Nane Nane 2020: Maonesho ya kitaifa kuanza Agosti 01 mkoani Simiyu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Maonesho ya Nane Nane kitaifa mwaka huu yatafanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka amesema maonyesho hayo yataanza Jumamosi, Agosti Mosi na kufikia kilele chake Agosti 8.

“Nawakaribisha wananchi wote kutoka mikoa mbali mbali na nje ya nchi kujionea mafanikio ya ubunifu sekta za kilimo,uvuvi na ufugaji,” Mtaka amewaambia waandishi wa habari.

Amesema pia kutakuwa na bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu na kupata elimu ya kukuza ujuzi. “Tunawakaribisha kuungana na viongozi wetu wa Taifa tusherehekee mafanikio ya sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi,” amesema Mtaka.

Amesema pia kutakuwa na burudani za wasanii. Maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima 88 kitaifa zinafanyika mkoani humo kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Mkoa huo wa kimkakati ulipewa fursa kuandaa maonyesho hayo kuanzia mwaka2018 kuongeza tija ya elimu kuhusu kilimo, mifugo na uvuvi kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa Mashariki.
 
Back
Top Bottom