Nani amewahi kuwa Waziri wa Fedha bora na sifa zake ni zipi?

Nyauba

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
1,098
105
Wadau natumai umuhimu wa wizara ya fedha katika mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu unaeleweka vema. ndio wizara mpangaji wa bajeti ya serikali na yenye uwezo wa kuelekezaa matumizi bora ya fedha za umma kupitia manunuzi na kupunguza gharama za uendeshaji ili kuleta tija nchini.

je waziri wa fedha kama kiongozi wa kisiasa mwenye ushawishi mkubwa katika utekelezaji wa bajeti ya serikali ameonyeshaa uwezoo wowote katika hili??

naomba tuwachambue waliowahi kuongoza wizara hii na tija yao kwa umma.
 
Nilimpenda sana Marehemu Steven Kibona kwa yeyote atakaye andika habari za mawaziri hawa, nitafurahi kuiona cv yake na mchango wake katika nchi hii
 
prof. mbilinyi alianza vizuri sana kuimarisha uchumi ila akaja kuangushwa mbele kidogo na tamaa ya rafiki yake mporogomyi wa kasulu:dance:
 
mawaziri wetu wa fedha toka uhuru ni hawa hapa:

1. Ernest Vassey 2. Paul Bomani 3. Amir Jamal 4.Edwin Mtei 5. Cleopa Msuya 6. Stephen Kibona 7. Prof.Kighoma Malima 8. Lt.Col.Jakaya Kikwete

9. Prof.Simon Mbilinyi 10.Daniel Yona 11. Basil Mramba 12. Zhakia Meghji 13. Mustafa Mkulo
 
Kwangu mimi ni Hayati Steven Kibona na Amir Jamal.........Walikuwa wazalendo wa kweli hawa
 
Kibona alifanya kazi ya kupunguza ushuru hasa wauingizaji mali nchini kiasi ilikuwa bora kulipa kodi seriklani kuliko mfukoni kwa Customs officers.
 
Back
Top Bottom