Nani amashindwa katika uchaguzi wa arumeru- ccm kama chama ua sioyi kama mgombea? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani amashindwa katika uchaguzi wa arumeru- ccm kama chama ua sioyi kama mgombea?

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by HISIA KALI, Apr 2, 2012.

 1. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tangu kutangazwa kwa ushindi wa CHADEMA kule ARUMERU kumekuwa na hoja mbalimbali hasa kutoka kwa upande ulioshindwa kueleza sababu za kushindwa kwao. Hoja hizi ninaweza kuziweka kwenye makundi makubwa mawili. Moja ni kuwa CCM kama chama ndicho kimeshindwa na CHADEMA. Pili, Sioyi kama mgombea ndiye ameshindwa na Nassari.

  Lakini mimi kwa tathamini yangu ya haraka ninaona hoja zote zinaweza kuwa na ukweli fulani ndani yake. Lakini hoja ya kuwa CCM kama chama cha siasa ndicho kimeshindwa naina ina mashiko zaidi. Sababu kubwa ni kwamba CCM imepoteza mvuto kwa wapiga kura. Kitu kinachowapoza CCM ni hali mbaya ya maisha wanaishi wananchi wengi kwa sasa. Wananchi wanaona kwa CCM na serikali yake imewasahau, inawakumbuka tu wakati wa kampeni. CCM inatoa ahadi nyingi sana kwenye kampeni wakati ikijua kuwa sio rahisi kutekeleza. Kwa mfano Mhe Kikwete mwenyewe katika uchaguzi uliopita alitoa ahadi lukuki na zingine kama mtu ana akili ya kawaida tu anaweza kugundua hawezi kutekeza.

  Pia huko Arumeru CCM kupitia kwa Lowasa ilikiri yeye kushindwa kutatua matatizo ya ardhi na maji katika jimbo la Arumeru. Kibaya zaidi Lowasa kwa maneno yake mwenyewe alisema uchaguzi huu mdogo umeipa CCM nafasi ya kujua matatizo ya wananchi wa ARUMERU. Hii ni kauli ya kushangaza kabisa na ni makosa makubwa kisiasa. Huwezi kuwaambia wananchi hivyo wakati CCM ndiyo imetalawa jimbo hilo tangu uhuru miaka 50 sasa, eti uchaguzi huu ndio wamepata nafasi ya kujua matatizo ya wananchi. Hii kwanza haikuwa nafasi hata ya kutoa ahadi bali kueleza mafanikio ya CCM katika kuboresha maisha ya wananchi na mikakati mengine ya kuleta maendeleo zaidi. Ahadi za kila wakati bali utekezaji zimepitwa na wakati.

  Zaidi, CCM ilishindwa kama chama kujikita kwenye sera za kutatua matatizo ya ARUMERU badala yake iliendekeza siasa zake za kizamani za kutoa matusi mpaka ya nguoni tena mbele umati wa watoto wadogo kabisa. Hawakujua kuwa wapiga kura ni wananchi ambao walikuwa wanawatukana. Hoja ilikuwa ni kuwashashi wananchi ili wabadili misimamo yao na kupiga kura CCM. Hii ya kuwatupia matuzi ni kuwachochea wawe na hasira zaidi ya CCM. Pia, visa vya kusema mambo ya uongo ni kosa la kisiasa mbele ya wananchi. Uongo wa wazi wazi kunawafanya wananchi kupoteza imani na chama kwani hawazi kukiamini chama kinachoongozwa na viongozi waongo.

  Sasa uchaguzi umekwisha na mshindi ameshapatika. Na amini tutaona mengi sana kutoka ndani CCM mpaka kufika 2015.
   
 2. makeyzan

  makeyzan Senior Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  za mwizi ni arobain na tunasema ccm kushiney na arobain zao zimeshafika laada wamwombe nelson mandera aje agombee 2015 ndio tuludishe imani.
   
Loading...