Namuona Rais Samia Suluhu Hassan akienda kunyakua tuzo ya Mo Ibrahim. Labda wana CCM wamkwamishe!

Capitrait

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
228
326
Awali ya yote mie binafsi nampongeza mno mno mno hadi sasa walau anatutia moyo na kuturudishia matumaini mapya!

Huyu Mama ana set standards za namna Kiuongozi Mkuu wa nchi anavyopaswa kuwa.

  • Hafokei
  • Haropoki
  • Yupo very composed
  • Hana papara
  • Anafahamu shida za watanzania ki uhalisia
  • Mpole kama Kiongozi Mkuu wa nchi
  • Hana mhemuko
  • Hana hamaki
  • Mtulivu
  • Hana ubinafsi. Muda mwingi anatumia wingi, yaani hasemi nataka bali tunataka. Hasemi nikikuta bali tukikuta
  • Mtaratibu.

Huyu ndio Rais aliyebeba tumaini jipya la watanzania. Huyu ndio Rais ambaye ninaamini wananchi wapinzani miaka yote walikuwa wanamhitaji, na sasa wamempata ndio maana mtandaoni ni nderemo na vivijo watu wamefurahi.

Wasichokijua wengi kuhusu Rais Samia ni hiki:

- Kabla ya kuingia kwenye siasa Rais Samia alikuwa mwanaharakati akifanya kazi kwenye NGO's kadhaa.

- Kilichomwingiza kwenye siasa ni pale alipokuwa anaona viongozi wa serikali wanapwaya kwenye utendaji wao yaani wakionekana kama hawajui vema kuhusu kero za wananchi wao. Hivyo, Rais Samia hakuingia kwenye siasa kwa tamaa ya vyeo ama njaa tumboni na akilini.

Kwa traits hizi za Rais Samia ni wazi kuwa atakuwa moja ya Marais Bora kuwahi kutokea katika utawala nchini Tanzania, na hatimaye kunyakua tuzo ya Mo Ibrahim.

Nani atamkwamisha?

- Wana CCM ndio watakaomkwamisha. Wana CCM wataweka mambo ya ukada kwenye utendaji wa ki serikali. Kitu ambacho wana CCM wengi hawakijui hasa wale wanaojiita makada na pengine hata viongozi wao ni hiki:

Watanzania wengi hawapo deep sana kwenye mambo ya uchama, watanzania ni watu humble sana wakihudumiwa vizuri. Kinacholeta mambo ya ukada Kwa watanzania wachache ni ukada wa wana CCM wenyewe hasa viongozi wao. Watanzania walio wengi kiu yao kubwa ni kuhudumiwa vizuri na uongozi bila kujali chama kinachounda serikali.

Tazama uteuzi na utenguzi wa Mkurugenzi wa TPDC just to see an example. Ile move for sure ni ya makada wa CCM.

Go Samia! Go Tanzania!
 
Hakika Mama ana roho safi 'Mungu ni mwema ametupatia Mama kiongozi bora ambaye hatu kutarajia!
Huyu sasa nina kuombea kwa moyo Mkunjufu kabisa awe na maisha marefu na yenye afya tele
 
Hata mimi nimeliona hili. Kwa Jinsi anavyoibadirisha Tanzania, ndani na nje Hadi vyombo vya kimataifa vinaanza kumkubali hivi Naona akistaafu hapo 2030( Mungu amwezeshe) akinyakua tuzo hii adhimu.
 
Madam President atadhihirisha hili mnamo May Mosi hii

Hamtoamini ati

Mwacheni Rais anaiunganisha nchi yetu (Mama Tanzania).

Ngoja aje kufuta machozi ya wafanyakazi kwa vitendo. Tanzania itajengwa na watanzani wenyewe yaani sisi

Asante
 
Aliifikisha wapi msumbiji kiuchumi na akili zake mfu zile???
Sera zipi mfu zaidi ya kumuua Rais Samora kwenye ndege? Yule msouth aliesema alishiriki kupanga njama kumuua Huyo Rais unaona kitu gani angetekeleza?
Ukweli ni kuwa maslahi ya magharibi huwaondoa viongozi thabiti wa nchi maskini wanaowapinga.
 
Hata mimi nimeliona hili. Kwa Jinsi anavyoibadirisha Tanzania, ndani na nje Hadi vyombo vya kimataifa vinaanza kumkubali hivi Naona akistaafu hapo 2030( Mungu amwezeshe) akinyakua tuzo hii adhimu.
Mama hatakiwi kustaafu Mkuu! Mama anatakiwa atawale mpaka dk. Ya mwisho! Yaani like zoezi la kumuondolea Rais ukomo wa kutawala lifanyike haraka sana!
 
Back
Top Bottom