Nani alimpa u-'SIR' George Kahama?, Tanzania wenye cheo hiki wapo wangapi?

Ninavyojua alipewa U-sir na Malkia wa Uingereza baada ya kukariri English dictionary word to word from A-Z
 
Mkuu hii tittle ya Sir alipewa na Malkia wa uingereza kwa kuwa mwafrika wa kwanza kuingia kwenye bunge la mkoloni mwaka 1958 akiwa kama mbunge wa Legico jimbo la Karagwe jimbo la ziwa magharibi na mwaka 1959 aliteuliwa kuwa waziri wa starehe na maendeleo kwenye serikali ya muda kabla ya uhuru wa Tanganyika! Alisoma shule ya Tabora then chuo cha Loughborough Uingereza! He is the only and only real Sir by little in Tanzania if not Africa just like Sir Alex and Bobby Robson and all real ones u know! Sio A.k.a ni real tittle ni mmoja wa unvalued treasures

longolongo za watu wa enzi za mumian na Rashid funika kikombe utazijua tu! Kahama u Sir wake ni nickname tu kwa vile uzungu ulikua mwing enz hizo so Nyerere kwa vile ni watani akawa anamuita Sir
 
Kwan baba rizy nchimbi na Mrema zile Phd zao nani aliwapa?? Mkishaniambia ndo turudi kwenye mada
 
Have always thought it was somethig of a nickname to him

That was more of a joke among friends that stuck than anything.

Sir Seretse Khama was knighted by the Queen as a genuine "Sir".

Sir George Kahama is as much of a Sir as Professor Majimarefu is a Professor.
 
Mkuu hii tittle ya Sir alipewa na Malkia wa uingereza kwa kuwa mwafrika wa kwanza kuingia kwenye bunge la mkoloni mwaka 1958 akiwa kama mbunge wa Legico jimbo la Karagwe jimbo la ziwa magharibi na mwaka 1959 aliteuliwa kuwa waziri wa starehe na maendeleo kwenye serikali ya muda kabla ya uhuru wa Tanganyika! Alisoma shule ya Tabora then chuo cha Loughborough Uingereza! He is the only and only real Sir by little in Tanzania if not Africa just like Sir Alex and Bobby Robson and all real ones u know! Sio A.k.a ni real tittle ni mmoja wa unvalued treasures


Acheni kudanganya watu bana! Kahama u Sir alipewa na Nyerere kwa kumtania tu kwani alikuwa mtani wake...angalieni kwenye google hakuna kitu kama hicho!! Hiyo ni kama ya asir Nature tu!
 
Jamani Hata Elton John Bwabwa lakini ni Sir Nyie Vipi mnababaikia u Sir! !
 
Jamani mwenye historia ya huyu mzee naomba atujuze na sisi tuweze kumfahamu vizuri maana nasikia anazichanga karata kumsaidia mtu mmoja mtaka urais 2015
 
Mkatoliki aliyeendelea!Ana wake 2.(J.K.Nyerere) anamiliki kampuni iliyoleta mkongo wa taifa seacom pamoja na Karamagi,Rostam.
 
Jamani mwenye historia ya huyu mzee naomba atujuze na sisi tuweze kumfahamu vizuri maana nasikia anazichanga karata kumsaidia mtu mmoja mtaka urais 2015
.
.
.
ndege ikaruka mara ya kwanza --- george akaguna...
ndege ikaruka mara ya pili -- george akaguna tena kwa sauti --mmmmnh (ule mguno wa kihaya)
iliporuka mara ya tatu -- nikamsikia george akipiga kelele -- maweeeee!!!!!

(RIP nyerere)
 
.
.
.
ndege ikaruka mara ya kwanza --- george akaguna...
ndege ikaruka mara ya pili -- george akaguna tena kwa sauti --mmmmnh (ule mguno wa kihaya)
iliporuka mara ya tatu -- nikamsikia george akipiga kelele -- maweeeee!!!!!

(RIP nyerere)

Sor naomba taarifa zake kama unazo inamaana alikuwa muhaya?
 
