Nang'oa mzizi wa fitna kuhusu views, jifunze mwenyewe kupata views halali na feki pamoja na madhara

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
2,733
2,000
Kumekuwa na uzushi ambao ukiachwa kwa muda mrefu basi ndio utaonekana ukweli.

kwa namna moja au nyingine mti wenye matunda hupigwa mawe mengi na ndio hiki kinachowatokea wasanii wanaopta youtube views kwa njia halali wakisingiziwa wananunua, kitu ambacho hakina ukweli hata wa chembe ya tone la chozi.

Pia kuna wasanii wanaotaka ummarufu wa haraka kwa kupata views nyingi wameishia pabaya kwa kuingizwa chaka na wataalam uchwa wa IT wanaojinadi wanaweza kuongeza views, na ni kweli wanaziongeza views ila ni views "FEKI" na matokeo yake hizi views feki huwa zinatambulika na youtube kwa kiasi fulani na zikitambulika basi hata video yako uliyojisifia imeingiza views milioni 1 ndani ya masaa machache usishangae baada ya saa zikasomeka laki 8 na ukaanza kulalamika zimerogwa kumbe au umeibiwa.

TUANZE NA VIEWS FEKI WA KUNUNUA

Hizi views zinatengenezwa na maroboti na zinanunulika mitandao kibao ila madhara yake ni kwamba nyingi zinachujwa, mifano ya mitandao ni kama

1. tube.biz

1586607885287.png
2. instant-fans.com

1586607940598.png


3. https://viewsta.com
1586607991427.png


4. fanssuply.com
1586608022597.png


kama mnavyoona, ni pesa yako tu hata views milioni unanunua, ila inabidi uwe mjanja, video yako ikipata views hata laki 6 unamwagia laki 4 ila baada ya hapo nyingi zinachujwa.

VIEWS HALALI (KUNUNUA / PROMOTION)

hawa hawanunuliki, ni kama unaweza kuweka bango lako la biashara watu wakiona na usipate mteja, inabidi bidhaa kwanza ivutiwe

Unaweza kutangaza video yako kupitia facebook na instagram, Video inaweza kuwa sekunde 30 tu, itafikia idadi fulani ya watu mfano elfu 60 wataliona tangazo ila unalipia kiasi Fulani (cost per click) kwa ambao watabofya tangazo kwa hiari yao wakaicheki video nzima youtube, kama hakuna ataecheki basi video hio hakuna anataka kuicheki na hukatwi kitu hapo utakuwa umetwanga maji kwenye kinu.

1. utachagua lengo la tangazo lako, kwakuwa unataka ku promote video yako utachagua video views.
1586608641033.png


2.utachagua bajet yako mfano dola 50 kwa siku (120,000/ pesa ya madafu)
1586608750983.png


3. kwa hii bajet tangazo lako linaweza kufikia takribani watu elf 38 hadi laki kwa siku ili kuwahamasisha watu watazame video yako nzima youtube, hawa watu endapo hakuna hata moja atashawishika kuangalia video yako kwa youtube basi hakuna views inahesabika. hapa video imelenga miji mikuu ya afrika mashariki. ni kama mbadala wa kuanza kufunga safari kwenda katika haya majiji kutambulisha ngoma kwenye vituo vya redio
1586609083902.png


4. Tunachagua iwafikie vijana umri 18 had 36 hawa, tunachagua jinsia ya kike huenda nyimbo ina mahadhi ya kike na tutachagua wanaopenda kurasa za kucheza, kuimba, n.k
1586609440486.png

5.pia tunaweza juchagua lionekane facebook peke yake, instagram, n.k
1586609526831.png

6. hata aina za simu pia
1586609583177.png


7. Na hivi ndivyo tangazo litavyoonekana, view ya youtube itatengenezwa tu endapo mtu ataminya "watch more" akiminya atapelekwa youtube kutazama video, hadi mtu aminye kuangalia video inabidi awe kaipenda au kuwa na hamasa ya kuicheki, bila hivyo huambulii view, huu ni mfano tu

1586611104874.png
 

Attachments

 • 1586608602206.png
  File size
  23 KB
  Views
  0
 • 1586608938174.png
  File size
  3.4 KB
  Views
  0
 • 1586610978543.png
  File size
  175.1 KB
  Views
  0

gwankaja

JF-Expert Member
May 16, 2011
8,225
2,000
Sasa unachopinga nini? Mbona umeeleza vizuri sana namna ya kununua views kwa fb ads? Au wewe kununua ina maana gani kwako?
 

mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
25,575
2,000
kwahiyo ili tujue msanii amenunua views ni mpaka zishuke hesabu basi,kinyume na hapo basi views ni halari???

na je hatuwezi kuendelea kununua views mpaka zikafika milioni hata 50 huko na kiendelea au tukifikisha 1ml bas zoezi la kununua linaisha!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tlg

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
795
1,000
kwahiyo ili tujue msanii amenunua views ni mpaka zishuke hesabu basi,kinyume na hapo basi views ni halari???

na je hatuwezi kuendelea kununua views mpaka zikafika milioni hata 50 huko na kiendelea au tukifikisha 1ml bas zoezi la kununua linaisha!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu you tube wanafyeka view fake, kuna program ( ka algorithm) ambacho kazi yake ni kuchuja fake na halali

Fake zikikutwa zinatolewa zote.
Hio algorithm INA accuracy kubwa sana more than 99%.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Extra miles

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
2,075
2,000
Bora youtube, huko kwingine kama spotify wanatoa wimbo na unakula ban kutumia spotify
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom