UZUSHI Nanasi huharibu ujauzito

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Nanasi ni tunda lenye faida lukuki kwa afya. Miongoni mwa faida za tunda hili ni kuongeza kinga ya mwili, kutibu mafua, kupambana na saratani, kuondoa maumivu pamoja na kulinda moyo.

973EA762-2BEF-497A-AF05-43B0395AE9D4.jpeg

Pamoja na uwepo wa faida hizi kwa afya, nanasi huhusishwa na changamoto ya kuharibika kwa ujauzito kwa wanawake, hivyo baadhi ya jamii huwashauri wasitumie tunda hili kama njia ya kulinda ujauzito wao. Ukweli upoje?
 
Tunachokijua
Nanasi huhusishwa na kuharibu ujauzito mchanga kwa wanawake.

Athari hii hutokana na uwepo wa vimeng’enya vya bromelain ambavyo kiasili hupatikana kwenye nanasi pekee.

Kwa mujibu wa USDA, Bromelain ni kundi kubwa la vimeng’enya vinavyopatikana kwenye tunda la nanasi ambavyo pamoja na kazi zingine, husaidia mmeng’enyo wa vyakula vyenye asili ya protini pamoja na kutibu au kudhibiti uvimbe mwilini.

Kuhusu ujauzito, ni kweli kuwa Vidonge vyenye bromelain huwa havishauriwi kumezwa na mwanamke mjamzito kwa sababu vinaweza kumfanya apoteze damu nyingi pamoja na kuharibu ujauzito. Hii inatokana na uwepo wa dozi ya kutosha kwenye dawa hizo inayoweza kuleta athari.

Hata hivyo, JamiiForums imebaini kuwa Bromelain inayopatikana kwenye nanasi ni chache sana kuweza kuleta athari zozote kwa ujauzito, haifikii kiasi cha kawaida cha dozi ndogo inayohitajika kuamsha uchungu wa mapema.

Pia, hakuna tafiti za kisayansi zinazothibitisha madhara haya kwa binadamu.

Kwa maana hiyo, nanasi linabaki kuwa tunda bora na salama kwa mwanamke mjamzito kutokana na uwepo wa virutubisho vingi vinavyofaa kwa mama na mtoto.
Ndo yale yale mjamzito asile mayai au kuku sijui atazaa mtoto hana tako mara sijui nini nywele eeh...?! WTF?
 
Ndo yale yale mjamzito asile mayai au kuku sijui atazaa mtoto hana tako mara sijui nini nywele eeh...?! WTF?
Mayai ni protein. Unapomlisha mjamzito mayai, kuku, samaki kwa kiwango kikubwa mtoto kuna uwezekano mkubwa akatoka mkubwa. Ikamletea shida wakati wa kujifungua ikalazimu ajifungue kwa operation.

Usipuuze maneno ya wahenga. Ulitumika uongo ili kusaidia jamii.

Miiko mingine ilikuwa ni marufuku kwenye kwenye misitu na vyanzo vya maji story zilikuwa kwamba kuna majoka makubwa ambayo ukienda linakumeza na kukugeuza chakula. Ili watu wasizoee kwenda maeneo ya vyanzo vya maji wakachafua na kuharibu.
 
 
Tusidharau wahenga.

Kama watu washasema nasisitiza mjamzito usile nanasi ,kama vitamin c kula machungwa.
 
Nanasi ni tunda lenye faida lukuki kwa afya. Miongoni mwa faida za tunda hili ni kuongeza kinga ya mwili, kutibu mafua, kupambana na saratani, kuondoa maumivu pamoja na kulinda moyo.

View attachment 2410631

Pamoja na uwepo wa faida hizi kwa afya, nanasi huhusishwa na changamoto ya kubaribika kwa ujauzito kwa wanawake, hivyo baadhi ya jamii huwashauri wasitumie tunda hili kama njia ya kulinda ujauzito wao. Ukweli upoje?
Nimewahi sikia hata damu ya mke na mme zisipoendanda Kinga ya mwili wa mwanamke huchukulia mimba kama ugonjwa na kuiharibu au kutoka mapema kabla ya muda wake
 
Mimba ikiwa changa haishauriki sana kwa sababu kuna acid ambayo ipo kwenye nanasi itakwenda kuchochea Hormone ya oxytocin na kuchochea uchungu ikapelekea mimba kutoka. Lakini kuanzia miezi 3 mtoto amekuwa amejishikiza vema kwenye mfuko na isilete madhara.
Wewe acha utapeli
 
Mimba ikiwa changa haishauriki sana kwa sababu kuna acid ambayo ipo kwenye nanasi itakwenda kuchochea Hormone ya oxytocin na kuchochea uchungu ikapelekea mimba kutoka. Lakini kuanzia miezi 3 mtoto amekuwa amejishikiza vema kwenye mfuko na isilete madhara.

Na wanashauri kama moja ya Kichocheo cha kuleta uchungu week zikitimia 40
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom