Nani ajiuzuru kwa uzembe?

ZeMarcopolo

Platinum Member
May 11, 2008
14,013
7,209
"Chanzo cha kuungua na kuharibika waya wa umeme wa chini ya bahari unaopeleka umeme Zanzibar kimebainishwa kuwa ni ukosefu wa betri za kuendesha jenereta za kupoza waya huo ambao unalazimika kupozwa muda wote bila kujali unazalisha umeme ama umezimwa.

Habari za ndani zilizoelezea tatizo hilo zilisema uzembe wa baadhi ya viongozi wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) ndiyo chanzo cha kukosekana umeme visiwani hapa kwa karibu wiki tatu sasa kwa vile ulishindwa kutoa Sh. 150,000 za kununua betrii." - NIPASHE.
 
watu wanakodolea macho mamilioni ya epa na ufisadi mpaka wanasahau kubadilishA BETRI ZA GENERETA
 
huo ni uzembe usio na mfano

sasa hivi wanalipa mamilioni ya fedha kwenye kutatua tatizo

s *** nzi
 
Jibu zuri.
Peke yake?

Kwanaza umeuliza "nani ajiuzulu",kama ulitaka zaidi ya hao si ungeuliza 'nani wajiuzulu?

Well,waziri wa nishati Zanzibar,mkurugenzi wa TANESCO zanzibar,Na area manager wa TaNESCO pamoja na karume
 
Kwanaza umeuliza "nani ajiuzulu",kama ulitaka zaidi ya hao si ungeuliza 'nani wajiuzulu?

Well,waziri wa nishati Zanzibar,mkurugenzi wa TANESCO zanzibar,Na area manager wa TaNESCO pamoja na karume

Wengine wote sawa Isipokuwa Karume, hili wala siyo Zanzibar peke yake ndivyo mashirika ya umeme yanavyofanya kazi Tanzania. Wenyewe wakiona umeme unawaka basi ni raha mstarehe hakuna mantanance wala nini. Kwani bongo mara ngapi mitambo/over voltage nk vimetokea ukifuatilia ni uzembe wa shirika?

Hapa ni Mkurugenzi wa Tanesco Zanzibar wa kwanza na Area Manager, Waziri pia kwa kushindwa kuwawajibisha baada ya kugundua hilo swala.

Rais labda tu kwa kutomtimua waziri wake, lakini hapa tutakuwa mbali sana. Labda kama tumepata kisingizio cha kusolve suala la Muafaka
 
naam hapa a;au tunazungumza mambo kiutuzima sio kulishana kasa kama anavotaka kutufanyua Mwiba wa shokishoki usiochoma.

haya masuali ya uzembe tanzania yameota nabu kila idara. Wakati umefika kutokuoneana haya. anaehusika kwa uzembe hata awe shemeji awajibishwe. ili liwe funzo kwa wengine

na kila mtu atimize wajibu wake
 
Mkuu,ndivyo nilivyomaanisha maanake mpaka sasa hakuna aliyewajibika.Waziri wake hajawawajibisha walioko chiniyake,sasa rais alitakiwa amtimue au angalao atoe maelezo ya kuridhisha.Sasa rais nae Kashindwa,basi sisi waajiri wake tumuwajibishe .Anastahili adhabu kabisa
 
naam hapa a;au tunazungumza mambo kiutuzima sio kulishana kasa kama anavotaka kutufanyua Mwiba wa shokishoki usiochoma.

haya masuali ya uzembe tanzania yameota nabu kila idara. Wakati umefika kutokuoneana haya. anaehusika kwa uzembe hata awe shemeji awajibishwe. ili liwe funzo kwa wengine

na kila mtu atimize wajibu wake

Kweli kabisa,huwezi kutesa wananchi kwa uzembe halafu uachwe tu hivi hivi
 
Kwanaza umeuliza "nani ajiuzulu",kama ulitaka zaidi ya hao si ungeuliza 'nani wajiuzulu?

Well,waziri wa nishati Zanzibar,mkurugenzi wa TANESCO zanzibar,Na area manager wa TaNESCO pamoja na karume

onesha kosa la kila mmoja, lililopelekea kukosekana kwa sh.150,000?= kwa wakati. Aidha kama kunakosa lingine/mengine yaliyopelekea kuharibika kwa mtambo huo, vinginevyo hao wanaonewa.

Labda tuwaulize (Mhe. Karume, Mhe. Wazuri wa nishati-SMZ na Mkurugenzi wa TENESCO Znz.) wamechukua hatua gani baada ya uzembe kujitokeza kwa wahasibu kushindwa kutoa malipo ya sh. 150,000/= katika wakati uliotakiwa.
 
Sasa ukisikika unasema hakuna umeme Zanzibar unakamatwa eti unaibuguzi serikali ya Wahafidhina, na polisi wapo mstari wa mbele kuwakamata watakaosikika wakitoa kauli hiyo ya hakuna umeme wala maji hazarani. ama kweli mwisho wa dunia unakaribia yaani nchi nyengine Mwenyezi Mungu anawapatia viongozi wazuri sisi huku ametuwekea mashaka matupu ,maana kusema kusema Unguja hakuna umeme wala maji imekuwa kosa la jinai mbona Pemba miaka nenda miaka rudi hakuna umeme wala maji na vingine tele hajakamatwa mtu wala kufunguliwa mashitaka ?
Sijui polisi huko nayo imishakumbwa na tatizo la kukosa umeme na maji mi nilizani matatizo haya ni walioko uraiani tu ,kumbe hata kambini kumekauka,na magwanda yale ya kaki halafu maji hakuna ,hawa bila ya shaka wamianzisha kamata kamata ili wapate watu wa kuchimba visima na kuwachotea maji ,hawana jingine.
 
Hapa bila Ubishi ni Amani Abeid Karume ajiuzulu ndiye anaye fuga ugonjwa.,
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom