Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Ni dhahiri sasa kuwa CHADEMA na UKAWA hawana mgombea mwenye sifa kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi Mkuu wa 2020. Ninasema hivi kwa sababu, Lowasa hatakuwa mgombea wa chama hicho kwenye uchaguzi huo.
Ubashiri wangu unaonesha kuwa kuanzia mwaka 2017 hadi 2018, CHADEMA kitakumbwa na mtikisiko mkubwa wa kisiasa ambapo makundi kadhaa yatazaliwa ndani ya chama hicho. Hata hivyo, litaibuka kundi kubwa la wafia demokrasia ambao watataka misingi ya haki na usawa itumike katika kuwapata viongozi wa chama hicho na mgombea Urais ifikapo 2020.
Kutokana na mtafaruku utakaojitokeza ndani ya CHADEMA ambapo Lowasa atalazimisha ateuliwe kuwa Mwenykiti pekee ili awe na nguvu ya kusimamia chama kwenye uchaguzi Mkuu, hali hiyo itamfanya afarakane na Mbowe anbaye anatamani kuendelea kukalia kiti hicho. Hali hiyo itasababisha mvutano mkubwa na makubaliano yatafanyika kuwa Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti na Lowasa awe Mgombea Urais. Hata hivyo, litaibuka kundi la wafia demokrasia ambao watataka kuwe na ushindani kwenye nafasi zote za uchaguzi na uteuzi. Hata hivyo, Freeman Mbowe atafanikiwa kuwarubuni wanachama wengi na hivyo kufanikiwa kutetea kiti chake.
Kimbembe kitakuwa kwa Edward Lowasa. Lowasa hatakuwa mgombea wa CHADEMA na UKAWA kwa vile litajitokeza kundi kubwa litakalompinga. Kundi hilo litalazimisha kuwe na upigaji kura wa siri kwenye mchakato wa kumpata mgombea Urais ili kurekebisha kasoro zilizojitokeza mwaka 2015. Kundi hilo litaibuka mshindi na Lowasa atatupwa nje ya ulingo. Frederick Sumaye ataibuka kuwa mshindi kwa nafasi ya mgombea Urais wa CHADEMA.
Hadi 2018, ACT Wazalendo na Zitto Kabwe watajumuishwa ndani ya UKAWA kwa lengo la kuupa nguvu upinzani. Baada ya kujumuishwa na Zitto Kabwe kuteuliwa na chama chake kuwa Mgombea Urais, atapambanishwa na wagonbea wengine ndani ya UKAWA ambapo kura za siri zitatumika kumpata mgombea. Katika kura hizo, wafuasi wa Lowasa hawatamchagua Sumaye na badala yake watampa kura Zitto kabwe. Hali itakayomfanya ndugu Kabwe kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya ACT na Mwamvuli wa UKAWA.
Hivyo, Zitto Kabwe atapambana na Dr Magufuli wa CCM. Magufuli ataibuka mshindi kwa zaidi ya asilimia 80 kwa vile CHADEMA hawatampigia kura Zitto hasa kutokana na msimamo wa viongozi wa chama hicho kuwa Zitto ni Msaliti.