Jamani mwenye historia ya huyu mzee naomba atujuze na sisi tuweze kumfahamu vizuri maana nasikia anazichanga karata kumsaidia mtu mmoja mtaka urais 2015
Clement George Kahama, al-maarufu Sir. George, ni mtumishi wa umma aliyekuwa mtendaji mkuu na mwanasiasa aliye mahiri na makini, katika utendaji kazi kuanzia nyakati za Tanganyika kudai uhuru mnamo miaka ya 1950, hadi kujitawala mwaka 1961, na baada ya uhuru mpaka alipostaafu utumishi wake kwa umma si miaka mingi iliyopita.
Kwa hakika, ni nadra mwanasiasa kukiri mapungufu katika matamanio ya utendaji wake, hata kama msingi wa mapungufu yale haukuwa ndani ya maamuzi yake binafsi, isipokuwa ni mkakati wenye kuamuliwa na dola.
Hata hivyo, kwa kuwa mapungufu yale yalihusu matamanio yaliyotokana na utafiti wake, anachukuliaa ni mapungufu yake.
Viporo vyake hivyo ni pamoja na vva kiuchumi amnbavyo tutavijadili baadaye.
Kwanza tutazame ni jinsi gani Sir George aliingizwa kimyakimya katika harakati za kudai uhuru wa iliyokuwa Tanganyika, na katika mazingira ya aina gani, na nani alimwingiza na kwa sababu gani.
Wengi wanajua na kukiri ya kuwa, Sir. George Kahama alikuwa rafiki wa karibu wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambaragae Nyerere, ambapo chanzo cha urafiki wao, ndilo jibu la jinsi gani mwanasiasa huyo mkongwe, aliingizwa kwa faragha katika siasa, hususan mazingira yaliyohusika.
Kwa wale wanaotambua kwamba dhamira ya wakoloni kuwa, ni kuendelea kutawala na kunyonya makoloni, wana imani ya kuwa Mwalimu Nyerere alipopelekwa masomoni Uingereza kuboresha taaluma yake ya ualimu, ilikuwa ni mbinu ya wakoloni ya kuzima japo kwa muda, vuguvugu lake la kudai uhuru wa Tanganyika, na ndiko alikokutana na Sir. George Kahama akisoma pia.
Kahama alipelekwa Uingereza na Chama cha Ushirika wa Zao la Kahawa cha jimbo lililoitwa Ziwa Magharibi wakati ule, likiwa na wilaya za Bukoba, Karagwe, Biharamulo na Ngara, na sasa ni mkoa wa Kagera, ili kusomea taaluma ya ushirika na masoko kwa ajili ya maendeleo ya chama kile.
Katika kutimiza dhana yao ya kuzima harakati za Nyerere za kudai uhuru, na kwa vile hakuwa peke yake katika harakati zile, wakoloni walimpatia masurufu yasiyokidhi mahitaji yake akiwa masomoni, kusudi akose uwezo wa kuwasiliana na waasisi wenzake kwa kuwatumia nyaraka kwa njia ya posta.
Alipokwisha taabika kwa muda mrefu akisaidiwa na baadhi ya wanachuo wenzake kutoka Tanganyika waliokuwa katika vyuo mbalimbali vya Uingereza, ndipo alipodokezwa ya kuwa yupo mwenzao aitwaye Clement George Kahama katika chuo kingine kuwa, alikuwa na uwezo kifedha kutokana na kusomeshwa na chama cha ushirika wa zao la kahawa.
Mwalimu Nyerere alifurahi akawa na matumaini ya kusaidiwa, kwanza kwa sababu alikwishaona ushirikiano wa Watanganyika wengine, akajua hata Kahama atamsaidia.
Lakini kwa mujibu wa Sir George, tumaini la Nyerere lilizidishwa na ukweli kwamba, wote wawili ni watani wa jadi.
Tangu walipokutana mpaka waliporejea nyumbani baada ya kuhitimu masomo, gharama zote za kutuma nyaraka za kisiasa kuja kwa waasisi wa harakati za kudai uhuru, zilitolewa na Sir George, kiasi kwamba, hata wenye kujadili ni jinsi gani alipachikwa cheo cha Sir, wanadhani Nyerere kiutani huenda ndiye alimwita vile kutokana na mazingira ya msaada huo.
Kwa mujibu wa mazungumzo yangu na Sir George niliyofanya naye kwa nyakati tofauti kati ya mwaka 1987 na 1990, nikiwa naye Beijing, China alipokuwa Balozi wa Tanzania nchini humo, na mimi nikiwa mtangazaji katika Idhaa ya Kiswahili ya Radio China, Sir George alikatiwa hata kadi ya TANU na Nyerere akapelekewa Uingereza kwa njia ya posta.
