Nani alaumiwe: Viongozi wa kisiasa Vs viongozi wa dini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani alaumiwe: Viongozi wa kisiasa Vs viongozi wa dini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Jun 7, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima kwanza!

  Binafsi naamini kabisa, suala la amani si jukumu la chama cha siasa pekee bali ni jukumu la watanzania wote. Kwa miaka mingi toka kuanza kwa mfumo wa vyama vingi kumekuwa na mivutano hapa na pale, majungu ya hapa na pale na uzushi wa hapa na pale kuhusu baadhi ya vyama vya siasa kuhusishwa na dini fulani.

  Wakati mmoja kiongozi wa kisiasa aliwahi kutamka maneno ya kejeli: "Kama viongozi wa dini wanataka kuingia kwenye siasa basi wavue majoho" na kupotosha ule wajibu walionao (viongozi wa dini) wa kukemea maovu katika jamii. Lakini hebu tujiulize swali dogo la tunaweza kuhubiri amani na umoja wakati tunahubiri udini miongoni mwa vyama vya siasa? Uchaguzi mdogo wa Igunga tuliona dini fulani ilivyotumika kisiasa kwa chama cha kisiasa? Tumeona Arumeru jaribio la kutaka kuwatumia viongozi wa kidini katika uchaguzi na katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 vilevile tumeshuhudia hili.

  Tukirudi upande wa viongozi wa dini, leo hii viongozi wa kidini wanaweza kukanusha kwa hoja zenye mashiko kwamba suala la kuvunja muungano ni suala la Wanzanzibar au ni swala la Waisilamu dhidi ya Wakristo? Kama kwa dhati Wanzanzibar hawataki muungano nadhani lilikuwa jambo la busara kuungana na Wakristo katika harakati hizi kuondoa dhambi ya kibaguzi ya imani za kidini. Viongozi wa dini fulani nao wanalalamika shule zao kupata matokeo mabaya ni hujuma without clear justification, je tunataka kutengeneza Taifa gani? Leo Padre kasema hivi kesho yule kajibu mapigo yale. Tukikubali kuishi kwa hisia za kibaguzi wa kidini ipo siku uvumilivu utatushinda?

  Binafsi nashindwa nani wa kumlaumu Mwanasiasa au Kiongozi wa Dini?
  :confused2:Sijui wewe?
   
 2. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hii ni jamii kaka na sisi ni binadamu tunamapungufu ndiyo maana tunakunya! Katika kila mkusanyiko wa watu wenye malengo fulani wapo ambao wanakuwa na dhamira ya kweli katika malengo husika na wapo wanaokuwa kama si njaa yao kuwaweka katika mkusanyiko huo basi ni waaribifu (wanafiki, watu wenye hiana) wapinga maendeleo katika jamii husika.
  Kwa maana hiyo katika siasa utawakuta watu wenye dhamira safi na mbaya lakini pia hata katika dini wapo wa aina hiyo hiyo!
  La muhimu hapa si kutaka kujua wanasiasa na viongozi wa dini ni wapi wanatuyumbisa!! ila ni kujua ni nini matatizo yetu na ni nani atakayeweza kutuongoza ili tuyaondoe matatizo husika! huku tukijiadhari na wenye dhamira mbaya.
   
 3. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  "La muhimu hapa si kutaka kujua wanasiasa na viongozi wa dini ni wapi wanatuyumbisa!! ila ni kujua ni nini matatizo yetu na ni nani atakayeweza kutuongoza ili tuyaondoe matatizo husika! huku tukijiadhari na wenye dhamira mbaya."


  I salute you Mkuu! Binafsi naamini makundi haya mawili ni makundi makubwa yenye nguvu katika jamii, lakini makundi haya mara nyingi ndio chanzo cha matatizo makubwa katika kuvunja amani na umoja katika jamii nyingi. Tatizo ni "udini" labda twende mbele zaidi na kujua ni nani anaweza kuonya makundi haya mawili? kwa sababu wanasiasa wanapotosha? Viongozi wa dini wanapotosha na wote nawalaumu, je ni nani mkombozi wetu katika jamii hii ya fikra kinzani?
   
