Namuonea huruma kikwete

MWANALUGALI

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
601
34
Kwa mara ya kwanza ktk historia ya nchi yetu, suala la udini limewekwa hadharani na kiongozi wa nchi baada ya kuwa limetumiwa na chama chake kumdhibiti Prof. Lipumba mwaka 2000 na mwaka huu wakatumia mtindo huo huo kumdhibiti Dr. Slaa asichukue urais.

Uchaguzi unaokuja 2015 ambao kwa utaratibu ambao siyo rasmi kwa CCM, tunategemea kuwa watamweka mgombea ambaye ni Mkristo. Ninasema hivyo kwa sababu Rais wa kwanza alikuwa Mkristo akafuatiwa na Muislam halafu Mkristo then Muislam tena. Kwa maana hiyo zamu inayofuata ni Mkristo!!! Kazi iliyo pevu na ambayo namuonea huruma JM.Kikwete ni namna gani atafanya kuwaridhisha Wanzanzibar ambao sasa inatakiwa kuwa zamu yao!!
Namuonea huruma Kikwete kwa sababu wakimuweka Mzanzibar lazima atakuwa Muislam na kuna uwezekano mkubwa ubara/uzanzibari na udini vikatumika sana na kuigawa nchi yetu ktk mapande. namuonea huruma Kikwete kwa sababu pamoja na migawanyiko mingine ya walio nacho na wasiokuwa nacho, kuendelea kuongezeka, namuonea huruma kwamba nchi hii ataiacha ikiwa ni vipande vipande na historia itamhukumu!!!. je na wewe unamuonea huruma?
 
Great thinker; hilo suala la Urais kupokezana kwa misingi ya Uislamu na Ukristo au Utanganyika na Uzanzibar halipo kwenye katiba yetu (mazoea siyo sheria)..
Isitoshe usilazimishe kutuaminisha kuwa ni jukumu la rais aliyepo madarakani kumweka mrithi wake,,,
hivyo hana haja ya kuumiza kichwa chake kuwa awaridhishe vipi akina nani kwa sababu hilo halimhusu...

Just thinking aloud...
 
Mkuu TAMNO great thinkers takes their time to think, nadhani huwa wanaachana na tabia ya kuwa wavivu wa kufikiri!! Unataka wote tume kama mbuni anayeficha kichwa chake kwenye mabawa akifikiri kuwa kwa vile hawaoni maadui zake nao hawatamuona? come on Mkuu, be more than that and think great !!

Ningelifurahi sana kama ungeniambia kuwa mabadiliko makubwa ya katiba yanakuja na kila kitu hakitakuwa na mizengwe tena na wala hesabu za CCM hazitafuatwa au kufua dafu!! Kila kinachotokea ktk nchi hubebeshwa/hupewa Rais aliyeko madarakani. Kumbuka mazungumzo ya siri ya Malim Seif na Karume yaliyozaa muafaka yamegeuka kuwa mtaji wa kisiasa wa Rais aliyeko madarakani pia kumbuka kuwa vifo vya Wapemba waliouawa na wengine kukimbia nchi kwa mara ya kwanza lilikuwa ni doa lisilofutika kwa Rais wa wakati ule!!!!
 
"Ukiisha tenda dhambi ya ubaguzi, ukawabagua wenzio, hauwezi kuwa salama maana dhambi hiyo itakuandama!"
 
Kwa mara ya kwanza ktk historia ya nchi yetu, suala la udini limewekwa hadharani na kiongozi wa nchi baada ya kuwa limetumiwa na chama chake kumdhibiti Prof. Lipumba mwaka 2000 na mwaka huu wakatumia mtindo huo huo kumdhibiti Dr. Slaa asichukue urais.

Uchaguzi unaokuja 2015 ambao kwa utaratibu ambao siyo rasmi kwa CCM, tunategemea kuwa watamweka mgombea ambaye ni Mkristo. Ninasema hivyo kwa sababu Rais wa kwanza alikuwa Mkristo akafuatiwa na Muislam halafu Mkristo then Muislam tena. Kwa maana hiyo zamu inayofuata ni Mkristo!!! Kazi iliyo pevu na ambayo namuonea huruma JM.Kikwete ni namna gani atafanya kuwaridhisha Wanzanzibar ambao sasa inatakiwa kuwa zamu yao!!
Namuonea huruma Kikwete kwa sababu wakimuweka Mzanzibar lazima atakuwa Muislam na kuna uwezekano mkubwa ubara/uzanzibari na udini vikatumika sana na kuigawa nchi yetu ktk mapande. namuonea huruma Kikwete kwa sababu pamoja na migawanyiko mingine ya walio nacho na wasiokuwa nacho, kuendelea kuongezeka, namuonea huruma kwamba nchi hii ataiacha ikiwa ni vipande vipande na historia itamhukumu!!!.
Haya tutayakuza wenyewe kwa sababu mpaka sasa kikwete hajawa muwazi anazungumza kitu gani kuhusu udini-ni siri yake na wale wachache ambao amewamegea!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Interpretation zetu kama hazioani na dhana aliyo nayo kikwete bado hoja hii itabaki kitendawili-kwa malengo gani anajua mwenyewe?????????????????????????????
 
Interpretation ya Kikwete na CCM yake ni kutumia udini katika kumkosanisha mgombea na wapiga kura wake! Wamefanya hivyo mara nyingi lakini sasa mbinu zao hizo zitawageuka mwaka 2015. Mwaka 1995, Mrema akiwa na nguvu nyingi za kisiasa; CCM walifanya kila mbinu kumgombanisha na Waislam naye kwa ujanja wake akawaingiza CCM mkenge, akawaahidi kuwapatia Mahakama ya kadhi ingawa alijua kuwa ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Sasa wanahangaika na Mahakama ya kadhi na for sure huu ndio mpasuko mkubwa wa kidini ambao unakuja!!!!

Haya mengine ya kuwapakaza Lipumba kuwa eti ni mjahidina na ameingiza mapanga kuwachinja Wakristo na hili la Dr. Slaa kuwa eti ni padre aliyetumwa na Kanisa katoliki kuja kuitawala Tanzania, yatamuandama mpaka kwenye chama chake!
Namuonea huruma maana Kikwete amejikuta ktkt ya mstari ambao hakuutarajia!
 
Great thinker; hilo suala la Urais kupokezana kwa misingi ya Uislamu na Ukristo au Utanganyika na Uzanzibar halipo kwenye katiba yetu (mazoea siyo sheria)..
Isitoshe usilazimishe kutuaminisha kuwa ni jukumu la rais aliyepo madarakani kumweka mrithi wake,,,
hivyo hana haja ya kuumiza kichwa chake kuwa awaridhishe vipi akina nani kwa sababu hilo halimhusu...

Just thinking aloud...
TANMO........... shambani kwako ukiacha watu wapite (watumie sehemu ya shamba lako kama njia) kwa miaka mitano...............basi huo mwaka wa sita utakapotaka kuziba hutaweza................ NA UKISHITAKIWA KWA KUZIBA UNAWEZA UKAFUNGWA................ MAZOWEA HUJENGA KAWAIDA................. NA KAWAIDA HUZAA HAKI........HATA KAMA HAIPO KWENYE MAANDISHI YOYOTE...........
 
well said mkuu
 
Hiyo ndo KATIBA halisi!
 
Ni vema Rais 2015 akatoka Zanzibar ili kudumisha umoja wetu...hivyo kila chama cha siasa kimsimamishe Mzanzibar aongoze nchi yetu...naamini pendekezo hili la mambadiliko ya katiba ni muhimu liwekwe wazi kwenye katiba

Ili CCM, CUF, Chadema watafute mgombea mzanzibar washindane itaondoa ubaguzi kuliko kuweka (mzenj vs mtanganyika)
 
Simuonei huruma hata kidogo kwani aliseme " NATAKA WATANZANIA WANIKUMBUKE NITAKAPO MALIZA KIPINDI CHANGU CHA UONGOZI" Inavyo onekana ndilo analotaka tumkumbuke nalo kwani kwa mema kama aliyo fanya Mwalimu, Mh. Ben bado hawezi kufuta hivyo labda kwa ubaya!!!!
 
Miiba ya JK
Mahakama ya kadhi na OIC
Urais 2015
Mtandao na wapambanaji
Ahadi zake kutimiza
 
Kanisa Katoliki lagoma kuzika

Imeandikwa na Peti Siyame, Sumbawanga; Tarehe: 14th December 2010 @ 08:00

KANISA Katoliki Parokia ya Familia Takatifu Jimbo la Sumbawanga, limegoma kuendesha ibada ya maziko kwa marehemu wawili wakidai ibada haitaendelea mpaka pale waumini ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotengwa na kanisa hilo, watakapoondoka ndani ya kanisa hilo.

