,wawili au watatu miongoni mwao wanaweza kuwa na afadhali au hata kufaa kabisa kwa nafasi hiyo.

Hivyo, wadau kupitia hapa JF, tutoe mapendekezo ya nani anafaa kumrithi Sirro iwapo ataondoka, ataondolewa au kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Kwa mnaowajua vizuri vigogo wa hili Jeshi, msaidieni Mama kujua ni yupi anafaa kuwa IGP baada ya Sirro(tumshauri).

Karibuni kwa mapendekezo (vetting isiyo rasimi).
20210829_161816.jpg
 
Wewe ndiyo unastahiri
 
Back
Top Bottom