Wanabodi,
Naomba kwa wajuzi wa mambo ya majengo ya mabunge duniani wanisaidie haya majibu:
1. Ni "Genius" gani alibuni jengo letu la bunge Dodoma na alikuwa anawaza nini kwenye kichwa chake?
2. Nimeangalia mabunge mengi ( mfano Kenya, UK n.k) , sijawahi kuona muundo kama wa kwetu wa viti vile. Kwanza viko comfortable sana, pili vina madesk yaliyotengenezwa specifically soft ili hata mwanamke mwenye mikono laini sana aweze kuyapiga kama ngoma, na yakatoa sauti nzuri ya kupendeza ( au kuudhi ukitaka)
3. Unadhani aliyetengeneza hilo bunge , alikuwa na master plan ya kupata wabunge vilaza in future ili sisi kama nchi yenye rasilimali nyingi tusiweze kujadili mambo ya maana na kila anapojitokeza anayetaka kujadili hoja za maana zipigwe "ngoma" kwenye meza mpaka ashindwe kusikika?
4.Ni kwanini serikali ya wakati huo, ( maana ndiyo walikuwa waasisi wa kuuza rasilimali zote walizoweza kuzifikia) iliruhusu huyo "genious" kujenga jengo la namna hiyo, nje kabisa ya mabunge mengine yote ya Jumuia ya madola? Maana kwa ukaaji wa wabunge wa Kenya, au UK, huna hata nafasi ya kupiga meza ( maana hazipo). Hata nafasi ya kusinzia haipo, maana watu wamekaa kikazi zaidi na wanasikiliza hoja zote kabla ya kupiga mikofi kama wehu!
Jana niliangalia Waziri wetu wa fedha akitoa hotuba ya bajeti, kuna mahali hata kabla hajaeleweka anataka kusema nini, majitu yanapiga meza mfululizo..pwa, pwa! pwa!!!! Yaani inanishangaza sana
Kwa ujumla, nahisi kuna masterminds fulani walijua wanafanya nini kuhusu hili bunge letu. Maana hizo fancy chairs ziliambatana na kuja maneno kama mheshimiwa, na marupurupu kibaoooo!
Baada ya hapo wote tu mashahidi, bunge sasa limenunulika na limekwisha. Kuwa mbunge si lazima uwe mweledi, bali uwe karibu na "wenyewe" na uwe bingwa wa vijembe ndo utadumu vipindi vingi.
Kama mie sijaelewa wakuu, naomba michango yenu...