Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,319
- 33,125
Nani Aliyepanga Mishahara Hadi Sh. Mil 40 Kwa Mwezi?
MIONGONI mwa mambo ambayo Rais Magufuli anastahili kupongezwa na Watanzania waadilifu – bila kujali ‘kambi’ zao – ni ujasiri wake wa ‘kuifyekelea mbali’ na kuipunguza mishahara ya baadhi ya waajiriwa serikalini na taasisi za umma iliyokuwa inafikia hadi Shilingi milioni 40 na zaidi kwa mwezi!
Wiki iliyopita kulikuwa na habari kwamba mishahara ya aina hiyo imefyekwa na serikali ya Rais Magufuli na kwamba hakuna Mtanzania anayefanya kazi serikalini na taasisi za umma atakayepokea mshahara zaidi ya Shilingi milioni 15.
Pamoja na hatua hiyo kupongezwa na mamilioni ya maskini wa nchi hii ambao hutembea bila viatu, wakanywa uji usiokuwa na sukari na wakachangia maji ya kunywa na punda katika mabwawa, swali kubwa hapa ni: Nani huyo aliyewapangia watumishi wa umma mishahara hiyo ya mamilioni na wengine akawapangia Shilingi laki mbili (200,000) kwa mwezi?
Ni ajabu kwamba serikali ambayo ndiyo ilibidi ionyeshe mfano mwema kwa waajiri wengine katika sekta binafsi kuhusu mgawanyo wa haki wa mapato na raslimali za taifa kwa wananchi wake, kwa miaka nenda-rudi imekuwa msitari wa mbele kuidharau kanuni hiyo tukufu.
Hii ni ishara ya wazi kwamba nchi ilikuwa imetopea katika dhuluma na ukatili. Ni ufunuo wa wazi kwamba nchi ilikosa wasimamizi waadilifu. Ni dhahiri uongozi wa kiadilifu ulikoma wakati wa Mwalimu Julius Nyerere ukaibuka tena wakati wa Dk. John Magufuli aliyetufumbua macho kuhusu uozo na dhuluma kibao ambazo wasomi na wajanja wa nchi hii wamekuwa wakiwafanyia Watanzania wenzao.
Tumefikia hatua ya ‘mamishahara’ ya aina hiyo kwa vile hapakuwa na kiongozi aliyekuwa anauonea aibu au uchungu umaskini wa Watanzania. Walioingia madarakani waliona wamepata bahati ya kujinufaisha, wakaisahau amri kuu ya Mungu ya: Mpende jirani yako!
Wakawasomesha watoto wao shule za ‘bei mbaya’ wakati watoto wa malofa wakisoma shule duni katika misitu ya Geita na Handeni, wakafurahi kusafiri kwa ndege wakati wengine wakisafiri kwa miguu, wakafanya harusi za mamilioni ya fedha kwao, watoto na wajukuu zao wakati Watanzania wenzao hata kuku mmoja wa Krismas hushindwa kununua!
Yote hayo yanawakumbusha waadilifu wote kwamba Afrika si maskini bali ina umaskini wa viongozi waadilifu na makini! Afrika ina kila aina ya utajiri ambao ungeifanya kuwa Bustani ya Eden iwapo ingekuwa na viongozi waadilifu.
Kiongozi ‘siriazi’ hatakubali uongozi wake utoe mshahara wa Sh. 45,000,000 kwa watumishi fulani na Sh. 200,000/= kwa watumishi wengine serikalini na taasisi zake – hata kama kuna tofauti za aina gani katika viwango vya elimu na utaalam, kwani masuala ya tiba, malazi, chakula na kadhalika wote wanakutana nayo mitaani.
Tofauti ya Sh. 45,000,000 na Sh. 200,000 katika mishahara ni kubwa mno hata malaika wa mbinguni hawawezi kuikubali. Kukubali tofauti ya aina hii kwa watu wanaoamka wote pamoja asubuhi kwenda kuwahudumia wananchi wenzao hospitalini, jeshini, shuleni, benki, na kadhalika, hakika ni kufanya dhambi! Ni kwa vile wote hao wana thamani sawa katika kuitumikia jamii.
Lakini, yote hayo yamefanyika mbele ya Watanzania wote, wakiwemo viongozi wa dini, wazee na vijana ambao wameiona dhuluma hii na wakaendelea kukaa kimya wasijue kwamba ndiyo huzaa ‘Panya Road’ na matatizo mengine. Ni kwa sababu kile alichotupa Mungu katika nchi yetu, tangu mbuga za wanyama, madini ya Tanzanite, dhahabu na kadhalika, vinafaidiwa na wachache kwa kisingizio kwamba walipoteza muda mwingi wakiwa darasani!
Wasomi wanasahau kwamba wananchi wenzao nao hupoteza muda wote wa maisha yao wakilima mpunga na mahindi ambayo kila mtu anavitumia kila siku.
Pamoja na kumtakia kila la heri Rais Magufuli katika kutufumbua macho na kuibomoa msingi yote ya dhuluma iliyodumu miaka kibao, safu hii inamwambia wazi kwamba uongozi uliomtangulia ndiyo uliotufikisha katika Tanzania aliyoikuta wakati anaingia Ikulu!
Mungu anawaona!
Mwandishi: Walusanga Ndaki
GBP.