Nani anaandikaga subtitles za movies za Bongo?

wao hamsini mpaka mia,ni jana tu nilikua naangalia documentary moja ya maproducer wanaijeria jamaa akasema wanaprodyusi muvi 500,kwa mwaka,yaani wao movi moja ni wiki tu iko tayari,na wanasema iko siku movie zao zitauza kuliko za hollywood,LMAO:rolleyez:
 
Tell me about it! Yaani hili la sub-titles bora waache kuweka, wajipange upya, watafute watu watakaoweza kuwaandikia ndio waweke! Yaani nikiangaliaga kwenye DSTV huwa naona aibu na naamini hata hilo soko la kimataifa wanalolitafuta kwa sub-titles hizi itakuwa ngumu!
 
...Juzi nimeona moja jamaa anamuambia mpenzi wake "Nimesahau kukusifia!" na kwenye caption imeandikwa "I forgot to Proud You!" Eh?
 
Afadhali kuna mtu ameanzisha huu uzi. Keroro balaa.
Wanatafsiri kiswanglish. Sijui aliepewa hiyo kazi ni Nuh Mziwanda Na Shilole?!!!!!
 
Mimi ndio huwa natafsiri bongo muvi tatiqzo wananilipa pesa ndogo sana embu fikiria buku tano kwa muvi moja bado nikiingia mtaani nakuta wameikata muvi wameweka pati wani na two
 
Jamani ni sawa bongo movie wanakosea sana ila haya mambo hata kwa wenzetu yapo.Kuna movie moja ya wakorea inaitwa missing you"ile movie ilibidi niitupe walikuwa wanaongea lugha yao ila subtitle ni kingereza ilikuwa ni zaidi ya bongo movie.Yani ilikuwa mbaya huelewi kitu.Sikuweza hata kuimaliza.kwaiyo ili swala ni la msingi sana wajirekebishe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom