Nani aliyemnyonga kamanda wa Polisi Zanzibar?

Gavana

JF-Expert Member
Jul 19, 2008
33,235
8,779
Hatuachi Kujiuliza: Nani walio mnyonga Camander Aziz Juma?

Asalamu aleikum ndugu zangu wazanzibari na watanganyika wa ndani na nje ya Zanzibar na Tanganyika. Ama mimi nimefika hapa na masikitiko makubwa sana ya kifo cha Camander Azizi Juma aliekuwa Mkuu wa Polisi Zanzibar. Innalillah Wainailahi Rajiun.

Camander Azizizi Juma alifariki Ghafla siku ya Alhamisi ya tarehe 6.Juni 2019 na kifo chake kimeacha masuali mengi yakujiuliza kwa sisi Wazanzibari au Watanganyika ambao hutetea HAKI na kukataa kuburuzwa na watawala waliopo madarakani.

Kamander Azizi licha yakuwa yeye alikuwa ni mkuu wa polisi lakini aliwahi kusomea Sheria lkatika masomo yake ya juu na kazi zake inasemekana alikuwa akifanya kwakutumia sheria zaidi kuliko Utashi wa Kisiasa na chuki zinazofanywa na Polisi wa Tanganyika na Zanzibar.

Kabla yakuendelea na mkasa huu wa mauti ya kijana wa Kizanzibari ambae aliwahi kuwa mkuu wa Polisi Zanzibar naalishika nafasi hio kwa miaka 4-5 kama sijakosea kabla yakuhamishiwa Tanganyika.

Katika kipindi chake cha uongozi hapa Zanzibar, ile piga piga ya Polic-CCM na kamata kamata ya Wazanzibari wasiokuwa na hatia nyakati za usiku zilipungua. Watu waliokuwa karibu nae wanatueleza kwamba alikerwa sana na Ukamataji wa Mashekhe wa Uwamsho na kupelekwa Bara. Kamander Azizi alikuwa ni msaidizi AG -kama PR kule Bara. Alikukamata nafasi hio hadi alipo kufa siku ya tarehe 6. Juni 2019 hapo nyumbani kwake Kibweni.

Marehemu kamander Aziz,i baba yake ni mtu kutoka Kaskazini Unguja na Mama yake marehemu ni mtu wa Ngwachani Pemba. Marehemu alilelewa katika maadili mazuri ya kiungwana ambayo yalimfunza mambo mengi ya Dini na Culture zetu za Kizanzibari. Family ya marehemu ni watu waliokuwa wenye heshma, kujitambua kama wao ni Wazanzibari na upendo miongoni mwa jamii za kizanzibari.

Sio hivo tu pia, marehemu Azizi alikuwa ni mtu aliekuwa amesomea Sheria sana na kazi zake zote alizokuwa akifanya alikuwa mara nyingi anafuata sheria kuliko kuchukua utashi wa kisiasa kama wanavofanywa Polisi wengine. Kwa upande mwengine tunaweza kumuweka katika kundi la Polisi waliokuwa wasomi na wasiotaka kuburuzwa buruzwa.

Kwanini tuwe na Conspiracy Theory juu ya kifo Chake?

Wakati wa Uongozi wa Kamander Aziz inasemekana kulikuwa na fitna kubwa na majungu yakipikwa ndani ya uongozi wake.

Kabla ya yeye kushika nafasi hio ya ukuu wa Polisi Zanzibar nafasi hio ilikuwa ikishikiliwa na Kamander Mussa umaarufu (Mussa Meno au Ronaldinho). Kutokana na habari ziliotufikia, inasemekana marehemu Azizi alikuwa akipingana na kamander Mussa Juma katika uendeshaji wao wa nafasi hio nyeti.

Nitawarudisha nyuma kidogo kwenye historia ya Mashekhe waliokamatwa Zanzibar ili niwape picha halisi ya kutofahamiana baina ya Kamander Azizi na kamander Mussa Meno. Inasemekana mwaka wa 2014-15 kulikuwa na mashekhe wengi wakikamatwa ovyo nakuwekewa ndani bila sababu zozote zile. Kuna siku Shekhe mmoja alikamatwa na askari polisi msikitini wakati akiwa anatoa Hutba. Shekhe huyu tunasikia hakuwa na kosa lolote lile, na wafuasi wake waliwahi kupigiana simu na kuzifukuza gari hizo 2 za polisi waliovalia kivita hadi walikomficha Shekhe yule.

