Nani alaumiwe kwenye tatizo la wafanyakazi hewa?

J33

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
1,552
1,512
Najua JamiiForums kuna wataalamu wa kila aina naomba mnipe ufafanuzi kwa hili!

Kuna watu waliacha kazi miaka 3 iliyopita wengine kwa kuandika barua au kimya kimya then wakurugenzi wakakata mishahara kama standing order inavyowaelekeza.Wakurugenzi kumbe walizuia mishahara isiingie kwenye account za walengwa ila wakapitishia wanapojua wao kwa muda wote huu.

Leo imekuja ishu ya wafanyakazi hewa unakuta na wewe upo wakati hukuwa unapata huo mshahara na wengine account zilifungwa kabisa. Nani anatakiwa alaumiwe hapa na ipi haki ya mtu anayechafuliwa jina kuwa alikuwa mfanyakazi hewa ??

Duc In Altum.
 
walaumiwe hao wakurugenzi waliokosa uzalendo na kuanza kuliibia taifa hili. sioni kama kuna cha kujiuliza hapo. ndo maana serikali inawachulia hatua hao jamaa,
 
Hilo la Wakurugenzi kwa jinsi ulivyoliweka sidhani kama inawezekana! Kwa zamani wakati wanalipana dirishani ndivyo walikuwa wanafanya lakini siku hizi mshahara unapita bank moja kwa moja!
 
hawa wakurugenzi wanakaaje na watumishi hewa! watu wanalipwa mamilioni wakati hawafanyi kazi! mimi nafikiri hawa waagiri waangaliwe! kwann mishahara inaingia halafu hairudi! hizo hela zinaenda wapi! wao wana majibu!
 
Hilo la mishahara lipo pia kwenye pension. Unakuta Babu kajifia zake kitambo lakini pension inaendelea kuja na kv inaingia kwenye a/c moja kwa moja, inaliwa na ndugu wa Babu!!

Unajua hii issue ya mishahara kwa walioacha kazi au kufa; kwa kiasi kikubwa ni uzembe tu wa Halmashauri wa kuto-update payroll mara kwa mara!! Sometimes zinaliwa na hao hao wafanyakazi walioacha kazi
 
Juzi nimepata taarifa kuwa kuna waliokuwa wafanyakazi huko Rukwa wakaacha kumbe wakurugenz walikuwa wanaendelea kupiga pesa kwa majina yao sasa wamatafutwa na polis kwa amri ya Mkurugenzi na baadhi wamekamatwa. Nashangaa kwann mwiz anawatafuta watu wasiohusika na account inasemekana zilishafungwa zaman!

Duc In Altum.
 
Back
Top Bottom