Wote wawili, Nyerere na Kahama walipokwisha rejea nchini na kila mmoja akaripoti kwa mwajiri wake, Mwalimu Nyerere alijiuzulu kazi ya ualimu katika Shule ya Sekondari Pugu, Dar es Salaam kusudi aendeleze kikamilifu siasa za kudai uhuru, ambapo Kahama aliendelea na kazi katika chama cha ushirika wa zao la Kahawa jimboni Ziwa Magharibi (BCU), mjini Bukoba.
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alisafiri nchi nzima akishawishi wananchi waunge mkono madai ya uhuru, akawa amekumbana na mikikimikiki toka kwa watawala wa kikoloni, yakiwa ni pamoja na kushtakiwa Mahakamani kwa tuhuma ya kichochea uasi kwa utawala wa kikoloni.
Alipokwisha dai uhuru hadi katika Umoja wa Mataifa New York, ndipo Nyerere alipopewa fursa na watawala wa kikoloni mwaka 1958, ya kuunda Serikali ya Madaraka wakiwa na lengo la kuhakiki uwezo wa Watanganyika kujiendeshea nchi yao wenyewe.
Wakati inaundwa Serikali ile, ndipo Mwalimu Nyerere alipomwita Sir George kutoka Bukoba, ili ajiunge na Baraza la Mawaziri la Serikali hiyo, akamteua kuwa Waziri wa Ushirika na Masoko na mwenyewe (Nyerere) akawa Waziri Mkuu.
Baadhi ya mawaziri walioteuliwa walikuwa Paul Bomani, Chifu Abdallah Fundikira, Rashid Mfaume Kawawa, Solomon Eliofoo, Nsilo Swai, Said Maswanya, Dereck Noel Bryceson, Sir. Ernest Versey na Amir Jamal.
Serikali ya Madaraka iliendelea kuwapo sambamba na ya kikoloni na ilipofika Desemba 9, 1961 kama ilivyoahidiwa na Umoja wa Mataifa, Tanganyika ilitangazwa kuwa huru, na Baraza la Mawaziri lenye madaraka kamili likaundwa, Sir George akiwa waziri wa kwanza wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mbali ya nyadhifa za uwaziri katika wizara mbalimbali, Sir George alipata kuteuliwa kuanzisha taasisi nyeti za kimaendeleo, zikiwa ni pamoja na Shirika la Taifa la Maendeleo ya Viwanda (NDC); Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA); na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Kati ya maswali mengi niliyomuuliza Sir George pasipo nia ya kuyatumia kihabari, lakini yakawa yamedumu katika kumbukumbu zangu, ni pamoja na jinsi gani baadhi ya watendaji kama yeye, waliweza kubaki karibu na Mwalimu Nyerere mpaka alipong'atuka madarakani, na wengine kama yeye akawashurutisha wabaki kumalizia voporo vyake.
Kwa tabasamu lake lisilokwisha katika sura yake, Sir. George aliniambia ya kuwa, aliweza kudumu karibu na Nyerere kwa sababu mbili: Kwanza ni kwa kuwa alijuana naye wakiwa wanafunzi ugenini, kwa hiyo, waliunda ukaribu wa aina yake kwa jinsi walivyosaidiana. Lakini pili, ni kwa kumjua Nyerere matakwa yake katika nafsi.
Nilipomtaka anifafanulie hiyo sababu ya pili, alisema kwa kuwa Nyerere ni mzaliwa katika ukoo wa utemi wa kimila, alitawaliwa na dhana itokanayo na mienendo ya utemi.
Akasema mtemi, licha ya kuwa na washauri wake, lakini fikra ya mwisho hata ikitoka kwa washauri, mwenye nayo ni yeye.
Kwa hiyo, alipokuwa madarakani akishauriana na washauri wake ambao ni pamoja na mawaziri wa Serikali yake, uamuzi wake ukishagota mahali, kila mmoja anatakiwa awe makini na jinsi gani azidi kuchangia mawazo ili asitofautiane na uamuzi wake.
Aliendelea kufafanua kuwa, endapo mshauri ataamini kuwa wazo lake ni la busara, hana budi atafute wakati muafaka kama vile kumtembelea nyumbani kwake kwa matembezi ya kawaida, halafu akishamdokeza wazo lake na Mwalimu akaliona lina mantiki, likiletwa mezani kujadiliwa na washauri wengine, basi wazo lile linakuwa ni lake yeye Mwalimu, na si la mshauri husika.
Alinichekesha pale aliponipa mifano ya washauri wa Mwalimu ambao sitataja majina yao, kwamba baada ya mawazo yao kupokelewa na Nyerere yakawa yamefanyiwa kazi, walinong'ona kwa watu kuwa ni mawazo yao.
