Namuunga mkono Anna Kilango Malechela kwa nguvu zote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namuunga mkono Anna Kilango Malechela kwa nguvu zote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by lara 1, Aug 5, 2012.

 1. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Kufuatia Mh. Sophia Simba kukalia hicho kiti awamu iliyopita na kuamua kutetea kiti chake awamu hii huku wakichuana vikali na Mh. Anna Kilango Malechela mimi msimamo wangu ni kumuunga mkono Mh Anna kwa hali na mali kwasababu zifuatazo:-

  1.UNDUGU NA KUJUANA KUMEZIDI

  Jumuiya hii imekuwa ikipoteza mantiki kabisa na kuwa jumuiya ya wake na watoto wa vigogo na mijimama ya mjini yenye majina makubwa ilhali uwezo wa mtu kuongoza na kukiletea chama maendeleo hauangaliwi kabisa wala kuzingatiwa. Kama huna jina mujini na pesa haiongei fungua njia kitoto chaanza tambaa. Na hili limedhihirika sana kipindi hiki kinachoisha cha Mh. Simba, ni dhahiri tukiendela kumkabidhi usukani kitakuwa chama cha watu fulani flani na mijimama ya mjini. Bora tubadili upepo tumuweke huyo mpare tuone hali itakuwaje ila hali ya Mh. Simba haifaiiiiiiiiiiiiiiiiii!

  2.CHAMA KIMEPOTEZA MUELEKEO
  Kusema kweli mpaka sasa chama kipokipo tu mradi kipo, hakina uelekeo wala ushawishi wowote. Chama hichi ilipasa kiwe chachu ya kuongeza wanachama wapya hususani kina mama kwenye kata na wilaya huko, ukizingatia chama chetu hiki kimesambaa sana yaani laiti lingetiliwa mkazo hili kila mjumbe kutimiza hili wala uchaguzi wa 2015 tungekuwa pazuri, Alivochukua Mh Simba nikajua kidogo mzoefu atatilia hili mkazo hamnaaaa, mpaka anamaliza chama alivokikuta ndo anakiacha. Bora tumfungulie njia Anna Kilango tuone nae manjonjo yake sio mtu tushaona uwezo wake hauturidhishi afu tumpe mda zaidi? hataaaa nabisha!

  3.CHAMA HAKIENDI NA WAKATI
  Chama hakikui kisera wala michakato, sera zile zile za kina bibi titi mpaka leo? Chama kinatakiwa kuiga mfano wa magamba kwenda na wakati, kwenda vyuoni kuvuna silaha mpya, kuwekeza katika vijana. Wadada wapo wengi sana wana uwezo huko vyuoni wanajiunga na magamba badala ya chama letu kubwa chama la kijani? Tena resources za kurecruit tunazo, nia tunayo na nguvu tunayo. Chama hakijikiti sekondari huko kupanda mbegu za kijani katika vibinti vidogo vikue kimtazamo wa kichama na kuja kuwa chachu mbeleni, Uvivu wa kupanda mbegu ndo watu wanajiunga ukubwani kumbe mamlukiii tu,kuja kuchafua chama. Haya Sofia hakufanya ya happen, tumpe nafasi Anna nae tuone karata zake zitakwendaje

  4.TIME FOR CHANGE
  Tumempa Sofia nafasi na tumeona uwezo wake, sasa mimi kwa mtazamo wangu kuwa aliyofanya Sofia hayatoshi na uwezekano wa kufanyika zaidi na zaidi ya hayo ulikuwepo na she didint make things happen! Its time for change, tumpe mtu mwingine nafasi alete mabadiliko, na aliponigusa ni kutamka wazi wazi kuwa mambo si mazuri, ataleta mabadiliko, sasa Sofia anadai chama ni madhubuti kwa hiyo hata umuhimu wa hayo mabadiliko hauoni, Bora aneona tuliko huku siko! Mda wa mabadiliko umefika wanachama wenzangu, tusizubae zubae.

  5. LACK OF VISION
  Anna kaenda kuchukua fomu, mda mchache aliopata na waandishi wa habari kaweka wazi vision yake ni kuleta mabadiliko endapo atapita, sasa mwenzie yeye alivoenda kuchukua mda aliopata na waandishi badala ya ksema vision na sera zake, kaanza kumuattack opponent wake. Hiyo inaonesha hajajipanga akishinda afanyeje na anatingishwa na nguvu ya mpinzani wake. Mi namuunga mkono mtu anejua kwanini anagombea ambaye ni Mh. Anna.


  ANNA KILLANGO MALECHELA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mie naona wote wawili yaani Simba na Kilango ni mabomu ya kawaida. Hakuna mwenye nafuu. Ila kwa vile nafasi wanayopigania ni ndani ya genge la mafisadi, wenye chenu mtajua mchague balaa gani kati ya mabalaa hayo mawili.
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wote wameharibika hakuna msafi kati yao hata mmoja
   
 4. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  sasa ndo wagombea hao, inabidi kuchagua mmoja. Ambaye hajaaribika sana
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Vote For Sophia Simba
   
 6. F

  FUSO JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,297
  Trophy Points: 280
  mnakumbuka shuka kumeshakucha?
   
 7. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hiyo mada peleka redio Uhuru.
   
 8. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Kwani Anna kilango si ndiye ameolewa na Yule kikongwe wa dodoma mtera? Kama ndiye yeye hafai
   
 9. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  jukwaa la watu waote hata ccm tupo huku na tunahaki, mbona mkiandika yenu ya magwanda tunawaachia nafasi? watanzania wote ni ndugu.
   
 10. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  its better late than never!
   
 11. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Hafai kwa sababu kaolewa na kikongwe au? people be objective, n stop negativity
   
 12. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwani mkono wake umefanyaje!!
   
 13. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ameingia na Halima Mamuya, hivi sasa ngoma inogile!!!!
   
 14. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Lile kongwe lilikuwa fisadi la kutupwa
   
 15. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,077
  Likes Received: 10,436
  Trophy Points: 280
  Haya magamba njoeni hapa mpige kura zenu kati ya Kilango na Sofia nani zaidi..

  Mimi sio kwamba wote hawafai ila ccm yote siitaki.
   
 16. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,296
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Halima Mamuya is a veteran contester, may be this time she might win. Ila nyinyiem mtajuana wenyewe.
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu sekondari kuna vijana na si akina mama hivyo sehemu yao ni UVCCM ja siyo UWT!Naona mwaka huu uchaguzi wa UWT utakuwa kabambe manake wamama wote hao ni kiboko kwa kunena! Uchaguzi uliopita naona Mama Simba alikutana na wepesi kwani MAma Kahama alionekana kuwa mwepesi na hakujua fitna za mujini! This time round wanakutana watu wa fitna. Mama Simba wa Dar Ilala na Mama Kilango naye wa Dar na amewahi kufundisha pale Kisutu Secondary; wote ni wamama wa MUJINI wanaenda KIMUJINI MUJINI! Na kila mmoja anawakilisha kundi kubwa ndani ya CCM na hapa ndipo tutaanza kuona kundi gani litatoa mgombea Urais 2015 na kundi gani litatoka kapa na hivyo kukaa kimya ndani ya chama ama kujiengua kabisa. Uchaguzi ndani ya CCM ni mtihani mkuu.
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mamuya angeacha tuone ngoma hii ikichezwa na hawa wawili. Unajua ngoma hii wameanza kuicheza zamani. Mama Simba aliwahi kumshutumu MAMA Kilango kwamba ni fisadi na aliwahi kuchukua pesa za Jeatu Patel kwa ajili ya kampeni za Urais 2005! Mamuya na Madabida wakae kando tuone ngoma ya hawa wawili.
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu Molemo kumbe huwa unakuwa hata upande huu wa pili ma una watu unaowaunga mkono huku? Safi sana.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2012
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kweli mkuu kwa Sophia na Kilango tungepata/tutapata burudani ya kutosha kwa sababub kila mmoja ana dark side zake na wote hawaogopi kuumbuana; itakuwa ni sinema tosha acha tukae mkao wa kula!!
   
Loading...