Marehemu hao ni aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Msua iliyopo Manispaa ya Sumbawanga, Mekitrida Maufi ambaye ni mke wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Rukwa ambaye pia kwa sasa ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa, Patrick Maufi.

Maiti nyingine ambayo jina lake halikuweza kupatikana mara moja, ni ya mtoto wa darasa la nne ambaye pia shule aliyokuwa akisoma haijajulikana.

Tukio hilo lilitokea jana saa 8 mchana na lilidumu kwa saa tatu pale waombolezaji walipoleta miili ya marehemu hao kanisani hapo kwa ibada ya maziko.

Wengi wa waombolezaji hao walikuwa ni wanaCCM wakimsindikiza mfiwa na wengi wao walikuwa wameshatengwa kwa kinachodaiwa kuwa waliisaliti imani yao ya dini wakati wa Uchaguzi Mkuu kwa kumshabikia mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Sumbawanga Mjini, Aesh Hilaly.

Baada ya waombolezaji kufika na majeneza ya miili hiyo mbele ya milango ya kanisa wakiwa tayari kuingia ndani, yalisomwa matangazo yaliyodai kuwa ibada ya kuombea marehemu haiwezi kufanyika hadi waumini waliotengwa (wanaCCM), watawanyike na wasionekane nje wala katika maeneo ya karibu na kanisa hilo.

Miongoni mwa waumini hao waliohudhuria, lakini wametengwa ni pamoja na mwenyekiti wa CCM Mkoa, Hypolitus Matete, Mwenyekiti CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini, Charles Kabanga, Katibu wa CCM Mkoa, Fraten Kiwango, Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Sumbawanga Mjini aliyefahamika kwa jina moja la Tumombe na Diwani wa CCM Viti Maalumu Kata ya Sumbawanga, Aurelia Kanyengele.

Hali hiyo iliibua dhahama na kusababisha vurugu ya makundi mawili kati ya waliyotengwa na wanaounga mkono maamuzi hayo ambayo yalitiliwa nguvu na Paroko wa Parokia ya Kristu Mfalme, Pambo Mlongwa aliyefika maeneo hayo na kuwashinikiza mapadri waliokuwepo pale kuendelea na msimamo huo huo na kuwafanya waumini kuwataka waliokataliwa waondoke ili ibada ifanyike.

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mjini, John Mzurikwao aliwataka waumini hao kwa kuwa wametengwa, watii maamuzi hayo na kuwasihi kuondoka hapo ili utaratibu wa ibada ya mazishi uendelee.

Viongozi hao baadhi walikubali na kurejea msibani, lakini baadhi ya waliotengwa walitoka nje ya uzio na kusubiri miili ya marehemu ili waungane na wenzao ili kwenda mazikoni. Ibada ya mazishi iliendelea.

Francis Chale ambaye ni Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM Wilaya ya Sumbawanga akizungumza na gazeti hili, alikiri si kutengwa tu, bali alivuliwa ukatoliki wake, akituhumiwa kumshabikia Hilaly ambaye ni Muislamu, aliyetuhumiwa na kanisa hilo kwa kuukufuru utatu mtakatifu katika moja ya mikutano yake ya kampeni alipojifananisha na Yesu Kristo kwa kuelezea dhana nzima ya mafiga matatu yaani Rais, Mbunge na Diwani.

"Kitendo hiki kimetusikitisha sana, tulidhani kwamba tumezuiwa tu kuhudhuria ibada za misa takatifu kumbe hata ibada za mazishi. Sasa kama hali ndio hiyo na kanisa linajitambulisha kwamba ni wakala wa Chadema, basi na sisi tuliotengwa tunajipanga tupandishe bendera ya Chadema kwa kila Parokia iliyopo katika jimbo hili," alidai Chale.

Hivi karibuni, Parokia kadhaa za Jimbo Katoliki limewasimamisha waumini wake kwa madai ya kuisaliti imani yao kwa kutotii imani ya kanisa ambayo yaliwataka wasishabikie mgombea wa CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Katika msuguano huo wa kiimani, tayari kanisa hilo limewasimamisha na kuwatenga makatekista kwa madai wamelisaliti kanisa kwa kuwahamasisha waumini wao kumshabikia mgombea wa CCM.

Hata hivyo, kutokana na mchakato huo, kanisa hilo linajiandaa kutangaza orodha ya mapadri waliolisaliti hadharani ili nao waadhibiwe kama walivyoadhibiwa waumini hao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom