Mzukulu
JF-Expert Member
- Feb 14, 2020
- 1,401
- 2,631
ULINZI WAIMARISHWA DODOMA:
Dodoma: 07 Julai, 2020
Wakati vikao vya uamuzi vya Chama Cha Mapinduzi vikitarajiwa kufanyika Jijini Dodoma, ukiwemo Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama hicho, Jeshi la Polisi limesema limeimarisha zaidi hali ya ulinzi na usalama.
Mkutano mkuu utafanyika Jumamosi na Jumapili na utakuwa na kazi ya kuchagua jina moja la mgombea wa CCM wa uraisi kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Zanzibar.
Leo katika mkutano na waandishi wa habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, ametoa onyo kali kwa yeyote atakayejaribu kuleta fujo au utapeli wakati wa vikao na mkutano mkuu wa taifa wa Chama Cha Mapinduzi.
Aidha, Kamanda Muroto, amewatoa hofu wageni wote watakaohudhuria mkutano huo kuwa hali ya ulinzi na usalama wa mali zao, umeimarishwa zaidi.
uhurudigital
Najaribu Kukumbuka ni lini nimewahi kukutana na Statement kama hii ikielekezwa kwa Vyama mahiri vya Upinzani kama CHADEMA, CUF na ACT.