Namuunga mkono Spika Ndugai, ujenzi Bandari ya Bagamoyo uendelee

Well said, hili ni bonge la investment, kwani mataifa mengi huku Africa wanaimezea Sana mate.. Hii opportunity sio ya kuiacha wala kuipuuz

Hapa naona kuna mvutano kati ya Kikwete na mradi wake wa Bagamoyo na Wafuasi wa Mwendazake . Kikwete alishajicommit kwa WACHINA kuhusu mradi huu. Sasa chini ya uongozi wa Magufuli alikuwa hana njia ya kufanikisha azma yake juu ya mradi huo. On the other hand Magufuli had the Standard Gauge Railway as a priority!!

Is it a coincidence that Kikwete is behind this move to revive the project that Magufuli condemned? No, it is not a coincidence because Kikwete believes that he is behind the success and ascent to the presidency of President Samia Suluhu Hassan and hence now is the opportune time to have the Bagamoyo project implemented. He has assembled a team of followers including the Speaker of the National Assembly to spearhead a campaign to resurrect the Bagamoyo project.

Kama mradi wa Bagamoyo utafufuliwa kwa mkopo au njia nyingine ile nini itakuwa hatma ya Miradi mingine ya mkakati? Kikwete na genge lake nia yao ni kuona hiyo Miradi ya Magufuli haikamiliki ili kuonesha kuwa hakufanikiwa kitu katika urais wake. Je wafuasi wa Mwendazake watakubali? Je nchi iko tayari kuacha miradi inayoendelea na kuanza mingine mipya?
 
Mtoa mada umeeleza upande mmoja tu wa mkata kama ni mzuri, i think uo mkataba umeuona namimi kwa nilivyomjua Magufuli alikuwa na uwezo wa kusoma page to page, Magufuli hakuwa mtu wakuletewa document akasaini tu hapana... naamini hii MU iliingia kwenye baraza la Mawaziri ikasomwa kifungu kwa kifungu huku wakipata tafsiri ya mwanasheria mkuu juu ya mitego iliyokuwepo na uenda ata Mh Rais Hayati aliupitia personal...!! Tueleze na kwa upande wa pili huu mkataba ulikuwa na hatari gani kwa nchi yetu?

Maana hii MU iliandaliwa na Wachina wenyewe lazima walijipendelea sana tu. Namimi sitaki kuamini kama Hayati aliukataa bila sababu.
 
Hapa naona kuna mvutano kati ya Kikwete na mradi wake wa Bagamoyo na Wafuasi wa Mwendazake . Kikwete alishajicommit kwa WACHINA kuhusu mradi huu. Sasa chini ya uongozi wa Magufuli alikuwa hana njia ya kufanikisha azma yake juu ya mradi huo. On the other hand Magufuli had the Standard Gauge Railway as a priority!!

Is it a coincidence that Kikwete is behind this move to revive the project that Magufuli condemned? No, it is not a coincidence because Kikwete believes that he is behind the success and ascent to the presidency of President Samia Suluhu Hassan and hence now is the opportune time to have the Bagamoyo project implemented. He has assembled a team of followers including the Speaker of the National Assembly to spearhead a campaign to resurrect the Bagamoyo project.

Kama mradi wa Bagamoyo utafufuliwa kwa mkopo au njia nyingine ile nini itakuwa hatma ya Miradi mingine ya mkakati? Kikwete na genge lake nia yao ni kuona hiyo Miradi ya Magufuli haikamiliki ili kuonesha kuwa hakufanikiwa kitu katika urais wake. Je wafuasi wa Mwendazake watakubali?
Usanifu ulianza 2004 wakati wa mkapa
 
Mimi naunga mkono mradi wowote ambao utaongeza au kuzalisha ajira kwa vijana wa taifa hili. Kiukweli ukiniuliza kati ya bandari na reli ipi itazalisha ajira nyingi nitasema bandari na kwa sababu hiyo Bandari ya Bagamoyo ijengewe mara moja.
 
Hoja hujibiwa kwa hoja!

Tuambie ubaya wa huu mradi kwa hoja zenye ushahidi. Kutumia hoja za uongo za Magufuli kukataa mradi siyo sahihi.

Tuelezeni kwa hoja specific siyo kutukana watu tu kwa kisingizio cha uzalendo uchwara!
Achane porojo wekeni mkataba hadharani Kama Magufuli alidanganya tutaona wenyewe
 
Hizi kelele zenu za bandari ya bagamoyo dawa hii hapa

Biashara ya duka, mtu huwa huingii mkataba wowote na serikali .Unaenda tu kuomba leseni yaliyobaki ya kwako.

Sasa serikali kama inaona kuna uhitaji wa biashara ya bandari itangaze tu kuwa tunahotaji biashara ya bandari hata mia anayehitaji aje aombe leseni ajenge.Mengine yote yake kuanzia kununua ardhi kufidia nk yanabaki kama ambavyo investor wengine wote hufanyiwa

Hii itakomesha huu utapeli wa watu kutaka kuuza nchi kwa mikataba ya kipuuzi .Bandati ni godown tu la mizigo ya nje inayoingia au kutoka hufikia kwenye hilo godown linaloitwa bandari haihitaji mikataba ya ajabu ajabu na serikali kujenga hilo godown la bagamoyo linaloitwa bandari ya bagamoyo

Ajenge godown lake na magodown mengine yataendelea kama yalivyo .Ndio maana ya biashara huria yenye ushindani

Madalali nendeni mkawaambie wajenge kwa pesa zao tutakuwa tu tunakutana nao TRA

Wawekeze tu kama wawekezaji wengine tu .Walete mitaji yao wajenge tukutane TRA lakini kidiwrko kikaratasi chochote cha mkataba kati yao na serikali waje tu.kama wafanyabiashara wawekezaji full stop.

Si sahihi kuuza nchi kwa sababu ya magodown yanayopigiwa debe kujengwa bagamoyo
 
Mtoa mada umeeleza upande mmoja tu wa mkata kama ni mzuri, i think uo mkataba umeuona namimi kwa nilivyomjua Magufuli alikuwa na uwezo wa kusoma page to page, Magufuli hakuwa mtu wakuletewa document akasaini tu hapana... naamini hii MU iliingia kwenye baraza la Mawaziri ikasomwa kifungu kwa kifungu huku wakipata tafsiri ya mwanasheria mkuu juu ya mitego iliyokuwepo na uenda ata Mh Rais Hayati aliupitia personal...!! Tueleze na kwa upande wa pili huu mkataba ulikuwa na hatari gani kwa nchi yetu?

Maana hii MU iliandaliwa na Wachina wenyewe lazima walijipendelea sana tu. Namimi sitaki kuamini kama Hayati aliukataa bila sababu.
Kati ya Mwendazake na Mkwere nani na mzalendo zaidi? Msisahau HOME SHOPPING CENTRE mbia wa Mkwere ambao mwisho mwisho mwa utawala wa mkwere na mwanzo mwa Utawala wa Magufuli walibadilisha jina na kuitwa GSM!!
 
Tuachane na viongozi hio ni personal zaidi, hao wote washa play part yao, tu stick na huu uwekezaji ambao ulikuwepo mda mwingi mkakati huu toka 2004 kabla ya hao viongozi, hoja yetu Bandari ya Bagamoyo pamoja na matunda yake Kama mleta mada alivyo state kwenye thread hapo juu.. ambao unagharimu $ 10 billions, nanukuu hio sio TZS ni USD.... Kati ya nchi 3, Tz, China & Oman..
 
Mkataba uwekwe wazi, tuone masharti yaliyopo.

Mtoa mada uliwahi sikia maelezo ya Hayati Magufuli kuhusiana na huo mradi? Una kipi cha kusema? Kama hukuwahi kumsikia katafute video aliyozungumzia Bandari, ujisikilizie mwenyewe.

Kama masharti ni yale aliyoyasema Magu, wewe unaona bado ni sawa kuendeleza?
 
Najua topic imepita, lakini ninajua kidogo kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo na napenda kumuunga mkono Mhe Spika kwa hoja zifuatazo. Na naamini Serikali yetu itazichukulia kama ushauri wa Mbunge kwa Serikali, ambao ndio wajibu wetu wa msingi kama Wabunge.

Muhimu kujua background ya mradi wa Bandari ya Bagamoyo. Kwanza, mradi huu ulibuniwa na Serikali yetu kama Bagamoyo Special Economic Zone mwaka 2004 chini ya Mpango Kabambe wa Ujenzi wa Sekta Mpya ya Viwanda. Serikali ya Japan ndio ilitusaidia kwenye hili. Mradi huu uliitwa “Tanzania-Mini Tiger 2020” na ulikuwa chini ya Wizara ya Viwanda.

Mamlaka ya Bandari nayo ilibuni Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009-2028) ambao ulipendekeza Bandari ya Bagamoyo ijengwe katika miaka ya 2021/2022 ili iwe tayari kujaza nafasi baada ya Bandari ya Dar es Salaam kufikia ukomo wa kuweza kuongezewa uwezo. Kwahiyo mambo mawili ya msingi hapa ni kwamba: (a) Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo tuliubuni sisi wenyewe, ulikuwa sehemu ya mipango yetu ya muda mrefu na haukujengwa kwa msukumo wa Wachina; (b) mradi wa Bandari ya Bagamoyo sio ni mradi wa Bandari, bali ni mradi wa Ukanda wa Kiuchumi ambao unaendana na mji wa viwanda.

Mwaka 2009 Mamlaka ya Bandari, kupitia kampuni ya Hamburg Port Counsulting ya Ujerumani, ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na
kuona una manufaa kutekelezwa. Mwaka 2011, Wizara ya Viwanda na Biashara, kupitia CowiConsult, nayo ilifanya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ), kwa kufungamanishwa na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.

Mipango yote hii ilikuwa ni yetu wenyewe, na tulijiridhisha kama nchi kwamba Bandari ya Bagamoyo tunaihitaji na tukaiweka kwenye Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa kama Mradi wa Taifa wa Kielelezo.

Mwaka 2013 na 2014, Kampuni ya China Merchants Ports Limited, ikiungana na Mamlaka/Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA), waliomba kuwekeza katika Mradi wa BSEZ na Bandari ya Bagamoyo. Baadaye kidogo, Korea Kusini nao, kupitia Taasisi yao ya Science and Technology Policy Institute” (“STEPI”) ilikamilisha Upembuzi Yakinifu wa kuwekeza katika kujenga na kuendeleza “Bagamoyo High Technology Park” kwa kushirikiana na EPZA pamoja na COSTECH. Kwahiyo hoja nyingine ya kuzingatia hapa ni kwamba Bagamoyo sio uwekezaji wa Wachina pekee, kama inavyodhaniwa. Yapo mataifa mengine. Oman wanaweka pesa yao nyingi. Na Korea Kusini nao wanaweka pesa na maarifa yao.

Kama nilivyoeleza hapo awali, kwa mujibu wa Mpango wa Pili wa Miaka Mitano wa Maendeleo (“FYDP II), Mradi wa Bagamoyo Special Economic Zone (BSEZ) ni Mradi wa Taifa wa Kielelezo. Mradi huo unatarajiwa kuwa utavutia uwekezaji wa Dola za Kimarekani bilioni 10; utakuwa na Viwanda 760 na hatimaye kutoa ajira 270,000 kwa awamu ya kwanza. Majadiliano ya Utatu wa Serikali ya Tanzania, China Merchants na Mfuko wa Uwekezaji wa Oman yalikuwa yanaendelea kuelekea makubaliano na hatimaye kuingia Mikataba ya Uwekezaji kabla ya kusimamishwa.

Zipo hoja kubwa tatu zinazosemwa kuhusu mradi huu: (1) utatutwika madeni kama vile Kenya na Sri Lanka ambapo Wachina walilazimika kutaifisha Bandari; (2) tutaua bandari ya Dar es Salaam; (3) haturuhusiwi kuendeleza Bandari yoyote na haturuhusiwi kutia mguu pale Bagamoyo kwa miaka 99.

Hoja hizi zote sio za kweli, na kwa kweli wawekezaji wa huu mradi wamekuwa wana-struggle namna ya kuzijibu kwasababu zinatolewa na watu wakubwa, na hao wawekezaji, hasa wa Oman, ni mamlaka za Serikali na wasingependa malumbano na Serikali yetu.

Hoja ya kwanza, kwamba tutakopa na kujitwika deni kubwa sio ya kweli: kwenye mradi huu hakuna hata senti tano ya mkopo tunachukua. Huu ni uwekezaji. Hakuna deni hapa, ni pesa ya kigeni inaingia kuwekezwa.

Hoja ya pili kwamba tutaua bandari ya Dar haina mantiki, kwasababu hata kabla Wachina hawajafika ilikuwa ni ndoto na mipango ya Mamlaka ya Bandari kujenga Bandari ya Bagamoyo. Ukisoma Mpango Kabambe wa Miaka 20 wa Uendelezwaji wa Bandari za Tanzania (The Tanzania Port Development Master Plan 2009-2028), wenyewe Mamlaka ya Bandari walitaka Bandari ya Bagamoyo iwe imejengwa ifikapo mwaka 2023. Bandari za Bagamoyo na Dar sio bandari shindani. Ni bandari zitakazosaidiana kuongeza shehena ya mzigo unaopita nchi mwetu. Full stop! Pia Bandari ya Bagamoyo itajengwa kwa kuzingatia teknolojia ya uundwaji wa meli za kisasa (4th Generation Shipbuilding Technology Port). Meli hizi, ambazo zitakuwa zinaongezeka kadri miaka inavyokwenda, haziwezi kutia nanga kwenye bandari ya Dar. Na kama unaitazama nchi kwa miaka 30, 50 ijayo, Bandari ya Dar ina ukomo wa upanuzi. Lazima kama nchi kujenga Bandari mpya kubwa katika ukanda huu ili kuendelea kunufaika na faida ya kijiografia.

Hoja ya tatu kwamba Wachina wanataka tusijenge wala kuendeleza Bandari yoyote kwa miaka 99 na tuwape wao bandari hiyo bila sisi kutia mguu pale sio ya kweli. Hakuna pahala popote wawekezaji wametoa hayo madai. Ukweli ni kwamba kote duniani mwekezaji anapoweka hela yake mwenyewe kwenye mradi atataka muda wa kutengeneza faida kabla hajakukabidhi mradi. Hapa Wachina na Wa-Oman walitaka miaka 33 ya concession. Je, ni mingi au ni michache? Inategemea pesa iliyowekwa (US$10bn) na standard practice kwingine duniani. Reli ya kuunganisha UK na France, ambayo imejengwa na sekta binafsi ina concession ya miaka 50. Kwa bandari standard practice ni miaka 25-40, kutegemeana na ukubwa wa uwekezaji. Cha msingi kwa timu ya negotiators wetu ni kupata financial models za wawekezaji na kuzichambua na kuona wanaanza kupata faida baada ya muda gani. Na cha kutambua pia ni kwamba concession inahusu tu faida ya Bandari na kwamba katika kipindi hiki cha concession bado TRA itakuwa inakusanya kodi nyingine zote husika za mizito bandarini.

