Namuona Piere Kwenye Kampeni za Uchaguzi 2020

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,310
Namuona Piere akiwa kwenye VX akila zake kiyoyozi huku amekunja nne akila keki ya taifa.

Namuona Piere akizunguka mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya, tarafa kwa tarafa, kata kwa kata na mgombea urais mojawapo wa chama cha siasa nchini katika uchaguzi mkuu wa mwakani 2020.

Tofauti na watu kama akina Dr Shika, Piere amekuja katika kipindi ambacho tunakaribia uchaguzi, hivyo kwa ule umaarufu na swaga zake atakuwa catalyst mzuri sana kwenye mikutano ya kisiasa.

Nadhani yule mkuu wa mkoa hakupiga mahesabu ya harakaharaka kwamba watu kama hawa huwa ni wazuri sana wa kuvutia watu kwenye mikutano ya kisiasa. Hakusoma alama za nyakati.

Hebu fikiria Piere yuko jukwaani mbele ya umati wa watu 1000 akiweka kionjo chake kile cha "Zitoooooooooo,,,,,atabaki kuwa juuuu, atabaki kuwa juuuu, juuuuu mawinguniii, Zitoooooo". Hapo nadhani utajua swaga za Piere zina thamani kiasi gani.

Lakini Piere nakushauri kitu kimoja, zichange karata zako vizuri, hii nafasi ilokuja kwako ni once in a life time. Japo watu wengine wanakuona kama mlevi fulani lakini hawajui tuu. Mkuu wa nchi mwenyewe juzi kasema Gongo sio haramu endapo itapitia shirika la viwango na ikahakikiwa ubora wake kabla haijawafikia watu kama nyie.

So wewe ni nani hadi usipige liquid, wakati ndo inayoongoza kwa kulipatia taifa kodi kubwa? Fanya makeke uwe ambasador kamili wa hiyo sekta.

Huyuhuyu Piere baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 tusishangae kumuona akipata siti pale bungeni, haya maisha hakuna aijuaye kesho yake.

Huyo ndo Piere bwana, mzee wa likwidi.

Kila la kheri Piere.

IMG-20190405-WA0002.jpeg
 
Back
Top Bottom