Nani Alihusika Na Maauaji Ya Aliyekuwa Rais wa Marekani John Kennedy 1963

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
image.jpeg
Tarehe 22 November 1963 ni siku aliyekuwa Rais wa Marekani wa 35 John F Kennedy aliuwawa kwa kupigwa risasi huko Dallas Texas Marekani. Rais Donald Trump amekubali ripoti ama mwenendo wa upelelezi wa mauaji ya kiongozi huyo aliyekuwa kijana sana kuchapishwa hadharani. Shirika la upelelezi la Marekani FBI na tume ya Warren Commssion zote zilitoa taarifa zao kuwa Oswald Lee ndio aliyekuwa muuaji pekee lakini kuna vikundi vingi vya haki za binadamu huko Marekani zinaamini njama ya kumuua Rais huyo ilipangwa na watu wasiojulikana. Aliyekuwa makamu wake L.Y. Johnson aliapishwa kuwa rais wa Marekani siku hiyo hiyo baada ya mauaji hayo mbele ya aliyekuwa mke wa Rais Kennedy Jaquelini Kennedy ndani ya ndege ya rais Air Force One.
Kwa taarifa zaidi ili kujua undani wa mauaji ya kiongozi huyo unaweza kutembelea website ya National Archives and Records Administration (NARA).
 
Back
Top Bottom