Polisi hao kwanza walimkimbiza shekhe huyo sehemu za Mazizini na walipoona watu wameshakuwa wengi sana na bado wengine wanaitana ndipo polisi walipoamua kumchukua Shekhe huyo hadi Madema. Wafuasi wa Shekhe huyu walizifuata gari hizi hadi Madema na kuanza kuzongea katika kituo nakuwataka polisi wamuachie shekhe wao.

Inasemekana Amri ya ukamatwaji wa Shekhe huyo haujulikani unatoka wapi, ila wazanzibari wengi walihisi kwamba polic-CCM walifanya hivo kwa lengo lao walitaka lifanyike zogo na wapate sababu ya kupiga watu.


Kitendo chakukusanyika watu pale Madema kilimkera mkereketwa Mussa Juma ambae alikuwa ni Mkuu wa Polisi Zanzibar na marehemu Azizi alikuwa kama msaidizi na mkuu wa kituo cha Madema. Kwa habari tulizozipata na baadhi ya polisi waliokuwepo kituoni siku hiyo, walithibitisha kwamba kamander Azizi alipokea simu kutoka kwa Mussa Juma na kumuamrisha atoe Gari 4 zenye polisi wenye silaha ili wawatawanye watu hao kwa nguvu na mabomu ya washa washa.

Mzozo ulitokea hapo kwani Kamander Azizi alikataa kata kata kutoa gari 4 za Polisi wenye Silaha za moto, na alifika mbali kwakumwambia Mkuu wa Polisi kama unataka mimi nifanye hivo basi lete maelezo hayo kwa maandishi na sio kwa simu.

Pia alisikika akimueleza kwamba ni nani alietowa Amri yakukamatwa kwa Shehe huyu msikitini na kumleta Madema wakati mimi kama ni mkuu wa kituo cha Madema sina habari hio? …..

Hivo marehemu Azizi alimwambia Mussa Juma kwamba, yeye kama mkuu wa Kituo atahakikisha wananchi hao hawaleti madhara katika kituo hicho na si vyenginevo. Baadae marehemu Azizi alipandishwa cheo cha Mussa Juma na Mussa akahamishiwa Tanganyika na kupewa fupa jengine angongone. Hapo ndipo Sakata la fitna za Upemba na Uunguja, Ukaskazini na Ukusini zikaanza hapo na kuwiva hadi zikenda kupakuliwa Tanganyika kwa Mabwana zetu.

Inasemekana baada ya hapo Kuna kundi la Wahadimu wa Kusini walifurahishwa na kitendo hicho cha Azizi kuvuliwa Ukuu wa Polisi Zanzibar. Lakini haikufika muda mrefu Mkuu wa Polisi Tanganyika alimwiota bara na kumteuwa kuwa kama Msaidizi wake au Spoke person. Wazanzibari wale waliokuwa kundi la Mussa Juma hawakufurahishwa na uteuzi huo.

Kulitokea nini Siku ya Kifo Chake?

Marehemu Azizi alikuwa Zanzibar Kibweni siku ya kifo chake alhamisi ya tarehe 6.Juni 2019 ambayo ilikuwa ni sku ya pili ya Eid El Fitri.

Inasemrkana marehemu Azizi alikuwa Bara lakini alikuja nyumbani kwa ajili ya skukuu.

Mazingira ya nyuma ya nyumba ya marehemu kuna miti miti mingi aliopanda kwa ajili ya upepo. Habari zilizotufikia siku ya Alhamisi usiku saa mbili marehemu alikwenda kusali Isha na baadae aliporudi nyumbani kwake watu walisikia kama miti hio inakamatwa kamatwa majani kana kwamba kuna watu wanajaribu kupita ndani ya uwanja wa nyumba yake.

Marehemu alifikiria ni Wizi hivo alichukua tochi yake nakwenda kuangalia nje kama kulikuwa na watu au laa. Baada ya muda wa dakika kupita bila ya yeye kurudi wala kusikia kelele yoyote ile ndio family ilikwenda nje kumuangalia kwavile waliona kimyaa na yeye hakurudi ndani.

Lakini walipotafuta tafuta na kumwita hawakuona kitu wakadhani kwamba baada ya incident ile iliomtoa nje labda aliekuwa maeneo ya jirani kwavile ana uhusiano mzuri na jirani zake.

