Nani alaumiwe endapo CCM itashinda jimbo la Kinondoni na Siha?

toto zuli

JF-Expert Member
Aug 20, 2012
265
278
Katika kosa ambalo CHADEMA wamelifanya litakuja kuwagharimu ni kusimamisha mgombea katika jimbo la Kinondoni na Siha.

Ikumbukwe ya kwamba siku chache zilizopita tulisusia uchaguzi kwa sababu ya kutokuwa na imani na tume lakini pia tukaorodhesha na kasoro kuhusu tume na chaguzi zilizotufanya tujiondoe katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Longido, Songea na Singida.

Leo hii tunashiriki uchaguzi na tume ile ile ambayo tulidai kwa ushahidi haikutenda haki leo tunashiriki uchaguzi na uchaguzi huu na tume ile ile ambayo mbowe alilalamikia na kasoro zote alizozitoa lakini sijui kama tume imezifanyia kazi na uchaguzi huu CCM wana asilimia zote za kushinda

Na endapo CCM itashinda hii itakuwa ni dharau kwa wapinzani na hapo ndipo mtawapa la kuongea akina Mtuliaa.

Je ikitokea tumeanguka ni nani alaumiwe kwanza katika hili maana tulisusa na sasa tunashiriki na tume ile ile ambayo tuliigomea sasa ikishinda CCM tutasemaje?
 
Kama ni kushindwa basi sababu haitakuwa tume... tujifunze kuwa wakweli!

CUF wana nguvu sana Kinondoni... hawa wanaweza kuzigawa kura!!!

Kususia Songea ilikuwa brilliant political move... unasusia kwa sababu "hauna imani na tume" lakini ukweli ni kwamba Songea, na Ruvuma kwa ujumla wamekunywa maji ya bendera ya CCM!!

Ikiwa CHADEMA walishindwa kuchukua jimbo 2015 wakati kulikuwa na amsha amsha ya kufa mtu; there's no way wangeweza kuchukua jimbo la Songea sasa wakati CHADEMA yenyewe wala haileweki eleweki!

So, kuliko kuingia gharama za uchaguzi na kupata aibu ya kushindwa, suluhisho ilikuwa ni kususia uchaguzi in a genius way... "hatuna imani na tume"!!!
 
Unasema CCM ikishinda nani alaumiwe?,

Ni Sawa na kusema Jua likichimoza asubuhi Nani alaumiwe!

Ushindi wa Kinondoni na Siha ni Kama Jua kuchomoza baada ya kupambazuka

Breaking news ni CCM kushindwa sio kushinda

Na Inshallah tutashinda kama tulivyoshinda Ruvuma, Singida na Arusha!
 
Kamanda :
1. Mwenyekiti alijiamulia kususua uchaguzi bila kutushirikisha wanachama; sijui alidhani chama ni sacos yake binafsi au alidhani uenyekiti ni ufalme ambapo unaweza kuamua tu
bila kuwashirikisha watu?! Uamuzi wa kususa uchaguzi haukuwa wa chama.

2. Kushiriki uchaguzi ndo kukuza demokrasia yetu.

3. Siasa za visasi za yule 'mshitaki wa taifa letu' hazisaidii kujenga chama, zinasaidia kukifanya chama kionekane ni kama genge la wahuni wasiostahili kupewa dhamana ya kuongoza nchi. Inabidi kufanya siasa za kistaarabu ili kujenga taswira nzuri ya chama.

4. Wa kulaumiwa ni mbowe kwa kushindwa kukiimarisha chama toka Dr Slaa ameondoka.
 
Katika kosa ambalo chadema wamelifanya litakuja kuwagharimu ni kusimamisha mgombea katika jimbo la kinondoni na siha.

Ikumbukwe ya kwamba siku chache zilizopita tulisusia uchaguzi kwa sababu ya kutokuwa na imani na tume lakini pia tukaorodhesha na kasoro kuhusu tume na chaguzi zilizotufanya tujiondoe katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa longido,songea na singida.

Leo hii tunashiriki uchaguzi na tume ile ile ambayo tulidai kwa ushahidi haikutenda haki leo tunashiriki uchaguzi na uchaguzi huu na tume ile ile ambayo mbowe alilalamikia na kasoro zote alizozitoa lakini sijui kama tume imezifanyia kazi na uchaguzi huu ccm wana asilimia zote za kushinda

Na endapo ccm itashinda hii itakuwa ni dharau kwa wapinzani na hapo ndipo mtawapa la kuongea akina mtuliaa.

Je ikitokea tumeanguka ni nani alaumiwe kwanza katika hili maana tulisusa na sasa tunashiriki na tume ile ile ambayo tuliigomea sasa ikishinda ccm tutasemaje
Kwahiyo wewe ulitaka wasusie hadi lini?
 
Kama ni kushindwa basi sababu haitakuwa tume... tujifunze kuwa wakweli!

CUF wana nguvu sana Kinondoni... hawa wanaweza kuzigawa kura!!!

Kususia Songea ilikuwa brilliant political move... unasusia kwa sababu "hauna imani na tume" lakini ukweli ni kwamba Songea wamekunywa maji ya bendera ya CCM!!

Ikiwa CHADEMA walishindwa kuchukua jimbo 2015 wakati kulikuwa na amsha amsha ya kufa mtu; there's no way wangeweza kuchukua jimbo la Songea sasa wakati CHADEMA yenyewe wala haileweki eleweki!

So, kuliko kuingia gharama za uchaguzi na kupata aibu ya kushindwa, suluhisho ilikuwa ni kususia uchaguzi in a genius way!!!
Kaka uko vizuli sana
 
Hapo lawama zitaenda kwa mapolisi.
Tegemeeni kamata kamata ya kufa mtu.
Tegemeeni watu kuwekwa ndani na watatoka baada uchaguzi
 
Zikiwa hazijibiwi ?

Unarudi kushiriki Uchaguzi bila ya kueleza sababu za kubadili uamuzi
Press release ya Jana imetaja tu majina ya Wagombea haikueleza sababu za kurudi japo za kususia zilielezwa

Mtatiro alimtukana Lipumba wiki iliyopita kwa kusema atashiriki Uchaguzi wa Kinondoni , Mara paaa na Mabosi wake wa Chadema nao wametia Timu kajikuta Hana pia kushika
 
Tamaa ni mbaya sana! Dola chama watajichukulia jimbo na cdm wataenda mahakamani ambako wanajua kuwa kuna muhimili uliojichimbia zaidi na kesi itachukuwa miaka 3 tunapoelekea uchaguzi mwingine 2020!
 
Back
Top Bottom