Suala lingine la kutazama katika kufanya maamuzi ni kuangalia dunia inaelekea wapi kwenye biashara ya kimataifa. Tutake tusitake, nchi yetu inategemea biashara ya nje kimapato na China kwasasa ndio kinara wa biashara ya import and exports duniani. Inaongoza kwa kuagiza na kuuza bidhaa nje na itaendelea kuwa kinara kwa miaka 50 inayokuja. Ukifungamana nao, utashinda. Kwa mujibu mpango wa China wa Belt-and-Road-Initiative (BRI), meli kubwa za bidhaa zitakazopita katika 21st Century Maritime Silk Road kusafirisha bidhaa kati ya China na Afrika ya Kati na Kusini, zitafikia katika moja ya Bandari za Mwambao wa Mashariki ya Afrika, kama Mlango na Kituo Kikubwa cha kupokea, kuhifadhi kwa muda na kusafirisha shehena kwa meli au usafiri wa nchi kavu. Kulingana na kudra ya kijiografia ya Tanzania ambayo inaimarishwa na uwepo wa Reli ya Kati (SGR) tunayojenga pamoja na reli ya TAZARA, Bandari ya Bagamoyo ambayo itaunganishwa na Reli ya Kati na TAZARA, itakuwa haina mshindani Nje ya Tanzania katika dhana nzima ya ushirikiano wa maendeleo ya uchumi baina ya China na Afrika, kupitia BRI kwa muktadha wa 21st Century Maritime Silk Road.

Mwisho, ni muhimu kutambua kwamba kuna siasa za ushindani na majirani zetu kwenye hili suala. Jirani zetu Kaskazini yetu wanapigana kufa na kupona mradi huu usitokee. Kwahiyo mtaona disinformation nyingi kuhusu huu mradi huku baadhi ya watu wetu wakitumika bila kujijua.

Wenzetu tayari wameanza tena kuifuata kampuni ya China Merchant kuwashawishi wahamishie ule mradi Kenya kule LAMU. Mwaka 2018 wakati wa mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kiongozi wao alikwenda Shenzen kuzungumza na China Merchant kuwashawishi waende kwao. China Merchat walikataa na ndio walikutana na Waziri Mkuu Mhe Majaliwa. Na majuzi, tarehe 25 Machi 2021 wameandika barua tena China Merchant kuomba mradi upelekwe kwao (barua nimeiona).

Mwisho, nitamalizia kwa hadithi ndogo: mwaka 1970, wakati Dubai bado ni kamji kadogo jangwani, wazungu waliona potential ya location ya Dubai kibiashara na wakamwendea mfalme wa wakati huo Rashid bin Saeed Al Maktoum kupendekeza wakajenge bandari na waiendeshe kwa miaka 30. Washauri wake wakamwambia tusiwape Wazungu bandari kwenye nchi yetu. Sheikh akawauliza “sisi tuna pesa ya kujenga?”, wakajibu hapana, akawauliza “tutaipata lini”, wakasema hatujui, akawauliza “Dubai itaendelea kuwepo miaka 30 ijayo?”, wakajibu ndio, akawauliza “baada ya miaka 30 wataing’oa bandari na kuondoka nayo?”, wakajibu hapana, akasema “tuwape”. Wazungu wakajenga Port Rashid mwaka 1972. Miaka 30 ikapita haraka. Watu wa Dubai wakajenga uwezo wa kuendesha bandari na wakaanzisha Dubai Port World (DP World), moja ya makampuni makubwa duniani. Dubai sasa ni kinara wa bandari duniani. Majuzi wamechukua bandari za Senegal na Angola. Na wamejenga bandari hadi Rwanda ambapo hakuna hata bahari, wanawasaidia Rwanda kwenye biashara ya logistics.

Mpendwa wetu hayati Rais Magufuli alipenda maendeleo. Alitaka nchi yetu ipate manufaa kwenye miradi na mikataba. Namna ya kumuenzi na kufanya makubaliano yenye tija kwa taifa kwenye mradi wa Bagamoyo. Na hilo linawezekana kama timu yetu ya negotiators itakuwa makini kuzingatia maslahi ya nchi.
Kwasasa simwamini kikwete, Magufuli wala Ndugai. Ninachotaka ni mkataba uwekwe wazi ili tujue nani muongo nani mkweli.
 
Back
Top Bottom