Nani Alaumiwe kwa Hasara Watanzania Waliyoingia Leo?

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
23,489
70,277
Mods msiunge uzi🛇

Kama tunavyojua ni muda wa wiki kadhaa sasa kumekuwa na vuguvugu la pambano la mpira wa miguu kati ya watani wa jadi Simba na Yanga almaarufu kama Kariakoo Derby.

Pambano hili lililosubiriwa kwa hamu kubwa hatimae lilikuwa lifanyike leo tarehe 8 Mei saa 11:00 jioni. Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida muda wa mchana wa leo ikaenea taarifa kutoka TFF kuwa muda wa kuanza pambano umesogezwa mbele mpaka 1:00 usiku na kuwa hiyo imetokana na maagizo ya wizara.

Chakusikitisha zaidi barua hiyo kwa umma wa wadau wa michezo (vilabu, media, mashabiki) haikuianisha sababu za kusogezwa mbele kwa pambano hilo. Zaidi ya kusema tu ni maagizo ya wizara.

Sasa napenda kwanza kuwauliza TFF (Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania) na TPLB (bodi ya ligi) je walipopokea agizo hilo walizingatia sheria inayohusiana na jambo hilo. Je kama walizingatia waliwaeleza waliowapa agizo hilo kuhusu sheria hiyo? Je kama waliwaeleza ni majibu gani walipewa mpaka kuamua kuvunja sheria hiyo?

Tunatambua kuwa muda wa kuahirisha au kusogeza mbele muda wa pambano inaweza kufanyia chini ya masaa 24 (nikimaanisha kama ilivyofanywa leo) lakini kwa sababu maaalum. Cha ajabu ni kuwa mpaka sasa sio TFF wala Bodi ya Ligi waliotoa sababu hiyo/hizo maalumu za kusogeza mbele muda wa kuanza kwa mechi hiyo zaidi ya kusema kuwa ni agizo la wizara.

Je viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza vyombo vyetu vihi hawana weledi juu ya sheria zinazosimamia soka letu?

Je gharama zilizotumiwa na vilabu katika kujiandaa na pambano hili zitafidiwa? Je gharama zilizotumiwa na mashabiki kusafiri kutoka mikoani au hata tarafa mbali mbali za jiji la Dar es Salaam zitafiwa na nani?

Je utaratibu utakuwa vipi kwa wale waliokuwa wamenunua tiketi kwaajili ya kutizama pambano hilo mubashara?

Je vombo vya habari vilivyotumia budget kuandaa vyombo vyao na watu wao kwaajili ya kurusha matangazo live katika channel za redio na runinga zitafidiwa na nani?

Je ni lini TFF na TPLB wataueleza umma wa Watanzania sababu za msingi za kusogezwa mbele kwa muda wa kuanza pambalo nilo na je watakapoeleza watawezaje ku justify kitendo hicho cha kutoa sababu baada ya usumbufu wote huu na sio kabla?

Haya ni maswali ambayo viongozi husika inabidi kuyajibu. Pia viongozi na mamlaka husika inabidi kuwajibika au ikibidi kuwajibishwa ili kuwa funzo siku nyingine.
 
Samia hamna kitu, hamna kitu..tumepigwa tuuu na Katiba.

Na hili liwazir, Pua kubwa,kichwa kikubwa na akili kisoda.

TFF nao wapuuzi tu , jambo kma hili linapotokea ,unashirikisha mawazo ya wadau kwanza .
Mimi nawalaumu zaidi bodi ya ligi na TFF kwa kukubali kufanyiwa maamuzi na wanasiasa wakati kuna sheria zinaongoza masuala ya kimpira.
 
Mods msiunge uzi🛇

Kama tunavyojua ni muda wa wiki kadhaa sasa kumekuwa na vuguvugu la pambano la mpira wa miguu kati ya watani wa jadi Simba na Yanga almaarufu kama Kariakoo Derby.

Pambano hili lililosubiriwa kwa hamu kubwa hatimae lilikuwa lifanyike leo tarehe 8 Mei saa 11:00 jioni. Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida muda wa mchana wa leo ikaenea taarifa kutoka TFF kuwa muda wa kuanza pambano umesogezwa mbele mpaka 1:00 usiku na kuwa hiyo imetokana na maagizo ya wizara.

Chakusikitisha zaidi barua hiyo kwa umma wa wadau wa michezo (vilabu, media, mashabiki) haikuianisha sababu za kusogezwa mbele kwa pambano hilo. Zaidi ya kusema tu ni maagizo ya wizara.

Sasa napenda kwanza kuwauliza TFF (Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania) na TPLB (bodi ya ligi) je walipopokea agizo hilo walizingatia sheria inayohusiana na jambo hilo. Je kama walizingatia waliwaeleza waliowapa agizo hilo kuhusu sheria hiyo? Je kama waliwaeleza ni majibu gani walipewa mpaka kuamua kuvunja sheria hiyo?

Tunatambua kuwa muda wa kuahirisha au kusogeza mbele muda wa pambano inaweza kufanyia chini ya masaa 24 (nikimaanisha kama ilivyofanywa leo) lakini kwa sababu maaalum. Cha ajabu ni kuwa mpaka sasa sio TFF wala Bodi ya Ligi waliotoa sababu hiyo/hizo maalumu za kusogeza mbele muda wa kuanza kwa mechi hiyo zaidi ya kusema kuwa ni agizo la wizara.

Je viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza vyombo vyetu vihi hawana weledi juu ya sheria zinazosimamia soka letu?

Je gharama zilizotumiwa na vilabu katika kujiandaa na pambano hili zitafidiwa? Je gharama zilizotumiwa na mashabiki kusafiri kutoka mikoani au hata tarafa mbali mbali za jiji la Dar es Salaam zitafiwa na nani?

Je utaratibu utakuwa vipi kwa wale waliokuwa wamenunua tiketi kwaajili ya kutizama pambano hilo mubashara?

Je vombo vya habari vilivyotumia budget kuandaa vyombo vyao na watu wao kwaajili ya kurusha matangazo live katika channel za redio na runinga zitafidiwa na nani?

Je ni lini TFF na TPLB wataueleza umma wa Watanzania sababu za msingi za kusogezwa mbele kwa muda wa kuanza pambalo nilo na je watakapoeleza watawezaje ku justify kitendo hicho cha kutoa sababu baada ya usumbufu wote huu na sio kabla?

Haya ni maswali ambayo viongozi husika inabidi kuyajibu. Pia viongozi na mamlaka husika inabidi kuwajibika au ikibidi kuwajibishwa ili kuwa funzo siku nyingine.
Hapa sijui pa kulala jiji hili, nimetoka Kigoma kwa Treni leo hii mechi imeahirishwa ? Sijui kiingilio changu ningetoa kama sadaka basi ningepata swawabu ,😠😠😠😠😠😠😠😠😠😠😠
 
Duh pole sana mkuu.
 
Back
Top Bottom