Baada ya masaa mawili kupita hajarudi ndani ndio family yake wakaanza kuingia wasi wasi na kupiga simu kwa majirani wa pale mtaani nakuuuliza. Ndipo wakatoka nje nakuanza kumwita nakumtafuta kwa tochi wakaona mwili wake ukininginia juu ya mti mmoja katika miti hiyo iliokuwa nyuma ya nyumba yake. Inasemekana marehemu alikuwa amefungwa mikono nyuma na (Ati) madaktari waliomchunguza wanasema kwamba shingoni kwake alikuwa na alama za mikono kamwa alikabwa Kibi kwanza kabla yakuwekwa kitanzi.

Wazanzibari wengi tuliosikia kifo chake tulisikitika sana na wale tulio ijuwa family yake hatukuweza kupata picha kama Azizi anaweza kujitundika mwenyewe. Ila kifo chake kinaambatana na utata wa Cheo chake alichokuwa nacho na asili yake anakotoka pamoja na Dini. Hakika Jeshi la Polisi Bara hawataki Zanzibar wawe na watu wazuri waliosoma katika nyadhifa za Polisi. Wao wanachotaka ni kuwaona Watu kama Kamander Mussa Juma ambae anaburuzwa.

Pili Azizi hakuwa kijana aliekuwa amehadaika na vyeo au cheo. Ni mtu alikuwa na kinaa pamoja na kujiamini na lile alilokuwa akilifanya. Kamander Azizizi anaambiwa kajinyonga mwenyewe. Lakini mtu aliejinyonga hawezi kujifunga kamba kwa nyuma.

Siku ya maziko yake tulitarajia Mkuu wa Polisi SIRO ahudhurie maziko yake lakini chakusikitisha ni Askari wachache sana wenye vyeo vya juu walihudhuria maziko yake.

Hata hivo Kwentu Sisi Wazanzibari haikutushuhulisha sana kwani wenyewe Tulitosha kwenda kumzika alhamdulilah . Allah amlaze mahali pema peponi, na kama amedhulumiwa basi Kamander Azizi atakuwa amekufa shahidi.

Watu wasiojulikana Sasa wameanza Stile mpya za Assacination na sio ile tulioifahamu katika kipindi cha nyuma cha tokea Utawala huu wa awamu ya tano kukaa madarakani.

Tukumbuke kwamba kuna watu wengi wasio hatia tayari wamepotea na wengine kushambuliwa kwa Risasi mchana kweupe na Serikali ya Magufuli imekaa kimyaa. Tunajuwa kwamba Polic-CCM wanatumika katika mauwaji na utekaji wa Watu wasio na hatia kwa vile tuu wanapingana na Utawala uliokuwepo.

Tunajuwa Kwamba bado kuna njama nyengine nyingi za utekwaji na Mauwaji unaandaliwa kwa ajili ya Viongozi wapizanni pamoja na wana sheria waliokuwa wamekataa kunyamazishwa.

Hata hivo Sisi Wazanzibari tunatakiwa tujiulize. Kwanini kifo cha mtu kama huyu kiwe kimyaa?

Kwanini hatuwezi kusema na kukemea. Inaonyesha kwamba sisi tumekuwa Wafu kiasi ya kwamba hata tuone maovu yanatendeka tunanyamaza kimyaa.

Tujuwe lilomfika mwezio leo huenda litakufika wewe kesho.

CHANZO: MZALENDO.NET
 
Tokea nikuwe na nianze kujua baya na zuri sijawahi Kusikia Mtu Kafa halafu Kifo chake kisihusishwe na Jambo lolote lile.

Na huenda huu ndiyo ukawa Utambulisho wa Uswahili Wetu ambao unatufanya kila uchao tubaki nyuma na hata tuchekwe na wale ambao wametoka huko Siku nyingi.
 
Si nafasi yangu kumhukumu yoyote yule, ila....

Hakuna muislam yeyote tena ambae ni askari polisi wa hapa Zanzibar (mzanzibar) ambae atabaki msafi huku anajua kabisa kwamba masheikh wameonewa na wanaonewa.

Nasikitika kufkiria kwamba familia ya the so called kamanda azizi itayapitia mabaya zaidi kuliko wanayoyapitia familia za kina farid na wenzao. Maana at least uamsho familia zao kuna watu wanazihudumia kwa kila kitu ila yeye ndio imetoka hivyo.

Hata hao waliokuwa wakimtuma kina sirro msibani hawakufika😀😀😀😀
 
Back
Top Bottom