Nani alieleta talaka duniani;nani anastahili kupewa talaka?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani alieleta talaka duniani;nani anastahili kupewa talaka??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Apr 23, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  Ndugu zanguni kila nkifikiria maswahili haya nahisi kienglisenglish rupu
  embu mwenye kutusaidia maana siku hizi hzi talaka zinagawiwa mahakamani
  kama juice za sayona akuna tena ati miaka miwili na hii miwili nani aliileta
  na nani anastahili??
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Inategemea na misingi ya imani na dini ya wanandoa, kwetu wakatoliki hakuna talaka labda muamue wenyewe lakini kwamba mmekwenda kwa Padre ili aitenganishe ndoa kazi ipo. Lakini best kitu muhimu ni kuchunguzana kwa muda wa kutosha kabla ya kuoana ili kama kuna mashimo muweze kuyafunika na mkiamua kufunga ndoa basi idumu. Tatizo la vijana na hata wazee wanaoamua kuoana ndo hivyo yuko kwenye safari zake toka Ubungo to Manzese, kafika barabara ya Shekilango kapanda binti na kukaa siti moja, wamebadilishana namba za simu, hii ni jumatatu na ijumaa ndani ya wiki hiyo hiyo wanatangaza ndoa sasa mkubwa mtadumu kweli?

  Back kwenye swali, talaka imeanzishwa na mwanadamu mwenyewe, ile ya agano la kale Musa aliruhusu kwa sababu ya mashinikizo ya wenye mioyo migumu ndo maana our lord Jesus alisema anayemtaliki mkewe na kuoa mwingine azini na yule anayemuoa aliyetalikiwa azini.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280

  kweli best ila tatio si muda wapo waliokaa miaka mitano uchumba wakaachana miez 3 awa awakuchunguzana m mpaka nasema labda kabla ya kuaoan wapewe mida ya miezi mitatu kukaa pamoja wachunguzane lakini si kujuana ndan ya ndoa nina uhakika wakikaa kabla kwa muda wanazimudu kabisa samahan sijaidhinisha mzini ila mwaweza kaa ndani bila kufanya lolote mkichunguzana kila mtu kitanda chake kama chumba kimoja mmoja alale chini kwa muda litalipuka tu kama kuna tatizo lakini haya ya kuingia ndani miezi miwiliunajuta ndio huyyuu sio
   
 4. m

  masho Member

  #4
  Apr 24, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni tabia ya mtu tuu hakuna lolote, kwa sisi wakristo no talaka,
   
 5. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #5
  Apr 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  definition ya talaka inasema "ni hati rasmi ya kisheria inayotolewa pale ambapo ndoa imevunjika kiasi cha kutorekebishika"............ kwa msingi huo, talaka si mbaya na ni kitu kizuri kabisa na kitakatifu hata mbele za Mungu.......... msichanganye mambo, kitu kibaya hapo ni kuvunja ndoa........... izingatiwe kuwa talaka hutolewa kwa ndoa iliyokwishavunjika ili kulinda na kuhifadhi haki na wajibu wa wanandoa hasa juu ya watoto na mali zailizopatikana ndani ya ndoa. ndio maana nasema ni nzuri na takatifu kwani inahakikisha maslahi na usalama wa wasiohusika na ugoomvi wa wanadoa (mfano watoto).... pia inahakikisha usalama wa wanandoa wenyewe na mali zao.... mfano kuna ugomvi uanoweza kuishia suicide kama hautamalizika.... kwa kutengana kisheria kunaondoa uwezekanao wa mmoja kumbugudhi mwenzie na kama kuna mali iliyochumwa kwa pamoja, inagawanywa kwa misingi ya haki.............

  nimalizie kwa kusema talaka ni matokeo ya kuvunjika kwa ndoa... yaani kusitishwa kwa utashi wa watu wawili mume na mke kuishi pamoja , kupendana na kushirikiana... na technically, si talaka inayovunja ndoa, bali ndoa mnavunja wenyewe na talaka ni cheti (certificate) tu............ kuwa mahakama "imethibitisha" baada ya kushauriwa na baraza la ushauri la ndoa kuwa ndoa hiyo ime(kwisha)vunjika kiasi cha kutorekebishika kwa namna yoyote le...............

