Uchaguzi 2020 Namuona Magufuli akishinda Uchaguzi Mkuu 2020 kwa zaidi ya 50%

Idrisa1510

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
252
350
Habari za mihangaiko watanzania wenzangu!

Binafsi mimi siyo mfuasi wa chama chochote cha siasa hapa Tanzania. Mimi ni mtanzania ambaye kura yangu ninaitoa kwa mgombea kulingana na sera zake na ushawishi wake kwangu.

Nimekua nikifuatilia baadhi ya kampeni za wagombea mbalimbali wa vyama tofauti kwa ngazi ya uraisi, na tathmini zangu zinampa nafasi kubwa Magufuli kuongeza miaka mitano mingine kwa ushindi wa zaidi ya 50%. Hii imekuja kufuatia sababu zifuatazo:

1. Zaidi ya nusu ya watanzania hawaja elimika, wengi wao wana elimu ya shule ya msingi (darasa la saba) au sekondari (kidato cha nne). Na hawa ndio wengi wao huvumilia kukaa kwenye foleni ya kusubiri kumpigia kura mgombea wakati wa uchaguzi, kwani wasomi wengi wa Tanzania wamekuwa na kasumba ya kutoshiriki katika upigaji kura kwa kuamini kura zao haziwezi badili matokeo au kwa kuamini ni upotevu wa muda.

Hili kundi kubwa ambalo halijaelimika vya kutosha, ndio hua linasahau masaibu ya kimaisha ya miaka yote mitano waliyopitia kwa ulaghai wa miundombinu na maendeleo feki ambayo kiufupi hayana faida kwa mwananchi ya kipato cha chini. Kundi hili halina taarifa za kutosha kuhusu hali ya taifa na life standard ya mwananchi mmoja mmoja, na hushawishika kwa maneno ya kilaghai na maendeleo yasio na faida kwao. Hivyo itakua ngumu kwa kundi hili kuzielewa na kuzikubali sera za upinzani.

2. Matumizi ya wasanii ( wanamuziki na waigizaji) na watu mashuhuri katika kampeni za JPM inampa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi mkuu. Iko wazi kuwa asilimia kubwa ya wasanii wa muziki na tamthilia Tanzania wameamua kushirikiana na chama cha mapinduzi. No matter wako kimaslahi au vipi, uwepo wao unaleta ushawishi mkubwa kwa wapigakura, kwani kila msanii ana followers ( mashabiki watiifu) ambao wako tayari kumchagua JPM si kwasababu wanazielewa sera zake ila tu kwa mahaba walio nayo kwa msanii huyo.

Mfano hai ni kwa washabiki walio poteza mapenzi yao kwa Real Madrid na kuhamia Juventus kufuatia kuhama kwa nguri wa soka wa Ureno Christiano Ronaldo. Kwahiyo, sio ajabu mtanzania wa Kasulu kumchagua JPM kwa sababu ya mahaba yake kwa Diamond, sio ajabu mtanzania wa Mtwara kumchagua JPM kwasababu ya mahaba yake kwa Harmonize na sio ajabu mtanzania wa Mkata kumchagua JPM kwa sababu ya mapenzi yake kwa mwanadada Zuchu.

3. Mchango wa vyombo vya habari na mawasiliano. Iko wazi kuwa baadhi ya vituo vya redio na tv vimejidhihirisha wazi kumuunga mkono mgombea wa uraisi kwa tiketi ya chama cha mapinduzi, JPM. Kuna kundi kubwa la watanzania pambao inakuwa ngumu kuwafikia physically. Kupitia vyombo vya habari kama redio na tv, inampa mgombea Magufuli nafasi ya kuishawishi hadhira hii kumpigia kura.

Nahakika support ya vyombo vya habari kwa upinzani haiko sawa uki linganisha na ile wanayopatiwa CCM. Hii itawezesha sera za mgombea wa CCM kuifikia idadi kubwa ya watu na hivyo inampa nafasi mgombea wa ccm kushinda kwa kishindo.

4. Kukosekana kwa ushirikiano miongoni mwa vyama vya upinzani. Haiwezekani kuiondoa CCM kwa aina hii ya siasa za upinzanani, huku chadema na Tundu, A.L., kule ACT na ex-kada wa CCM, na bila kusahau kule CHAUMA na Bwana Misosi wao. Ilipaswa vyama vya upinzani viungane kumshambulia adui yao mmoja ambaye ni JPM, kuliko wao kwa wao kushambuliana kunyang'anyana vikura vichache vitakavyoacha na Raisi wa wanyonge, in their voices, bwana JPM.

Hivyo kuto kuwepo kwa ushirikiano miongoni mwa wapinzani kunanifanya niitupie karata yangu ya ushindi wa kishindo kwa bwana JPM kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.

5. Ukosefu wa tume huru na ya haki, mchango wa jeshi la polisi na taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kama TCRA , misikiti na makanisa, n.k.

IMANI YANGU
Kuna kipindi cha miaka 10 tena kwa CCM kuendelea kuitawala Tanzania. Naamini hili wimbi kubwa la wahitimu wa vyuo linalo achwa mtaani bila ajira huku likiongezeka kila mwaka, familia zote zilizo athirika kwa namna tofauti tofauti kutokana na utawala wa CCM, hali ngumu ya kimaisha inayozidi kuwaandama watanzania na mengine mengi kwa pamoja matokeo yake itakua ndio chachu ya kuondoka kwa serikali ya Mapinduzi madarakani. Na hicho kipindi, kitaambatana na machafuko ya amani.
 
Hizo 50% zitatokea kwa ma DED, NEC, Police na TISS baada ya kuiba kura. Magufuli kiukweli hawezi akapata zaidi ya 30%.
Amewasababishia Watanzania kwa ujumla wao maisha magumu sana
 
Kwa point ya pili naomba nikukosoe.

Mpira ladha yake hailingani na siasa.

Niombe radhi tafadhali
 
Back
Top Bottom