Namuona Pasco Mayalla kwenye teuzi za Rais Magufuli

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,592
29,715
Kwanza nimpongeze member mwenzetu huyu kwa kuthubutu na kuomba uteuzi wa kugombea ubunge wa Kawe kupitia CCM. Mchakato wa uteuzi umekamilika wateuliwa kugombea kupitia CCM wameshatajwa.

Jimbo ambalo pasco Mayala aliweka nia kupitia jimbo la Kawe na aliyepitishwa kupeperusha bendera ya CCM ni askofu Gwajima. Hivyo kwa hitimisho hilo inapaswa watia nia wote wa jimbo hilo kupitia CCM na hawakupata nafasi wataifanyia kampeni CCM ipate ushindi dhidi ya Mbunge wa sasa mhe. Halima Mdee ambaye amepitishwa tena kugombea kupitia chama cha CHADEMA.

Ninamuona Pasco Mayala kama mtu makini mwenye uthubutu pia msimamo mahiri unaodhihirisha utajiri wa fikra nyingi chanya. Ukipitia posts zake ilikuwa siyo rahisi king'amua huyu ni mwanaCCM. Alishawahi kutoa hoja zilizomfikisha mbele ya kamati ya maadili ya Bunge ambapo alitoka akiwa mshindi.

Msimamo wake na endapo ataendelea kuonyesha uzalendo kwa nchi yake ninamuona ni mtu ambaye anasubiri muda muafaka kuteuliwa kwenye serikali ijayo ambapo bila shaka tunajua JPM atashinda tena.

Ninamuona kwenye nafasi ya kiweza kuwa mbunge au Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa au Katibu wa Wizara au Afisa Tawala au Msemaji wa Ikulu, anaweza kufaa kwenye nafasi hizo au zinazoweza kuhitaji huduma yake.

Mimi kama mwanachama mkongwe wa JamiiForums ninaona kwa dhati nyota ya ndugu yetu ikipaa angani. Nina ombi moja kwa Pasco, usiache kuisemea JF hasa yale chanya ambayo wengi wanaziba masikio kana kwamba hawayajui. Usiache kututetea.

Wakatabahu
Msanii.
 
Back
Top Bottom