Nani amewahi kula hii kitu?

Wanyamwezi tuna mboga yetu inaitwa nsansa na nyingine nswalu hizi nyingine huwa zinachanganywa na uyoga aiseeh zikipikwa huwa ni tamuu hasa ikiungwa na karanga weeh ugali wa dona uliochanganywa na Muhogo iiggh acha tuu tuambiwe tunabeba mizigo mizigo maana tunakula vinono.

Mwaah wanyamwezi wenzangu aka wakadama.
Daaah aisee nsansa majani ya kunde yanachemshwa then yanakaushwa.
 
Mashroom naziogopa nliona kuna kipindi cha hospital ER kuna couples walipata athari mbaya kutokana na kula aina flani ya mashroom
 
Duh tangu nihamie Dar sijawahi kula tena hiyo kitu...mara yamwisho kuila ni mwaka 2003 kule Sengerema kwa bibi. Tamu sana,japo zingine ni za sumu...so nilikuwa nikienda porini kuvuna ninazi identify kabisa....ile ni sumu, ile mboga, ile changa mno, etc. Unakuta yamejiotea tu, konokono wamejikinga chini huo mwanvuli. Nafika nang'oa, konokono anajipanga upya

Hahahaaa konokono atajiju


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom