Nani alifanya "Due Diligence" ya Dowans? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani alifanya "Due Diligence" ya Dowans?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Nov 10, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  HATUA ya Rais Jakaya Kikwete kukiri kuwa kulikuwapo na udhaifu katika kufanya uchunguzi wa kutosha (due diligence) kuhusu kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond, aliyoitoa wakati wa kujibu maswali ya wananchi, imeanza kutafsiriwa na wabunge kama mwongozo wa ripoti ya Serikali itakayowasilishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda bungeni kuhusu utekelezaji wa maazimio 23 ya Bunge kuhusu kampuni hiyo.

  Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete alikiri kutofanyika kwa kile alichokitaja kuwa ni ‘due deligence’ udhaifu ambao uliibuliwa pia na Kamati Teule ya Bunge, iliyoongozwa na Mbunge wa Kyela, Dk. Harisson Mwakyembe. Hali hiyo inaunganisha mtazamo unaofanana kati ya Bunge na Rais Kikwete.

  Katika azimio namba saba kati ya hayo 23, kamati teule ya Bunge ilipendekeza kuwa: “Wajumbe wote wa kamati ya Serikali ya majadiliano (Government Negotiation Team-GNT) ambao ni maafisa waandamizi wa Serikali wawajibishwe kwa manufaa ya umma kwa kulitia hasara taifa kutokana na kushindwa kutumia elimu na ujuzi wao kulinda maslahi ya taifa.”

  Baada ya mapendekezo hayo, Agosti 28, mwaka 2008, Waziri Mkuu pia alitoa taarifa bungeni kuelezea hatua zilizochukuliwa katika utekelezaji wa maazimio hayo na hususan azimio hilo namba saba, ambalo linawahusu vigogo wa Serikali ambao ni pamoja na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

  Wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja. Kamati hiyo ilikuwa na jukumu la kutoa ushauri mzuri kwa Serikali kwa ujumla.

  Katika taarifa yake, Waziri Mkuu alieleza hatua zilizochukuliwa kuwa ni pamoja na kuwataka wahusika hao pamoja na kuandikiwa ili kutoa maelezo ya utetezi au ufananuzi katika kile kilichotajwa kuwa ni kuwapa haki ya asili ya kusikilizwa.

  Mbali na timu hiyo ya GNT ambayo katika sakata hilo ilipewa jukumu la kushauri serikali, pia ipo timu nyingine ya wataalamu iliyokuwa imepewa jukumu la kutathmini wazabuni wote katika orodha ya wazabuni waliokuwa wakiwania zabuni ya kuzalisha umeme kwa wakati huo.

  Waziri Mkuu alieleza kuwa miongoni mwa maeneo ambayo watumishi hawa wametakiwa kutoa maelezo ni jinsi walivyohusika katika mchakato mzima na kuingiza Serikali katika mkataba unaonekana kutokuwa na maslahi kwa Taifa ni pamoja na kutotumia utaalamu na uzoefu wao kikamilifu ili kutambua mapema kuwa Richmond Development Company LLC haikuwa na uwezo kitaalamu, kifedha na kuzoefu na hivyo kutokidhi matakwa ya zabuni.

  Maeneo mengine kwa mujibu wa Waziri Mkuu kwa wakati huo ambayo wahusika katika kamati hizo mbili walitakiwa kujieleza ni kutozingatia kikamilifu Sheria ya Manunuzi ya Umma, ya mwaka 2004 katika mchakato mzima wa kutoa zabuni, wajumbe kushindwa kuishauri Serikali kuhusu kuifanyia Kampuni ya Richmond Development LLC uchunguzi wa awali (Due Diligence) pamoja na ukaguzi baada ya tathmini ya zabuni (post qualification).

  Katika kipengele hicho cha ‘due deligence’ ndipo panapotajwa kuwamo katika ripoti itakayowasilishwa na Waziri Mkuu na kwamba kwa kuwa tayari Rais alikiri kuwa jambo hilo halikufanyika ipasavyo, matarajio ya wabunge wengi ni kuwa ripoti hiyo itakayowasilishwa kwenye mkutano huu wa 17 wa Bunge itabainisha hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika.

  “Tayari Rais Kikwete aliungana na maoni ya Kamati Teule ya Bunge hasa kuhusu kutofanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu Richmond , alikiri kuwapo kwa tatizo hilo hadharani alipozungumza na wananchi kwa hityo utaona wahusika wakuu kwenye suala hili wanamakosa ya wazi ambayo yametambuliwa tayari na Rais,”

  “Kwa hiyo tunatarajia kusikia tu hatua zinatazochukuliwa kwa kuzingatia kukiri huko kwa Rais. Na ukweli ni kwamba unapokuwa na timu za watumishi wanaoaminika ni watalaamu na kisha kazi haifanyiki vizuri na Rais anakiri ni wazi hatua kali zinapaswa kuchukuliwa kama ambayo kamati teule ya Bunge ilivyopendekeza,” alidokeza mbunge mmoja.

  Katika taarifa yake hiyo ya Agosti 28, mwaka jana, Waziri Mkuu pia aliweka bayana kuwa wahusika walipewa nafasi ya kujieleza na wakafanya hivyo na katika mkutano wa 16 wa Bunge, Waziri Ngeleja alitoa taarifa iliyokataliwa akisema wahusika walipewa barua za onyo.

  Lakini kutokana na mazungumzo ya Rais wakati akijibu maswali ya wananchi, alihidi kuwa taarifa ya sasa bungeni kuhusu Richmond itakuwa nzuri hali ambayo itafsiriwa kuwa wahusika ambao hawakufanya utafiti wa kutosha kuhusu Richmond watachukuliwa hatua za ziada.

  Pamoja na kusubiriwa kwa hamu kwa taarifa ya serikali kuhusiana na Richmond, ndani ya Bunge kumekuwapo na mgawanyiko wa dhahiri kuhusiana na sakata hilo ikielezwa kuwapo mkakati mahususi wa kusafisha wanasiasa na watendaji wa serikali waliochafuka kutoka na kashfa ya kampuni hiyo.

  Mgawanyiko huo umeelezwa kuwa chanzo cha msuguano uliopo sasa kati ya Bunge na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambako Mkurugenzi wake, Dk. Edward Hosea, ameonekana kuwa na jeuri ya kulumbana waziwazi na wabunge baada ya kutaka kuwahoji kuhusiana na suala la posho.

  Dk. Hosea pekee ndiye aliyebaki katika watendaji wa serikali waliotajwa katika kashfa ya Richmond na kwamba kupona kwake kulitokana nay eye kutokuwamo katika timu ya majadiliano ya serikali iliyoundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu kutokana na kashfa hiyo, Edward Lowassa. Hosea yeye alituhumiwa kupindisha taarifa ya wataalamu wake, tuhuma ambazo alisafishwa nazo Agosti mwaka huu na Bunge kuridhia.

  Makundi ndani ya Bunge yanaashiria hata kukiyumbisha Chama cha Mapinduzi (CCM) chenye wabunge wengi na kukilazimu chama hicho tawala kuunda Kamati ya Maalumu inayoongozwa na Rais Mstaafu, Ally Hassan Mwinyi akisaidiwa na wana CCM mashuhuri, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Abdulrahman Kinana.


  Source: Raia mwema  Makongoro Mahanga na Bi Sofia Simba tayari wameshaonyesha misimamo yao.Nilidhani huo ni msimamo wa serekali,
   
 2. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Huyu Rais hana lolote, Yeye mwenyewe na zao (Product) ya Richmond na EPA hivyo hawezi kabisa kufanya lolote wahusika kwani wao ndo walio mweka. Kitakacho fanyika ni kufunikiza kombe mwanaharamu apite.
   
 3. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Woote hao wanakula sahani moja,wasituzuge! Kikwete hawezi kuwafanya lolote wahalifu wenzie.
   
 4. s

  shabanimzungu Senior Member

  #4
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Crying wolf!
   
