Byendangwero
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 871
- 56
Watu wote makini, wanakubaliana ya kuwa rais Kikwete hastahili hata kidogo kutuchagulia jopo la wataalamu wa kuratibu mchakato wa uandikaji wa katiba mpya. Hii inatokana na sababu zifuatazo; kwanza, yeye siye aliyeanzisha hoja hiyo, na hivyo itakuwaje basi, akaingilia hoja ya watu bila ya kujadiliana nao kwanza. Pili, kuna ushahidi ya kuwa yeye pamoja na serikali yake hawapendi kuwepo kwa katiba mpya. jambo hilo linazua hofu kwamba kujiingiza kwake kuna lengo la kuizima hoja hiyo. Na mwisho, zoezi hili linahitajika liwe shirikishi katika hatua zote, jambo ambalo halitawezekani ikiwa tume itakayo ratibu mchakato huo itateuliwa na rais. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, tume hiyo baada ya kukamilisha kazi yake, inatakiwa itayarishe ripoti ya mapendekezo yake na kuipeleka kwa rais; na rais kwa upande wake ataichambua ripoti hiyo na kuchukua yale tu atakayeona yanamfaa. Katika hali hiyo, hakuna uhakika ya kuwa katiba itakayotokana na mchakato wa aina hiyo, itakuwa inawakilisha matakwa ya watu. Ili kuepukana na kasoro hizo kuna haja kwa wadau wote kukaa pamoja na kukubaliana mfumo utakaotumika katika kufanikisha suala hili. Najua kuna wale wanao amini ya kuwa kazi hiyo itafanywa na bunge, lakini upende husipende, bunge letu lilivyo sasa, haliwezi kufanikisha jambo hilo bila ya kuwepo shinikizo kutoka kwa wadau; hasa kwa wakati huu ambapo rais amekwishatoa msimamo wake, na kwa wakati huo huo wadau mbalimbali wanaonekana kutoa kauli zinazokinzana. Labda tujiulize ni nani achukue jukumu la kuwakutanisha hao wadau. Naona chadema ifanye kazi hiyo. Hii inatokana na ukweli kuwa Katibu wake mkuu anakubalika miongoni mwa wengi wa wadau hao na hivyo anaweza kuwa kiungo muimu.