Nani amefika equatorial Guinea? Nimesikia rais wao amekaa miaka 40 madarakani jee maendeleo yakoje huko?

deo paul555

JF-Expert Member
Oct 22, 2018
1,405
520
Habari wadau,nimesoma sehemu kua nchi hiyo rais wao amekaa miaka 40 je katiba yao ikoje na maendeleo ya nchi hio yakoje? Mwenye kufahamu nchi hiyo nisaidie siifahamu vizuri karibuni.
 
Habari wadau,nimesoma sehemu kua nchi hiyo rais wao amekaa miaka 40 je katiba yao ikoje na maendeleo ya nchi hio yakoje? Mwenye kufahamu nchi hiyo nisaidie siifahamu vizuri karibuni.
mkuu you can google that county pls, kwa swahili unaweza kugoogle hio taifa na ukajisomea weyewe, sasa si katika miaka ya 60s na 70s , google imefanya kazi iwe rahisi mkuu
 
hatutaki huu upuuzi na usifikiriwe wala kujaribiwa ni laana na ushetani na mwisho wake hua sio mzuri
 
Nilifika kisiwani Bioko ambapo ndipo ulipo mji mkuu wa Equatorial Guinea unaoitwa Malabo mwaka 2017.
Kiujumla nchi yenyewe ni ndogo kieneo na ina wakazi wachache sana. Maana wakati huo kulikuwa na raia kama Milioni moja na laki tatu.
Siasa zao ni za chama kimoja huku ukoo wa Nguema ukiwa ndio umeshika hatamu. Kuna makabila mengi ila kabila la Nguema ambaye ndiyo rais lina karibia asilimia 90 ya raia wote hivyo wana ushawishi mkubwa wa kuamua maamuzi ya nani awe au aendelee kuwa rais.
Rais na makamu wake wa rais ni wanafamilia lakini pia mawaziri wengi ni kutoka katika familia moja.
Hali ya uchumi ni mbaya licha ya nchi hii kuongoza katika kupata mapato kutokana na biashara ya mafuta.
Wananchi wana hali za kawaida tofauti na familia za viongozi.
Ila kuna vibinti vyeusi virembo vya kutosha hapo Malabo.
Hawa raia wa nchi hii ni wapole hatari.
 
Back
Top Bottom