 4. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kiongozi! Udini sasa unatuvuruga! Lakini hii ni silka ya mwanadamu! anapokuwa na mtazamo tofauti au imani tofauti na mwingine basi hujengeka dhana kuwa wote kati yao hawawezi kutendeana haki sawia kwasababu tu ya hizo tofauti zao za kiimani na mitazamo!
  Sasa inapotokea hali kama hii tunamwitaji kiongozi shupavu atakaye hakikisha kuwa kutoaminina huko katika mazingira kama hayo hakupewi nafasi pale yanapokuja masuala ya msingi katika jamii yetu!
  Chukulia mfano Mwl. Nyerere! aliudhibiti ukabila na udini kwa hekima kubwa!alitufanya wamoja! leo hii japo huyu aliopo anatugawa kwa udini na ukanda lakini bado inakuwa ngumu kidogo sababu baba wa taifa! alitufanya wamoja toka huko nyuma.
  Chukulia mfano mwingine Mzee Mandera alipoapishwa kuwa raisi wa kwanza mweusi huko SA watu walifikiri atawatimua makaburu lakini kinyume chake alitengeneza muafaka nao leo hii huuwezi kuamini ule ubaguzi wa rangi uliokuwa umepungua kwa kiasi kikubwa.
   
 5. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kiongozi anaye tuongoza leo ndiyo chanzo cha hali hii! Kumbuka huko nyuma maaskofu walikuwa wakikosoa pale wanapoona mambo yanakwenda ndivyo sivyo! lakini leo hii maskofu wakikosoa anachofanya bwana mkubwa anawapikia ubwabwa mashekh na anawaambia wajibu!
  Ni kweli ulio wazi kuwa huko nyuma sisi waislamu atukupewa msukumo katika suala la elimu!lakini jambo hili halikutakiwa kutumiwa sasa kuonyesha kwamba eti wakristo wa tanzania wanatunyonya sisi waislamu.
  La muhimu hapa kama Kiongozi anayetuongoza sasa angekuwa na dhamira ya kweli ya kutufikisha katika malengo yetu tuliokusudia angejaribu kuiweka sawa hali hiyo na siyo kuwachochea mashekh wa shura ya maimamu kutembea nchi nzima kusema nchi hii inaongozwa kwa mfumo kristo!
  Kiongozi huyo ana dhamira mbaya! yeye anataka kutawala nakujinufaisha tu! hana imani hata chembe!! yeye kutawala na kuiba tu! hivyo haoni kama ni hatari kuiacha hali iliyopo kuendelea!
  Ninahisi anayo ndoto kuwa akiendelea kutugombanisha wakristo na waislamu uenda tukaingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ili yeye andelee kutawala na kutuibia wala afikiri kuwa dhambi hiyo itaanza kumsambaratisha yeye! Ni mroho! na mrafi! hana dini! ni mshirikina!
   
 6. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mbelwa umeenda wapi chochea uzi wako watu wachangie na uzi mzuri sana huu!
   
 7. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu! Nimejaribu kuwa mvumilivu kusubiri mawazo ya Watanzania wengine nione wana mtazamo gani kuhusu hili, kama nilivyosema awali makundi haya mawili ndio yanawakilisha jamii pana na kwa mtazamo huu makundi haya yana influence kubwa kuishape jamii.
   
 8. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni viongozi wa dini walio waoga na wanafiki, ambao wako tayari kutumika na wanasiasa mafisadi na wasio na uzalendo ambao wanawaza kutawala kwa damu au amani.
  Inaniudhi na kunisikitisha sana pale viongozi wa dini wanapokubali kutumiwa na wanasiasa kama ngao ya kuwakinga dhidi za hoja za viongozi wa dini nyingine hasa hoja za Maaskofu. Nachukia viongozi wa dini wanaopinga hoja muhimu za kitaifa mradi tu zimeletwa wa dini nyingine. Wanatumiwa na watawala kutuvuruga na wanawatupa kama toilet paper.
   
Loading...