Nani amewahi kushitakiwa na kufungwa kwa kuvuruga uchaguzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani amewahi kushitakiwa na kufungwa kwa kuvuruga uchaguzi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaa la Moto, Nov 5, 2010.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Jana wakati wa kujibu maswali kwenye mkutano na waandishi wa habari Professor mmoja mzee mwenye nywele nyingii jina sikulijua, alisema kuwa nchi ya Tanzania imesifiwa sana na wadau wa nje kwa utaratibu na sheria walizojiwekea katika tume kuhusiana na tume.
  Kisha akasema sheria ya mtu anayevuruga uchaguzi ni kali kiasi hata wadau wa nje waliwashangaa. Lakini shida niliyonayo ni kuwa pamoja na kuwa na sheria nzuri masikioni mwa wadau wa nje na kwenye karatasi sheria hiyo inatusaidia nini? Nilitegemea kusikia waandishi wetu wakiuliza swali kama hilo. Badala yake waliendelea kuuliza maswali yale yale (repeatable questions).

  Ningelikuwa karibu ningewauliza maprofessor wa tume, je tangu sheria hiyo itungwe ni nani ambaye amewahi kufungwa au kutozwa faini ya sh milioni 2 kama alivyokuwa anajaribu kutushawishi yule msomi wa nywele nyingi?

  Je tume wanataka kutuambia hakuna mtumishi wa tume au wakala wake ambaye amewahi kuvuruga uchaguzi? Na akisema hakuna swali linalofuata lingekuwa je hizi kesi ambazo mahakama imewahi kuthibitisha kuwa tume ilikosea nani alikuwa held responsible? maana sehemu nyingine ilibidi uchaguzi urudiwe na kugharimu pesa nyingine nyingi za taifa hili. Je nani aliwahi kupewa adhabu?

  Basi kama kweli sisi ni mfano bora katika sheria, basi pia sisi ni mfano bora wa nchi iliyo na sheria zisizo na mashiko. Hakuna maana yoyote kuwa na sheria ambazo hazifanyi kazi.

  Labda wenzangu nyie mwajua nani aliwahi kuumwa meno na sheria za tume kwa kufungwa au kulipa faini kwa kuvuruga uchaguzi?
   
Loading...