GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Acha mvua ya maneno inyeshe na hata radi acha inyeshe zaidi ili ikawe fundisho kwa wengine Katika kuandika hadithi zao hapa duniani
Hoja hazipigwi Lungu bali hujibiwa kwa hoja"Hii ni nukuu ya Mrisho Jakaya kikwete aliyoitohoa toka kwa mwalimu Nyerere"
Nukuu ya Mzee mstaafu Rais Mwinyi"Maisha ya mwanadamu ni kitabu cha hadithi, ewe mwanadamu ukiondoka uache kitabu chenye hadithi nzuri"
Ni fikra mfu tu na mawazo mgando ndio unaweza kuacha kuwasemea wanasiasa Marehamu kwa mema au mazuri yao
Walikuwepo mitume na manabii, Kila siku habari zao zinasomwa misikitini na makanisani, Hawa manabii na mitume walishafariki karne nyingi zilizopita lakini habari zao zinasomwa kila jumapili na ijumaa kwenye makanisa, masinagogi na misikiti
Wewe mwanadamu ni nani tuache Kuongelea habari zako mbaya na nzuri ukiwa tayari ni mfu
Tunasoma habari za Petro, Yuda na Yohana kipindi cha Pasaka tabia na matendo yao na hakuna anayetukataza kwa kusema kitabu Chao kimefungwa hapa duniani
Tunasoma habari za Mtume Mohammad na hadithi zake tena watu Wengine wanazikejeli lakini hakuna aliyewazuia watu wasijadili hoja
Tunasoma habari za akina Pilato na Herode kwa utawala wao hakuna anayesema habari na vitabu vyao vimefungwa tuache wapumzike
Habari za Marehamu Nyerere, Mkapa, Magufuli huwezi kuzuia watu waseme, Hawa ni wanadamu watasemwa kwa wema na mabaya yao
Kwanini Magufuli anajadiliwa zaidi kwa mabaya na sio wema hii ni kutokana na aina ya utawala na mfumo alioutumia kwenye mfumo wa utoaji habari na maoni ya watu wake, Kila mtu aliguswa na utawala wa JPM kwa wakati wake,
Television zote na Radio ziliimba kishindo awamu ya tano tu, Walioimba kishindo ni mnyato walifungiwa
Acha mvua ya mjadala iwake na itawaka zaidi kwa lengo la kuueleza ukweli familia yake na Taifa kwa ujumla