 5. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  mbuzi wa bwana HERI aliingia shambani kwa bwana HERI akala mazao ya bwana Heri na bwana HERI akaona yote HERI.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Nov 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kikwete amekuwa akirudia kuwa katika suala la Richmond aliagiza ufanyike uchunguzi wa kutosha juu ya uwezo na ukweli wa kampuni hiyo (due diligence). Na akakiri kuwa kama hilo lingefanyika labda matatizo ya Richmond yasingetokea. Hata hivyo, hadi hivi sasa sijamsikia akisema au mtu yeyote serikalini akitueleza kama hiyo "Due Diligence" ilifanyika kabla ya kuwapa Dowans mkataba wa Richmond.

  My assertion ni kuwa kama ilivyokuwa kwa Richmond ndivyo ilivyokuwa kwa Dowans! Hakuna aliyechukua muda kutafuta ukweli wa kampuni hii kiasi cha kuwaacha wajaze taarifa za uongo kwenye fomu za BRELA na kuwapa legal standing katika sheria zetu wakati wao utapeli wao ni mkubwa zaidi kuliko wa Richmond!
   
 7. M

  Mundu JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu,

  Nchi yetu hii ni bora liende. Nilikuwa na swali linalofanana na hilo leo asubuhi. Ni nani anayewafanyia Due Diligence mawaziri kabla hawajateuliwa. Hususan kwenye suala la maadili?
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji,

  Due Dilligence ya nini huku walikuwa wanaijua ni kampuni "YAO"?
   
 9. anthomata43

  anthomata43 Member

  #9
  Nov 10, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Namuomba Rais JK aangalie sana Richmound itamuweka pabaya uchaguzi wa 2010. Kwani wananchi wanamuona kam yuko upande wa mafisadi hivyo namuomba ashughulikie mapema iwezekanavyo.
   
 10. M

  Misana Member

  #10
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Richmond imeshamweka pabaya JK, yaani sijui ni mwananchi yupi hajui hili sakata la Richmond labda watetezi waliobaki ni wale ndugu zangu wa Monduli waliowapokea victims wa Richmind kama mashujaa
   
 11. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2009
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  DUE DILIGENCE!!!!!!!? ya nini? kwa faida ya nani? By the way nani afanye hiyo due diligence wakati wote si wasafi? kingunge na mahogiano kwenye kamati ya Mwinyi wametuthibitishia hayo.
   
 12. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Due diligence?

  Not in Tanzania kwa sababu mitanzania ndivyo tulivyo.
   
 13. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kuna maneno mengine ambayo Raisi hatakiwi kuyatumia kabisa katika mazingira ya uongozi tuliyonayo serikalini sasa hivi. Due Diligence inayopikwa au iliyoko machimboni? Hivi hayo maneno yamemtokea hapo kwenye hilo swala moja tu?
  hivi hajakumbuka kusema watumie hiyo hiyo kuchunguza Kagoda, deep green nk. ili hatua za kisheria zichuliwe? Anangoja nini mpaka leo?
   
 14. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  The virulent virus in this vivacious vicious circle of Vogon-ugly bureaucratic mediocrity continues to contaminate what's left of our collective consciousness to the point of risking extinction level event (people are mentioning the army boys openly, right here, did you see it yesterday?) the said virus, further spiraled by criminal complacency into the voluminous vortex of agnostic apathy, is powered by pathetic poverty of mind, party politics patronization , programmed puppeteering, psychological power palavers and petty pretty punditry.

  CCM, the pretense of a play is over, or rather the actors have forgotten even their lines and the audience will soon start to demand it's ticket money.

  I can't risk playing into 1-800-GET-INDICTED, but do not say I did not warn you.
   
 15. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Nadhani wote pamoja na Kikwete wamesahau kiapo walichoapa kulitumikia Taifa. Kama wangekuwa wanakumbuka isingelikuwa na haja hata ya kutamka kutumia "due diligence", ilitakiwa hatua kali tu kufuata baada ya kiongozi kushindwa kutenda kazi yake kama alivyoapa kulitumikia Taifa.
   
 16. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2009
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwanangu hii lugha unamwandikia Professor gani asome? Nimecheka kwa sababu hata muingereza hapa anatoka kapa! Hata hivyo you are very insightful! Tusonge mbele mkuu
   
Loading...