Mwalimu alipopewa habari juu ya ‘majigambo' ya watu waliompatia ushauri, washauri hao ukawa ni mwisho wa kuionekana kuwa karibu na Mwalmu.
Alisema ya kuwa kimsingi huo ndio mwenendo wa watawala karibu wote duniani.
Nilipenda kujua kwa nini yeye Sir George, aliteuliwa na Nyerere mwishoni mwa utawala wake kabla ya kung'atuka mwaka 1984, aende kuwa Balozi wa Tanzania China, ambapo alikwisha nidokeza mapema kabla ya kuwa alitaka naye astaafu.
Alinijibu ya alishindwa kumkatalia kwa sababu hakutaka kumkaidi Mwalimu wakati anapumzika.
Alikiri ya kuwa, uteuzi ule japokuwa aliupokea akijihisi kuchoka, lakini alijifunza mengi China kuliko mahali popote alikopata kuwa Balozi wa Tanzania.
Ni wakati huo alipopata wazo la kuifanya Zanzibar iwe kama Hong Kong ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini, kama kitovu cha biashara cha eneo hili, kama ilivyo Hong Kong yenyewe kwa eneo la Asia Kusini Mashariki na Mashariki ya mbali.
Lengo la Mwalimu Nyerere kumteua Sir George kuwa Balozi wa Tanzania nchini China ilikuwa ni kwenda kujifunza jinsi Wachina licha ya siasa yao ya ujamaa, waliweza kukaribisha sera za kibepari ili ziwasaidie kuboresha ujamaa wao, jambo ambalo linabainika dhahiri hivi sasa. Mwalimu alitaka mbinu hiyo itumike hapa Tanzania.
Jibu la jumla alilopata Sir George ni kwamba uwekezaji wa mitaji ya kigeni ilikaribishwa China bila kuacha ujamaa wake, na sasa taifa hilo limekuwa tishio kwa mataifa makubwa ya kibepari.
Taifa hilo limekuwa tishio kiuchumi wakati ujamaa wa nchi hiyo ungali palepale ukiungwa mkono na wananchi wake.
Sir George anasema kuwa, hata wakati utawala wa China unarudishiwa eneo la Hong Kong na Waingereza, China ilitangulia kuboresha miji yake ya pwani iliyoko mkabala na Hong Kong, kiasi kwamba mataifa ya kibeberu hayakufurukuta kuitambia China juu ya mji wa Hong Kong, kwa sababu miji ya Guanghjou, Zhuhai, Shengzhen na Shanghai, ilikwishakuwa na hadhi sawa na Hong Kong au kuizidi.
Sir George Kahama alimalizia mahojiano yake ya hivi karibuni kwa kusema kuwa, licha ya mazoea ya wanasiasa kutokiri mapungufu katika utendaji wao, lakini yeye anasikitishwa na kutokamilisha ndoto zake tatu anazoamini kwa umuhimu wake ulivyo, siku moja walioko madarakani watazitekeleza.
Ndoto hizo tatu ni pamoja na ileile ya kuigeuza Zanzibar kuwa Hong Kong ya eneo la Afrika Mashariki, Kati na Kusini; ya pili ni kuanzishwa kwa benki ya ushirika ambayo wadau wake wakuu watakuwa ni Vyama vya Kuweka Akiba na Kukopa (SACCOS); na ya tatu ni kuyafanya makao makuu Dodoma yawe ya kweli ili Serikali ihamishie kabisa makao yake huko.
Baada ya kurejea kutoka China alikokuwa Balozi na kuhamia kwa muda Zimbabwe, Sir George alianzisha Kituo Cha Uwekezaji Mitaji Tanzania, yaani Tanzania Investment Centre (TIC), kwa lengo la kuvuta mitaji ya ndani na nje ili kuzidisha maendeleo ya kiuchumi nchini, ikiwa ni sehemu ya mafanikio ya miaka 50 ya uhuru inayosherehekewa hivi sasa.
kwa sasa ni mwenyekiti wa SeaCom Tanzania

- See more at: Raia Mwema - Sir George, muasisi mkimya wa harakati za uhuru
 
SIR GEORGE KAHAMA ALIKUWA RAFIKI NA MTANI MKUBWA WA MWALIMU ..KWENYE HOTUBA ZAKE ALIKUWA AKIMUONEA SANA AKITAKA KUTOA MIFANO YA KUCHEKESHA ...

Alikuwa anasema hakuhangaika kujuwa dini za mawaziri wake ...siku moja akaamua kuwaambia watu wa usalama wamletee baada ya kuona dalili za udini......akakuta mkatoliki ni yeye na kahama tu ...ndipo akasema .." na ukatoliki wa Kahama rafiki yangu ni wa mashaka ....maana mwenzangu siku hizi ameendelea ana kina mama wawili.."

MWACHENI MZEE KAHAMA APUMZIKE NA MAJOZI YA KUFIWA NA MWANAYE JUDITH KAHAMA....I USE TO KNOW THE LADY AND HAD WORKED WITH HER ....SHE WAS SO KIND..
 
Back
Top Bottom