Namwagiza Anna Makinda Kufunga Bunge Sasa Hivi, Haraka sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namwagiza Anna Makinda Kufunga Bunge Sasa Hivi, Haraka sana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Feb 10, 2011.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Spika, Anna Makinda

  Shikamoo mama.

  Mimi Gurudumu (bila gari), raia wa Tanzania, nachukua nafasi hii kukuagiza kwamba ufunge bunge haraka sana pindi tu upatapo ujumbe huu kupitia wasaidizi wako ambao wanafuatilia mijadala kwenye janvi hili saa 24.

  Mimi siyo tu raia wa nchi hii bali ni mwajiri wako, pia nimeajiri wabunge wote na serikali yote ya Tanzania. Hii ni kutokana na kwamba nalipa kodi kupitia mshahara wangu kila mwezi, na kila nachonunua pia nalipa kodi - kila siku.

  Ni kutokana na mamlaka haya niliyonayo kikatiba (raia na mwajiri) nakuagiza ufunge bunge pindi tu upatapo hii barua. Pia ibara ya 27 ya katiba ya JMT inanipa wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi. Hivyo basi nakuagiza ufunge bunge mara moja kwa sababu zifuatazo;

  1. Sasa hivi serikali haina fedha za kutoa huduma kwa waajiri wake (wananchi) kutokana na kufuja hovyo pesa kidogo tulizo kusanya na pia kushindwa kukusanya kodi kufikia malengo. Hivyo pesa kidogo tuliyonayo sasa inatakiwa iwahudumie wananchi mahitaji yao muhimu kuliko kukirimu wabunge kufanya usanii na kusema uongo bungeni.

  2. Bunge lako limepotoka kabisa. Kwamba halitupatii ufumbuzi wowote wa matatizo yanayotukabili wananchi. Badala yake limejikita kwenye siasa za unazi, unafiki, kupakana matope, uongo, kuropoka, kupeana mipasho, kudharauliana, na kukomoana. Tulitegemea bunge hili litutatulie matatizo yetu ya umeme, njaa, uchumi mdororo, ufisadi, elimu iliyoporomoka ubora, huduma za afya zilizoporomoka, upatikanaji wa maji safi, kilimo bora, foleni za magari mijini. Badala yake Bunge lako limekuwa likijadili tu, kama ambavyo sisi tunajadili kupitia kwenye vyombo mbali mbali vya habari. Mnachokifanya hapo mjengoni hakina tofauti na tunachokifanya wananchi nje ya mjengo.

  3. Bunge lako limekuwa mfano mbaya kwetu sisi wananchi. Kwanza watendaji wa serikali wanasema uongo Bungeni. Rejea kauli za baadhi ya mawaziri walipokuwa wanajibu maswali (hata Waziri Mkuu) kutoka kwa wabunge, kwamba wanatoa majibu hewa ya kisanii. Pili, limeshindwa kutuonesha kwamba linajua matatizo yetu, na kwamba lina nia na uwezo wa kuyatatua. Sana sana ni kuzomeana na kushangilia mambo ya hovyo hovyo.

  Mama, mheshimiwa, Anna Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, naomba uheshimu na kutekeleza maagizo yangu haya. Ni muhimu kufanya hivyo kwa sababu kila wananchi tunapotazama wabunge wanavyoongea bungeni tunakonda kwa uchungu. Tunajiuliza kama hiyo ndiyo namna sahihi ya kutumia pesa zetu, na muda wenu. Naamini una uchungu na pesa zetu na muda wa wabunge wako 350.

  Tafadhali tekeleza maagizo yangu, kwani kutokutekeleza ni kufuja mali na rasilimali za watanzania na pia ni kutumia vibaya kodi yangu.

  Wako,

  Gurudumu (bila gari)
  Raia wa Tanzania, na mwajiri wa wabunge wote na serikali nzima ya JMT
   
 2. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Tuitume hii kwenye email ya bunge na email binafsi ya mama Makinda
   
 3. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Duh, hii kiboko!

  Afadhali umetukumbusha kwamba tumewaajiri!
   
 4. Dyslexia

  Dyslexia Senior Member

  #4
  Feb 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tupe vithibitisho kuwa aliyosema waziri mkuu ni uongo?una kazi wewe mwanaume?:laugh::laugh:
   
 5. n

  ngoko JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mhe. Gurudumu, Hizi kodi unazolipa huwa zinabadilika na kuwa na property ya Chang'aa pale zinapoanza kuwahudumia wabunge na wateule wachache wanotumia muda wao mwingi kupiga vijembe na mipasho bila kujadili mambo ya msingi. Sasa basi kwa kuwa chang'aa ukianza kuilamba lazima utalewa na ikizidi sana utakufa au kupofuka naamini hawa waheshimiwa wa mipasho wameshapofuka tayari kama hawatapata msaada wa kidakitari basi shimo refu linawasubiri wakapumzike humo.
   
 6. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  :twitch:
   
 7. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Labda wasaidizi wake watamtonya..ni barua iliyosheheni ukweli..
   
 8. n

  ngoko JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hujui kama kesi imeahirishwa polisi wanatafuta ushahidi ??? sasa huyo PM katoa wapi hiyo conclusion kama Mhe. Hakimu bado anasikiliza hiyo kesi ?
   
 9. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Jamani, nani kakuambia mimi ni mwanaume?
   
 10. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Pengine tumuombe Kiranja na wenzake wamfikishie
   
 11. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #11
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Haahahahahahahahaahaa, tehteheteheteheteh, kwa haraka kachukulia hakuna gurudumu la kike!! hahahahaha, loh samahani hakuna Gurudumu ambapo mmiliki wajina hilo anaweza kuwa mwanamke. Kwa Tanzania yupo mmoja tu tena yeye si gurudumu bali ni Iron lady "Asha Baraka" mmiliki wa twanga. Kuhusu Makinda sijui ya kuku au bata ni aibu tupu. Pia nauliza wabunge wa Chadema wamesharudi bungeni? Maana huku chato kijijini kwa Magufuli sioni Tv wala nini niko interior sana nijuzeni fasta!!! Niko juu ya mti natafuta mtandao wa modem yangu.
   
 12. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #12
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Haya sasa, mohamed mnyaa wa cuf naye anapiga madongo kwa chadema. Hawa watu sasa they sound like vichaa. Inaonekana chadema imewachanganya akili sana
   
 13. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #13
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Pole mkuu, Chadema wako bungeni, wanafurahia mipasho ya ccm na cuf
   
 14. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #14
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  It is sad, really sad. The smiles we have today will some day be history and mark my words, it won't be long!
   
 15. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #15
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ahaaa, sasa mbunge mmoja anasema kwamba eti serikali isichakachue muda wa bunge kukaa kwa sababu ya pesa. Anasema wakati mwingine bunge linaitwa kwa wiki tatu lakini wanaambiwa kutokana na ukosefu wa pesa wakae wiki mbili tu. Pumbafu kabisa, hata siku moja msikae!!!
   
 16. kwamtoro

  kwamtoro JF-Expert Member

  #16
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 4,815
  Likes Received: 770
  Trophy Points: 280
  ipo siku, nitajitoa mhanga mjengoni, ili siasa ianze upya. Somalia, yanapatikana kibao. Mkuu wa kaya akiwepo, hapo ndipo patamu zaidi. Nimekata tamaa.
   
 17. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #17
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Pole mkuu, wengi tumekata tamaa. Utawezaje kuingia mjengoni na mabomu?
   
 18. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #18
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  aa wapi, kwa tanzania hii you will die before it happens
   
 19. kwamtoro

  kwamtoro JF-Expert Member

  #19
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 4,815
  Likes Received: 770
  Trophy Points: 280
  njia za kimafia, pale amna ulinzi. Chenge aliweza kumwaga upupu, kwa nini nishidwe kuutegesha muiraq.
   
 20. D

  DENYO JF-Expert Member

  #20
  Feb 10, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa jinsi watu walivyokata tamaa sintashangaa ................................................
   
Loading...