Nani alifungua mlango wa ndege iliyopata ajali ni hoja mfu, CHADEMA na Wanaharakati acheni utoto

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,160
1,493
Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa baadhi ya Wanachama wa Chadema tena wengine Viongozi mfano ni Sugu, Heche, pambalu na Wanaharakati wengi wakipinga kwa nguvu zote kuwa Kijana Majaliwa hakufungua mlango wa ndege iliyopata ajali hivi karibuni huko Bukoba.

Ni ukosefu wa hoja na upumbavu kulalamika kwa hili, hata kama ni kweli kijana Majaliwa hakufungua yeye mlango wa ndege, muhimu ni kuwa alikuwa wa mwanzo kabisa kusaidia manusura ajali, alifanya kazi kubwa ya kusaidia ndugu zetu, alipambana mpaka kutaka kuhatarisha maisha yake.

Haiwajengi kulalamika kwa hili ila nikuonyesha ukosefu wa hoja, hata kama mlango ulifunguliwa na wahudumu basi walifanya kazi yao na Mungu atawabariki kwa hilo.

Tanzania itajengwa na Watanzania.

Mungu ibariki Tanzania

Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Kweli ni upumbavu kama kweli wanabishania nani kafungua mlango wa ndege.

Ila wewe pia inaonyesha ni kijana wa hovyo.

Nimejaribu kuangalia mabandiko yako ya nyuma inaonyesha upo hapa kwaajili ya siasa uchwara za kiccm na kichadema.

Shenzi kabisa wewe.
Mkuu Texas Tiger kosa langu lipi sasa? Sinatumia Uhuru wangu kutoa maoni au kuna sehemu nimevunja sheria?
 
Kweli ni upumbavu kama kweli wanabishania nani kafungua mlango wa ndege.

Ila wewe pia inaonyesha ni kijana wa hovyo.

Nimejaribu kuangalia mabandiko yako ya nyuma inaonyesha upo hapa kwaajili ya siasa uchwara za kiccm na kichadema.

Shenzi kabisa wewe.
Hahaha.........!
 
Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa baadhi ya Wanachama wa Chadema tena wengine Viongozi mfano ni Sugu, Heche...
Mbona mnatutafuta lawama bure tuseme ya kwetu mtupe kesi, point ni hatuko tayari kukabiliana na dharura hasa kwa upande wenu nyie mlioshika hatamu. Madaraka mnayapenda lakini kazi ndio hamuwezi, zaidi ya kusifiana ujinga. Mnatengeneza agenda na propaganda zenu kututoa katika reli ili muendelee kufanya yenu. Mungu ambariki raisi hapa kwa lipi kwanza hakuwepo pili mmemwambia umri wa hiyo ndege, na ajali imetokeaje???

Au ndio mmempamba majaliwa zaidi na kusahau wahanga wa ajali yenyewe, vipi meshawalipa fidia na wao wamepoteza wapendwa wao, mali zao na muda wao ebu walipeni haraka na waiteni na bungeni ili muwasikie wenyewe manake hamtaki hata kusikia kutoka kwa waliokuwa ndani ya ndege. Mmetengeneza cinema yenu na mnatembea nayo, wahudumu si wapo kawaulizeni.

Hakuna anayewalalamikia nyie hamna baya endeleeni hivyo hivyo na mambo yenu dunia inawaona. Tanzania itajengwa na watanzania kweli ila viongozi na nyie mataga mnafanya kazi ya ujenzi wa nchi hii kuwa ngumu mno.
 
Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa baadhi ya Wanachama wa Chadema tena wengine Viongozi mfano ni Sugu, Heche...
Chadema kuna kipindi nilikuwa nawaona wanaleta changamoto na nilikubali hoja zao na ni ukweli Marehemu Sitta alikuwa akiwapa mambo mengi ya ndani na wakaweza kupanda kisiasa lakini baada ya Sitta kuondolewa pale juu na wao wakapoteza muelekeo kwashindwa kutafuta vyanzo vingine.

Leo hii na kumbuka wana watu vijana wako smart sana tu lakini wanadandia kila lenye ku trend hujui wanasimamia nini maana sio kila lazima uliongelee mambo mengine unaacha yanapita.

Leo hii ukimuuliza wewe kama mpinzani nini tofauti yako na huyu wa CCM? na uhakika hawajui wataanza kukutukana. Sipendi CCM lakini ukiangalia mbadala unaona bora ya hawa maana unawajua.
 
Hao wanaolalamika watuambie ni kwanini hawakuwaokoa wale 19 ambao wote walitwaliwa na Mungu.

Waseme walikuwa wapi?
Kweli kabisa ni swali muhimu kabisa hili..
Tatizo kuna utamaduni unajengeka kuwa kitu kikiwa supported na Chama fulani Wapinzani lazima wapinge bila kujali ni kweli au sio kweli, hivyo hivyo kitu kikiazishwa na upinzani upande wa pili utapinga bila kuangalia uhalisia wa jambo
 
CCM itaendelea tawala sababu Chadema ina watu wachache wenye uelewa Mbowe, Lissu, Mnyika

Wengine wengi ni wa hovyo sana
 
Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa baadhi ya Wanachama wa Chadema tena wengine Viongozi mfano ni Sugu, Heche, pambalu...
Hizo hoja sio za chadema ni maono ya mtu binafsi kama watu wengine. Ipo siku itakuwa kuna hoja wanaongea waislamu/wakristo kisa tu mtoa hoja ni member wa dhehebu hilo.

Jifunze kutofautisha maoni ya kichama na maoni ya mtu binafsi. Kuwa member au kiongozi wa kichama hakumwondolei mtu kuwa na maoni na mtazamo binafsi kama mwanadamu na mtanzania
 
Swala la Majaliwa limekuwa kubwa kuliko ajali.

Kwanini huu muda wa Kumjadili Majaliwa usingetumika kujadili hatma ya manusura na haki zao, fidia Kwa familia zilizoondokewa na wapendwa, ukosefu wa vifaa vya uokoaji vya kisasa Tena karibu na uwanja.

Kutwa kucha Majaliwa...

Aliyepewa kapewa, Mungu akitaka kukupa hakuandikii barua. Muda wa Majaliwa kutoka hatu Moja kwenda nyingine ulifika. Haijalishi njia iliyotumika kumtoa sehemu A kumpeleka sehemu B.

Tunalalamika viongozi Huwa wanatutoa kwenye mstari tuanza kujadili upumbavu.

Sasa kwenye hili Bado tutasingizia viongozi ndio wanaanzisha hizi nyuzi za Majaliwa!!?
 
CCM itaendelea tawala sababu Chadema ina watu wachache wenye uelewa Mbowe, Lissu, Mnyika

Wengine wengi ni wa hovyo sana

Ccm itaendelea kuwa madarakani kwasababu wananchi bado ni vilaza wakutupwa.

Wewe pamoja na mimi, na mamilioni ya waTz wengine.

Chadema au Ccm haiwezi kumletea maendeleo mwananchi asiyejitambua.

Tunawalaumu wanasiasa ila kwa uhalisia sisi wananchi ndiyo mazombi wakutupwa.
 
Ccm itaendelea kuwa madarakani kwasababu wananchi bado ni vilaza wakutubwa.

Wewe pamoja na mimi, na mamilioni ya waTz wengine.

Chadema au Ccm haiwezi kumletea maendeleo mwananchi asiyejitambua.

Tunawalaumu wanasiasa ila kwa uhalisia sisi wananchi ndiyo mazombi wakutupwa.
Elimu tunayopewa ni ya kuwa wajinga zaidi

Nchi yetu maji yamekuwa tatizo kisa tu mto umekauka
 
Nchi ina watu wa hovyo, kikubwa watu wameokolewa. Jambo la kushukuru. Habari za nani kafungua mlango naona kama hazina mashiko kwa sasa, tuna mengi kama taifa ya kujadili na kufanya
 
Back
Top Bottom