Megawatt B
JF-Expert Member
- Aug 23, 2011
- 259
- 69
Wapendwa, tukio la siku hizi mbili timu zetu kongwe za Simba na Yanga kucheza pale Chamazi zimenipa fikra ya kutaka kujua nikiwa shabiki wa timu hii Simba Sports Club. Kwa muda mrefu viongozi wa timu ya Simba aka Mnyama, Wekundu wa Msimbazi, wana sema wana eneo(kiwanja) eneo la Bunju ambalo litatumika kujenga uwanja huo. Naomba yeyote aliewahi kuona eneo hilo anijuze lipo sehemu gani. Mimi nipo Bunju, nimezunguka Bunju A na B mpaka Mabwepande kutokea Mapinga hakuna aliyesema pori lile ndilo eneo la wana Msimbazi ambalo wafadhili "WATURUKI" inasemekana watasaidia kuporomosha ka min Emirates hapo! Msaada tafadhali