Nani amewahi kupata laana kwa kupiga/kutukana wazazi?

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,527
3,801
Wakuu,

Nimekuwa nikisikia sana swaala la kwamba mtu akitukana/ kupiga au akikataa kusaidia wazazi anaweza pata laana kama kufukuzwa kazi, kuwa kichaa au kufariki kabisa.

Binafsi namfaham kijana mmoja alikuwa anasoma UDOM, pindi tu alipofika chuo alianza dharau kwa baba yake mzazi (hakuwa na tatizo na mama yake).

Kijana huyo mzee wake alistaafu kazi Tazara hivyo alikuwepo tu, katika ugomvi na mzee wake siku moja alimtukana mzee wake na kumwambia yupo yupo tu anashinda ndani kuanzia asubuhi mpaka jioni na hana msaada kwa familia (ilitamka maneno haya nje ya nyumba, akiropoka na watu walisikia huku kila mtu akishika kichwa).

Kijana aliendelea na masomo yake lakini ilipofika June/ July, 2011 ikiwa ni kama miezi sita baada ya kumkashifu mzazi wake hadharani kijana huyu alishiriki kwenye mgomo. Baadae chuo cha UDOM kilitoa orodha ya watu waliokuwa chanzo cha mgomo na hivyo kufukuzwa chuo, kijana huyo alifukuzwa chuo na kurudi nyumbani.

Watu wengi mtaani walisema hiyo ni laana toka kwa mzazi wake. Lengo la uzi huu ni kutaka kukusanya shahidi mbali mbali zinahusianisha baadhi ya matukio katika maisha ya watu na kutukana au kutosaidia wazazi wao, je umeshawahi kushuhudia kitu cha namna hii?? lete mambo
 
Ninachojua, milango ya baraka hujifunga unapo kosa adabu kwa wazazi wako. Kuna baraka hutoka kwa wazazi wetu kutokana na maneno yao kwetu. Wazazi waki kufurahia baraka hukufuata. Ila haimaanishi kwamba huto toboza kimaisha hata kama hawajakubariki, ila kuna vitu mtu atavikosa. Mzazi hana uwezo wa kulaani, kama amekiweka tumboni mwake na kuangaika na wewr hawezi fanya hivyo, ata hudhunika kama mzazi au anaweza hata akasema vibaya kwa ajiri ya hasira
 
Mzazi akikulani mfano baba ,magonjwa kwako hayatakoma hususani kichwa kuuma na mwishowe kuwa kichaa,na na laana ya mama huwezi fanikiwa hatakidogo utakuwa wakutangatanga.kumbuka (mheshimu baba na mama upate heri na maisha marefu)najamii yote
 
Ni kuheshimiana tu mtu yeyote anaweza kukulaani na laana ikakushika,
Na anaeadhibu ni Mungu tu hayupo mzazi ambaye kakuhangaikia maisha yake yote na eti akulaani kisa umemjibu mbofu hayupo mzazi wa hivyo hasa mama ni ngumu mno kunuwia kwa kumuombea mabaya mwanae wenye uwezo wa kulaani fastafasta tu huwa ni ndugu MF shangazi mjomba mama wadogo na baba wadogo
 
Baba yangu hua anasema maneno magumu hadi napata mawazo kua ni baba yangu kweli! Ila basi Tu yeye mwenyewe anadai hanilaaini anasema kilichoko moyoni
 
Jaribu wewe utaona mwenyewe...! Ila ujue sumu haijaribiwi kwa kuilamba..
 
Wakuu,

Nimekuwa nikisikia sana swaala la kwamba mtu akitukana/ kupiga au akikataa kusaidia wazazi anaweza pata laana kama kufukuzwa kazi, kuwa kichaa au kufariki kabisa.

Binafsi namfaham kijana mmoja alikuwa anasoma UDOM, pindi tu alipofika chuo alianza dharau kwa baba yake mzazi (hakuwa na tatizo na mama yake).

Kijana huyo mzee wake alistaafu kazi Tazara hivyo alikuwepo tu, katika ugomvi na mzee wake siku moja alimtukana mzee wake na kumwambia yupo yupo tu anashinda ndani kuanzia asubuhi mpaka jioni na hana msaada kwa familia (ilitamka maneno haya nje ya nyumba, akiropoka na watu walisikia huku kila mtu akishika kichwa).

Kijana aliendelea na masomo yake lakini ilipofika June/ July, 2011 ikiwa ni kama miezi sita baada ya kumkashifu mzazi wake hadharani kijana huyu alishiriki kwenye mgomo. Baadae chuo cha UDOM kilitoa orodha ya watu waliokuwa chanzo cha mgomo na hivyo kufukuzwa chuo, kijana huyo alifukuzwa chuo na kurudi nyumbani.

Watu wengi mtaani walisema hiyo ni laana toka kwa mzazi wake. Lengo la uzi huu ni kutaka kukusanya shahidi mbali mbali zinahusianisha baadhi ya matukio katika maisha ya watu na kutukana au kutosaidia wazazi wao, je umeshawahi kushuhudia kitu cha namna hii?? lete mambo
Waheshimu baba yako na mama yako, hii ni amri ya kwanza yenye ahadi. Dhambi zote zina laana, hii ya kumtukana mzazi ina ziada maana umevuka mpaka. Nina ndugu yangu alipata matatizo makubwa kutokana na laana ya mzazi, maisha yake yalikuwa magumu wakati ni msomi na ana kazi yenye mshahara mkubwa.
 
Laana haiji haraka kama mwanga wa radi, bali huanza taratibu na kuna uwezekano isikupate wewe ikaenda kuupata uzao wako wa mbali
 
Ni kuheshimiana tu mtu yeyote anaweza kukulaani na laana ikakushika,
Na anaeadhibu ni Mungu tu hayupo mzazi ambaye kakuhangaikia maisha yake yote na eti akulaani kisa umemjibu mbofu hayupo mzazi wa hivyo hasa mama ni ngumu mno kunuwia kwa kumuombea mabaya mwanae wenye uwezo wa kulaani fastafasta tu huwa ni ndugu MF shangazi mjomba mama wadogo na baba wadogo
hata wazazi wa kuzaa wapo wako hivyo, ila basi
Muhimu ni kuheshimu wazazi wako no matter what situation you are going through
ukiona unashindwa weka maji mdomoni usiongee nao.
 
Yes wapo wazazi akikwambia hiki ukambishia kidogo huyo anaanza kuongea ovyo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom