Nani amewajazia 'kitaalamu na kiusahihi' wagombea wa CCM? Inaruhusiwa kujaziwa fomu za kugombea?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,516
Hadi sasa, saa mbili na dakika 25 usiku wa Alhamisi ya tarehe 7/11/2019 sijasikia hata mgombea mmoja wa Mtaa, Kijiji au Kitongoji wa CCM aliyeenguliwa au kutoteuliwa kugombea nafasi aliyoiomba kwenye uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa.

'Vilio' na malalamiko dhidi ya kuenguliwa na kutoteuliwa kugombea yanatoka tu kwenye vyama vya upinzani. Hata rufaa za wagombea wa upinzani nyingi zimeshatupwa.

Yanatajwa makosa mbalimbali, hasa katika ujazaji wa fomu za kugombea, yaliyopelekea kuenguliwa au kutoteuliwa kwa wagombea wa vyama vya upinzani. Inavyoonekana, wagombea kupitia CCM wamejaza kwa usahihi na kitaalamu fomu zao.

Katika ufanano huo wa wagombea wa CCM wa kutokosea hata kidogo kujaza fomu zao nchini kote(kitu ambacho ni kigumu kwakuwa utofauti wa kibinaadamu haukosekani), nani amewajazia wagombea wa CCM fomu zao kwa utaalamu na usahihi? Kama yupo, inaruhusiwa kujaziwa fomu hizo?
 
Suluhisho ni KUSUSIA tu. Hongereni sana Chadema kwa kuchukua hatua sahihi na kwa wakati sahihi. Nina imani na vyama vingine vya upinzani navyo vitasusia ili ibakie Ccm peke yake.

Mwakani pia kama kawa, ni kususia tu. Na kura hatupigi. Huu utoto tukiendelea kuulea, unaweza ukaja kutuharibia amani ya nchi. Hivyo kuamua kususia, ni njia nzuri na salama! Maana hata policcm watakosa wa kuwaumiza.
 
CCM inapendwa sana mpaka wagombea wake wanajaziwa fomu ili wasikosee
Mimi interest yangu si wagombea wa chadema au ACT,interest yangu ni kuona kama baada ya kurudisha ccm kwa 100% tutaendelea na kupata unafuu wa maisha au hali ya maisha ndo itazidi kuwa mbaya?I do believe watanzania wengi hatuna akili sawa sawa, sasa kama maisha yatazidi kuwa mabaya reaction ya watanzania dhidi ya ccm itanipa kuproof kama hatuna akili kweli au tunazo lla tuliamua kujitoa ufahamu tu
 
Tutafika Tu
IMG_20191107_210959_234.jpeg
 
Back
Top Bottom