Uchaguzi 2020 Nani alitegemea mikutano ya kampeni ya 2020 ingekuwa mitamu na imeegemea upande mmoja kuliko hata 2015?

lukoma

JF-Expert Member
Jul 1, 2013
2,995
2,245
Utamu wa kampeni za mwaka huu mawe yanarushwa upande mmoja tu tofauti na 2015. Mfano leo kalipua liinternational airpot la chotola. Tofauti na 2015, EL alitupa kigugumizi lilipokuja suala la ufisadi. Lakini 2020 TL ni very smart, very clean! Hizi sera sijui comedy za maendeleo hayana chama hata taa za barabarani zinawamulikia hadi panya, tuzaliane kwa kuwa matiti tunayo sio bure ni kukosa hoja wameshikwa pabaya.

Jana kwenye kipindi kimoja Star TV kuna kada wa CCM alikwenda na fomu ya madai ya kuvunjiwa nyumba yake na serikali ya CCM eti uthibitisho wa TL ni mwizi hawezi kuwa rais!! Akaulizwa mbona hii ni fomu ya madai yako ya kubombolewa nyumba na ubomoaji uliotekelezwa na serikali ya CCM alitumbua macho kama limjusi lilibanwa kwenye mlango.!!

Tunataka, Uhuru, Haki na Maendeleo. Huwezi wabomolewa wananchi nyumba bila kuwalipa eti maendeleo barabara ya lami, hii barabara kwa manufaa ya nani?
 
Wakuu wekeni ratiba ya Mzee wa ubweche... wengine tumechoka kelele.

Mzee wa ubweche ndiye so far anaonekana anatekeleza anachokiongea.

Screenshot_2020-09-01-19-10-40-1.jpg
 
Smart people are at work, hutaona vurugu, hutaona fujo, wagombea wote watalindwa, na wataanza kupendwa na hata kuahidiwa kazi ndogo ndogo baada ya uchaguzi na wahisani.

Watasema uchaguzi ulikuwa huru na haki na Tanzania kuna demokrasia . Upinzani umelogwa ushasahau tume huru mpaka sasa, hata fujo ikitokea itaonekana wao ndio waanzilishi.
 
Utamu wa kampeni za mwaka huu mawe yanarushwa upande mmoja tu tofauti na 2015. Mfano leo kalipua liinternational airpot la chotola. Tofauti na 2015, EL alitupa kigugumizi lilipokuja suala la ufisadi. Lakini 2020 TL ni very smart, very clean! Hizi sera sijui comedy za maendeleo hayana chama hata taa za barabarani zinawamulikia hadi panya, tuzaliane kwa kuwa matiti tunayo sio bure ni kukosa hoja wameshikwa pabaya.

Jana kwenye kipindi kimoja Star TV kuna kada wa CCM alikwenda na fomu ya madai ya kuvunjiwa nyumba yake na serikali ya CCM eti uthibitisho wa TL ni mwizi hawezi kuwa rais!! Akaulizwa mbona hii ni fomu ya madai yako ya kubombolewa nyumba na ubomoaji uliotekelezwa na serikali ya CCM alitumbua macho kama limjusi lilibanwa kwenye mlango.!!

Tunataka, Uhuru, Haki na Maendeleo. Huwezi wabomolewa wananchi nyumba bila kuwalipa eti maendeleo barabara ya lami, hii barabara kwa manufaa ya nani?
Ndio maana comedy hazina nafasi wakati huu kwani tumesha zichoka
 
Back
Top Bottom