Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Nadhani simulizi ya wizi inaweza kusimuliwa vyema kwa Mkuu wa nchi ikadhibitiwa kwani yeye anamiliki vyombo vyombo vya udhibiti. Naomba nichokonoe wizi huu wa madini ili wanaohusika wazibe palipotoboka.
Wizi unaweza kufanywa Kwa sababu mwizi amedhamiria kuiba lakini pia wizi unaweza kusababishwa na urasimu wa watoa huduma. Naomba niwaambie kwamba urasimu wa watoa huduma umezalisha nipe nikupe na hapa ndipo milioni moja ya Rushwa inapopofusha macho na kuruhusu madini ya mabilioni kuvuka mpaka.
Nchi jirani wanauza madini yanayozalishwa nchini, wanayatoa wapi? Watu wamehifadhi madini nyumbani je wanavuka nayo vipi maeneo ya uchimbaji?
Mbinu zinazotumika kuiba na kusafirisha madini kinyemela nje ni hizi zifuatazo;
1. Kwenye machimbo ya mirerani watu wanaboresha mahusiano na walinzi, yasemekena hakuna motisha kwa walinzi so kumotishana Kati ya walinzi na wenye madini kunasaidia kuvusha mzigo.
2. Katika mgodi huohuo limezaliwa kundi ambalo linafahamika kama " unajua Mimi ni Nani". Kundi hili limeingia ubia na viongozi na watu wenye nguvu na sasa wanoko wote waliokuwa wanadhibiti madini wanaondolewa waingie makabaila wanaoendana na mfumo wa dili. Ni kawaida Sasa hivi mtu kupiga simu juu akilalamika kusisumbuliwa na viongozi wakubwa kutoa maelekezo bila kujua dhamira ya malalamiko nikusafisha njia.
3. Mipakani hakuna ukaguzi, na penye ukaguzi watu wanaficha mzigo kwenye buti na kuandaa kiasi cha kusafisha njia. Wenye fedha waliojificha kwenye chama hakuna kukaa nikuchekeana tu. Ukitoa fedha kidogo wenye dhamana wanakuita mkarimu na wanakusafishia njia pamoja na kukupigia simu kukuuliza unapita lini Tena?
4. Wapo wenzetu wenye rangi wanaojihita wawekezaji wao wanaondoka nayo kwenye private jet, kumbuka nao wakikaguliwa sana wanalalamika usumbufu na wanasiasa wanawaabudu hivyo vijana wazalendo wanawajibishwa kwa uzalendo wao. Baadhi kurunzi linaeleza wanapita VIP no usumbufu.
5. Wanasiasa na wafanyabiashara wanafidia uporaji waliofanyiw awamu ya tano.
Nini, kifanyike? Mhe. Asomapo umbea huu aufanyie kazi may be atabaini si umber au stori za vijiweni kama nilivyozisikia vijiweni bali ndio ukweli. Vinginevyo kauli ya tumechezewa sana inarudi kwa Kasi tena ikidhaminiwa na watu walewale aliowateua.
Hawa watu sijui kwanini wanapenda kumkwamisha aliyewateua na sijui kwanini anayeteua anawaonea huruma aliowateua wanaomsaliti kwa kuvunja moyo wazalendo wachache waliopo mtaani. Hudumu umbeya wenye ukweli.