Nani alaumiwe endapo CCM itashinda jimbo la Kinondoni na Siha?

Naona Pohamba amepata waunga mkono wengi kwenye hz post za kinondoni. Wanalalamika kwa cdm haikugombea na why sasa wagombee. Like za kutosha. Ukweli kwamba km unafikiri kwa Uhuru na kwa kutumia akili ya kawaida na si form iv, utaelewa ukweli kwamba Chadema wapo vizuri sana kwa maamuzi yao.
 
Katika kosa ambalo CHADEMA wamelifanya litakuja kuwagharimu ni kusimamisha mgombea katika jimbo la Kinondoni na Siha.

Ikumbukwe ya kwamba siku chache zilizopita tulisusia uchaguzi kwa sababu ya kutokuwa na imani na tume lakini pia tukaorodhesha na kasoro kuhusu tume na chaguzi zilizotufanya tujiondoe katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Longido, Songea na Singida.

Leo hii tunashiriki uchaguzi na tume ile ile ambayo tulidai kwa ushahidi haikutenda haki leo tunashiriki uchaguzi na uchaguzi huu na tume ile ile ambayo mbowe alilalamikia na kasoro zote alizozitoa lakini sijui kama tume imezifanyia kazi na uchaguzi huu CCM wana asilimia zote za kushinda

Na endapo CCM itashinda hii itakuwa ni dharau kwa wapinzani na hapo ndipo mtawapa la kuongea akina Mtuliaa.

Je ikitokea tumeanguka ni nani alaumiwe kwanza katika hili maana tulisusa na sasa tunashiriki na tume ile ile ambayo tuliigomea sasa ikishinda CCM tutasemaje?

Ulaumiwe wewe unaependa lawama
 
Mpaka hoja zao zitakapojibiwa

Wana Chadema wa Longido, Singida na Songea Sijui wanajionaje Sasa hivi walivyoachwa solemba na kikundi cha kina Mbowe
Songea wapo poa tu, sema jingine. Uchaguzi wa Songea si sawa na hz mbili za kizembe zinazotutia Hasara zisizo na lazima. Na safari hii watu wa dar mtapimwa uwezo wenu kwa maamuzi ya kinondoni.
 
Songea wapo poa tu, sema jingine. Uchaguzi wa Songea si sawa na hz mbili za kizembe zinazotutia Hasara zisizo na lazima. Na safari hii watu wa dar mtapimwa uwezo wenu kwa maamuzi ya kinondoni.

Pole, Jogoo asipowika au akiwika patakucha tu
Mkishiriki au msiposhiriki CCM itashinda tu
 
Back
Top Bottom