  kwa hiyo mahakama ikona bado uko mwanya wa kurekebisha, haipaswi kutoa hati ya talaka na badala yake inapaswa kuwapa muda wanadoa waendelee kujarib kurekebisha hayo yaliyopotoka ndani ya ndoa yao.............. labda hapa mahakama inaweza kulaumiwa kiasi fulani kwa kutoa talaka kirahisirahisi (kama mleta mada alivyosema wanagawa kama juici za sayona)......... kweli mahakama haiwezi kukwepa lawama kama wanagawa talaka kama juici za sayona...... wanapaswa kutoa talaka pale tu amabpo kwa hekima ya hakimu na wazee wa baraza hawaoni namana ile ndoa invyoweza kurekebishika

  the bottomline is, hakuna sheria yoyoyte inayozuia watalaka kuoana tena .......... endapo watasameheana na kujirudi kila mmoja kwa tabia iliyopelelkea kuvunjika ndoa, wanaweza kukufunga ndoa upya na ama wakasameheana na kuhuisha ndoa yao........... na wengi wamefanya hivyo baada ya ushauri nasaha..........
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,250
  Likes Received: 5,632
  Trophy Points: 280
  mbona sijakuelewa unasema talaka nzuri tatizo kuvunja ndoa
  so talaka inatolewa wanapojenga ndoa ama??
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mkuu nimemwelewa vzuri sana hope ukirudia tena utamwelewa ila kifupi ni kwamba mpaka mnakwenda mahakamani kudai talaka ni kwamba nyie wawili mnakuwa mlishavunja ndoa kabisa na mdomana mahakamani ampewi mpaka muwe mmepitia mabaraza ya usuluhishi ambayo ni serikali ya mtaa, then kama ni wakristo kanisani, kisha ustawi wa jamii ustawi wa jamii ndo top pale laima uwe na barua za kutoka kanisani kwamba mmesuluishwa imeshindikana na pale ustawi mmnasuluishwa kisha inapelekwa mahakamani so wanaovunja ndoa ni wanandoa wenyewe mahakamani mnakwenda kupewa cheti tu kama mlivyofunga ndoa mlipewa cheti hope imekuwa safi zaidi mkuu
   
 8. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #8
  Apr 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145

  mkuu upo wrong kidogo talaka ipo kote kote na maanisha na wakristo wa madhehebu yote
   
 9. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #9
  Apr 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  soma vizuri hilo andiko yesu mwenyewe aliruhusu kumwacha mkeo kama umemfumania na mke/mume
   
 10. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #10
  Apr 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mkuu nakubaliana na point yako kabisa kwani kwenye uchumba watu wanajificha sana makucha yanakuja kufunguliwa mkiwa kwenye ndoa hapo ndo kasheshe linaanza na ndo unaanza kupata sura alisi ya mke/mume yani nashindwa kabisa nisemeje kwani naunga mkono hoja yako ila naogopa kuambiwa tunafagilia uzinzi
   
 11. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #11
  Apr 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mkuu, nakuomba siku njingine unaquote au unagonga kitufe cha "kutambua" (au thanks) ili nijue kuwa mchango unaoongelea ni wangu........... kuanza kujibu moja kwa moja wakati mwingine inakuwa ngumu kujua unajibu hoja ya nani na hasa kama thread itakuwa imechangiwa na watu wengi..........

  back to the thread...........nakuomba usome tena na ntena na taratibu kabisa bila haraka nilichoandika na bila shaka utaelewa................... pia soama maelezo ya ziada aliyoroa dphone yameeleza vizuri sana nilichoandika.............. talaka na kuvunja ndoa ni vitu viwili tofauti kabisa............. talaka haivunji ndoa, na mkienda mahakamani kutafuta talaka kabla ndoa yenu haijavunjika, hamuipati kamwe ......... kuvunja ndoa kunafanywa na wanadoa wenyewe!!! na wakishaivunja ndo wanenda mahakamani kuomba "hati" ya talaka ili kuvunijka kwa ndoa yao kutambuliwe kisheria...........

  asante drphone kwa kunisaidia kufafanua........ ubarikiwe..............
   
Loading...