Nani amelitendea haki Jukwaa la Michezo kwa mwaka 2021?

Satoh Hirosh -Unazi uendelee, sema mwanangu inabidi uhame huko kwa makolo kwasababu hujazaliwa nao ila tunaendelea kufarahia michango yako ndani ya jukwaa letu na kuishi kama familia

Mwifwa -Moja kati ya watu wanaonifanya niendelee kuwepo jukwaa hili kwa fact zao konki za michezo

Dabil -Ukiondoa unazi ulionao kwa makolo ila tunafurahia uwepo wako mkuu ktk jukwaa letu
Pamoja sana mkuu ,Ila kumbuka damu pia ni nyekundu
 
JF ktk jukwaa la Michezo imekuwa ni sehemu iliyotufanya tusijikie wapweke kabisa, Wanachama wafuatao wamelifanya jukwaa hili kuwa sehemu salama zaidi ya kuwepo Jf:-
Scars-Mtu wa kutoa changamoto ktk maada mbalimbali za kimichezo na mnazi kweli wa Simba SC

ESPRESSO COFFEE -Nashukuru kwa kuanzisha kwako kwa nyuzi za live updates za michezo mbalimbali ya ligi kuu ya Tanzania Bara

demigod - Tunashukuru kwa nyuzi zako za kufikirisha kuhusu michezo na kutoa changamoto ktk mada mbalimbali pia kwa unazi wako kwa timu ya Dar es Salaam Young Africans


ChamasonMorisonBwalyason -Tunashuru kwa uchangiaji wako uliotukuka ktk jukwaa letu la Michezo humu JF na pia kwa unazi ulionao kwa Simba SC

NAWATAFUNA -Tunashukuru kwa jitihada zako za kuchangamsha jukwaa hili na pia kwa unazi wako kwa Simba Sc

denooJ-Tunashukuru kwa nguvu zako ulizoweka ktk jukwaa hili la Michezo na uchangiaji wako uliotukuka na hongera kwa unazi wako kwa Dar es Salaam Young Africans

Nyamizi - Tunashukuru kwa unazi wako uliotukuka kwa Simba SC na uchangiaji wako mzuri ndani ya jukwaa hili na kujihisi sisi ni familia moja

Narudi tena kuendelea kutoa shout out kwa wanachama wote waliofanya jukwaa hili kuwa bora zaidi
Wabheja sana mtani
 
Castr, Willjr,Insigne,computeraresnal, Relief Mirzska, Nyamuswa hawa and some few others wanalitendea haki jukwaa letu la Arsenal.
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom