Nani alikabidhi madaraka ya Kufikiria kwa Serikali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani alikabidhi madaraka ya Kufikiria kwa Serikali?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MwanaHaki, Apr 24, 2009.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Apr 24, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Ndugu Wanabodi,

  Baada ya kutokea kwa mabadiliko ya hali ya hewa, yaliyoambatana na ukame uliosababisha, mnamo mwaka 1994, mgao wa umeme ulioisababishia Tanzania athari kubwa ya kiuchumi, kwani watu wengi walipata hasara kubwa, binafsi nilidhani lingetokea jopo la wataalam, kama vile wachumi na wanasayansi, ambao wangeishauri Serikali nini ifanyike, ili hata kama hali hiyo mbaya ya hewa ikijirudia, hatua za dharura ziwe zimekwishaandaliwa.

  Jambo hilo halikufanyika. Matokeo yake, ukaja ufisadi wa Richmond na majeraha mengine ya vita hii kali ambayo sitaki kuyataja hapa, kwa kuhofia kutonesha vidonda vyenu.

  Swali ninalouliza ni, baada ya kukabidhi madaraka ya utawala kwa Serikali, ye, tulikabidhi pia madaraka ya kufikiria? Jambo hili halikuhitaji mtu apewe ruksa ya kufikiria nini kifanyike, wala kuitwa atoe ushauri wake. Lilihitaji mtu, kama mtaalam, mwanasayansi - fizikia, uhandisi, elektroniki, mazingira, umeme, n.k. - ajitokeze na kusema nini kifanyike. Aandaye Mkakati Kazi, ambao ungefuatwa na Serikali, au ungekabidhiwa kwa Wajasiriamali/Wawekezaji wa Ndani, ambao wangeutekeleza.

  Wote mmejionea jinsi ambavyo TANESCO imeshindwa kufanya kazi yake. Haina wataalam wa kutosha, waliopo wamechoka hata akili zao. Najua baadhi yao wamo humu, wataona ninawaone. Lakini niwaulize. Je, umeme unazalishwa kwa njia moja tu, yaani ya kutumia nishati itokanayo na bidhaa za petroli (dizeli, gesi, n.k.)? Mbona hata siku moja sijawasikia wataalam wa TANESCO wakishauri njia mbadala za kuzalisha umeme zitumike, kama vile nguvu za upepo, au teknolojia ya Stirling (ambayo imezuiwa makusudi na Serikali ya Marekani pamoja na Jumuiya ya Ulaya, kwani itaiwezesha nchi hii kuacha kuagiza mafuta au kuchimba gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme)?

  Kwa mtazamo wangu, umefika wakati Watanzania (wazawa) waanzishe shirika mbadala la umeme, ambalo litatumia njia mbadala za kuzalisha umeme, likianzia na nguvu za upepo. Kampuni kubwa kama vile Suzlon na Vestas zimetengeneza wind turbines zenye uwezo wa kuzalisha 3.0 MegaWatt kila moja. Vestas wamefanikiwa kufikia kiwango cha 3.0 MegaWatts, zikinunuliwa 10 tu, hizo ni 300 MegaWatts, ambazo zinaweza kutosheleza kwa sehemu kubwa ya Tanzania Bara au hata Zanzibar yote!

  Ninawaomba wataalam wa Uhandisi wa Umeme wawasiliane nami kwa njia ya simu - 0786-019019 - ili tuanze Mkakati Kazi binafsi, wa kuangalia jinsi ya kusonga mbele.

  Penye Nia pana Njia, na Umoja ni Nguvu, bila kusahau, Kidole Kimoja Hakivunji Chawa!

  Tusikubali nchi hii kuwekwa rehani na mafisadi wa Dowans, Richmond, Songas na IPTL!

  ./Mwana wa Haki
   
 2. S

  Shelute Mamu Member

  #2
  Apr 28, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu Sophia Simba amedhihirisha kuwa ni mmoja wa Maafisadi wanaowapa KIBURI Maafisadi PAPA kwa kutumia madaraka makubwa aliyopewa Serikalini. Huyu mama ni yule yule aliyewadanganya na kuwashawishi wanawake wengi (hasa waliokuwa wanasali Efatha) kwamba kuna Msaada kutoka kwenye Shirika fulani la nje ambao alisema watawajengea nyumba za bei nafuu eneo la iliyokuwa Tanganyika Packers. Utaratibu ilikuwa unatoa kiingilio cha Tshs.46,000/= na unaanza kutoa fedha kila mwezi na kwamba watakao toa kiasi kikubwa ndio wangekuwa wa kwanza kujengewa nyumba za bei nafuu.

  Wanawake wengi wakaanza kutoa michango yao ambayo wengine zilifikia hadi milioni 3. Lakini mwisho wa siku hakuna kilichojengwa wala wanachama kuelezwa kinachoendelea. Kilichotokea ni kufunga ofisi ambayo walikuwa wanaitumia eneo la Kawe na kutokomea na fedha mabilioni za akina mama walala hoi hadi leo - zawadi aliyopewa na Serikali baada ya wizi wa kimasomaso kabisa ni kuwa Waziri !!! nchi hii kweli inatisha. HUYU ndiye anasimama kutetea MAAFISADI. Jamani ebu viongozi muogopeni Mungu. Kumbukeni siku ya kunyamaza kimya kwa Mkristo sana sana atakwenda na SUTI au Gauni moja safi fullstop na kwa Mwislamu hata alivyokula kabla ya kunyamaza vitakamuliwa - fikirieni hayo mambo kuweni na kiasi. Muogopeni Mungu - pigeni picha Paraparanda itakapolia - hivyo viti mtaviona vichungu na vitawaunguza.
   
Loading...