Elections 2010 Nane washikiliwa Mpanda (wanadaiwa ni CCM)

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Sunday, 31 October 2010 18:21 Mwananchi Online
Imeandikwa na Kibada Kibada, Mpanda

KAMANDA wa polisi Isunto Mwantage amesema watu nane wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi baada ya kukutwa na silaha za jadi ikiwa ni pamoja na fimbo, rungu na visu.

Watu hao wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa CCM, walikamatwa usiku wa kuamkia Oktoba 31 mwaka huu, usiku wa manane.

Polisi waliwakamata watu hao ambao walidai kuwa wanawatafuta wafuasi wa Chadema kwa madai kuwa walikuwa wanaandika katika barabara maneno ya kampeni kwa kutumia rangi bila kibali.

"Maneno hayo yalikua chagua Arusha, Ruvuma, Iringa na kwingine chagua Chadema hali iliyoashiria ni wafuasi wa Chadema," alidai mmoja wa watu hao.


Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Polisi baadhi ya majina ya waliokamatwa ni Yasini Katampa(52) ambaye ni mgombea udiwani kata ya kashaurini CCM, Deogradius Libe (22), Saidi Benade (32), Nakunde Charles (26), Antoni Abel (21) na Joachim Kweka (46).
 
Polisi waliwakamata watu hao ambao walidai kuwa wanawatafuta wafuasi wa Chadema kwa madai kuwa walikuwa wanaandika katika barabara maneno ya kampeni kwa kutumia rangi bila kibali.

After Dr. Slaa is sworn in office he should forgive all these scofflaws...............
 
Back
Top Bottom