Nani aliyewaambia na kuwadanganya hawa Wahubiri kuwa abiria wa mabasi ya mikoani ni wakosaji, mapepo na tunahitaji kuhubiriwa nao tukiwa safarini?

Kinachonikera ni uwongo wanaotumia mwingi(Mwingine mara hoo nimeacha kazi flani nimeamua kumtumikia Mungu Wakati hakuna lolote. Siku moja nilimfuma mmoja nlosoma nae akalamba F zote form Iv na namfaham fika namkuta kwenye gari anahubiri alishawahi kuwa meneja wa benk eti sauti ya bwana ikamwambia aokoke.

ALAFU WANAJAZA WATU HOFU SANA.
Anaaza taja taja ajali zilizowahi toke kiasi kwamba kama huna imani yakutosha unaeza ona ndo unaenda kufa. Sababu ya kujaza hofu watu ni ili ukifia muda wa kutaka sadaka utoe kubwa.
Mnhuuu hapo kwenye sadaka
 
Ajabu Sana,mbona hamuwakandii wanaoingia kuuza Korosho na juisi?kwani uliwaambia una shida nazo?
VP kuhusu wale wanaouza bidhaa kutoka kampuni za uingereza Kama dawa za meno na fangas?
 
Ajabu Sana,mbona hamuwakandii wanaoingia kuuza Korosho na juisi?kwani uliwaambia una shida nazo?
VP kuhusu wale wanaouza bidhaa kutoka kampuni za uingereza Kama dawa za meno na fangas?
Korosho,juisi,dawa za meno nk ni mahitaj ya muhimu. Kuhubiriwa sio kitu muhimu kiviiiiile. La sivyo pale Aljazeera wangejenga na kanisa
 
Ndugu yangu kaa kimya. Kwa vile tu hujui hukumu ijayo na moto wa milele. Ungekuwa na ufunuo huo, nawe ungekuwa mhubiri mkubwa mno wa kuwasaidi watu wasiende jehanum. Pili Mungu hana dini. Waislamu, wakristo, wapagani wote wanatakiwa kusikia injili. Biblia inasema " Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanae wa pekee ili kila mtu amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele." Kwa hiyo tunatakiwa kutambua hayo kwamba kila mwanadamu anatakiwa kujua haya. Kwa vile wewe ni muislamu unaona kwamba haya hayakuhusu. Yanakuhusu sana rafiki yangu.
 
Back
Top Bottom