Namuona Barbara Gonzalez katika picha ya Marina Granovskaia wa Chelsea

iron finger

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
358
220
Nyuma ya mafanikio ya Chelsea chini ya Bilionea wa Kirusi Roman Abromovic yupo mwanamke wa shoka na jasiri Marina Granovoskaia,Aliajiriwa katika kampuni ya mafuta ya Mrusi Roman Abromovic ya sibnfet mwaka 1997 kabla ya kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Abromovic kwenye bodi ya Chelsea mwaka 2010,huwezi kukuta akitajwa sana katika vyombo vya habari.

Kwa miaka zaidi ya kumi amebaki kuwa gizani, hajawahi kuonekana katika shughuli za nje ya uwanja.Ana rekodi ya kuwa CEO wa kwanza kutofanya na Interview na chombo chochote cha habari duniani tangu ajiunge na Chelsea mara nyingi kuonekana wakati wa kutambulisha wachezaji wapya au kusaini mikataba mbalimbali,Huyu ndie Marina injini ya mafanikio pale the Blues.

Licha ya kuwa gizani bado amebaki kuwa mtu mwenye kauli kubwa katika mambo ya kiutendaji Marina ndiye aliyeamua kwenda tofauti na uamuzi wa bodi kwa kutaka Didier Drogba aongezewe kandarasi kubakia darajani mwaka 2009.Alihusika pia katika kurejesha mahusiano mazuri kati ya Roman Abromovic na Jose Mourinho hadi kupelekea Mourinho kurejea Chelsea kwa mara ya pili mwaka 2013,

Dili zote za kusajili wachezaji kuanzia Fernando Torres,Eden Hazard, Diego Costa, Kai Havertz Timo Warner, Hakim Ziyech na wengineo wote mpaka deals za kuajiri makocha tofauti zilisimamiwa vilivyo mwanamama huyu mwenye asili ya Kirusi na Canada

Sio mnunuzi mzuri wa wachezaji tu pia ni bingwa mzuri wa kuuza wachezaji kwa faida,ameweza kuingiza faida kubwa kwa mauzo ya Diego Costa, Nemanja Matic,David Luiz kwenda PSG ,Eden Hazard na Alvaro Moratta kwa uchache.

Granovskaia alihusika kwa sehemu kubwa wakati wa makubaliano ya udhamini mpya wa jezi kwa kuingia mkatabaj uliovunja rekodi wa pauni milioni 900 na miamba ya nguo Nike mnamo mwaka 2016, zaidi ya mara mbili ya mkataba wake wa awali na Adidas.

Maamuzi ya Roman hayana tofauti kubwa na ya Mohammed Dewji(Mo)mdhamini na mmiliki wa Club ya Simba baada ya kuondoka kwa Senzo Mbatha, tofauti na matarajio ya wengi alileta jina geni katika soka la Tanzania mwanadada Barbara Jaime Gonzalez ambaye kabla ya hapo amefanya kazi katika kampuni za Mo kwa muda kidogo, licha ya umri mdogo lakini ameonekana kuwa na mafanikio na malengo ya kuifikisha mbali Simba.

Barbara anavunja rekodi ya kuwa CEO mwanamke wa kwanza Tanzania na pengine Africa katika umri mdogo pia huku akihudumu katika club ambayo kwa sasa ni mojawapo ya miamba katika soka la kiafrika, licha ya pressure kubwa na kutokuzoea kwa baadhi ya watu ameweza hadi sasa kuonesha matumaini makubwa, Simba SC ipo katika hatua ya robo fainali ya champions League.

Kuondoka kwa Sven Vandenbroeck katikati ya msimu na michuano ya kimataifa kuliwapa wakati mgumu Simba lakini chini ya utendaji makini wa Barbara Simba walifanikiwa kumpata Didier Gomes ambaye anaonekana bora na kupata mafanikio makubwa zaidi ya mtangulizi wake,hii inathibitisha utendaji makini wa Barbara

Usajili wa Thadeo Lwanga, Larry Bwalya, Chris Mugalu unaonekana pia kuthibisha maono makubwa ya Barbara katika njanja ya ufanyaji biashara nzuri ya usajili kama ilivyo kwa Marina Granavoskaia wa Chelsea.

Nje ya uwanja Barbara amefanikisha deal ya kusaini mkataba wa kwanza mnono wa uzalishajj jezi kwa Tanzania, Simba wakiingia mkataba na kampuni ya Fredi Vunja Bei wa kitita kisichopungua zaidi ya bilioni 2

Wakati kila mtu akizungumza na kuhoji kuhusu mkataba wa Mohammed Hussein Zimbwe Jr ,Barbara hakutetereka alikuwa akifanya kazi kimya kimya, katikati ya mayowe na kuulizana Tshabalala alionekana akisinya Simba ni Kazi ya Barbara mfukuza mwizi kimya kimya

Licha ya muda mfupi akihudumu kama CEO wa Simba lakini mafanikio yake ndani ya uwanja na nje ni makubwa,bado ana mipango mikubwa ya kutengeneza Simba iwe taasisi kubwa kimataifa,kuifanya iwe na timu bora ya vijana na wanawake, kuongeza mapato ya club na kufanya ijiendeshe kwa faida,tayari jina la Barbara linanifanya nimuone Barbara Gonzalez kama Marina Granovoskaia wa Simba, wakati Roman Abromovic yuko zake Urusi akila mvinyo katika Yatch zake ni muda sasa wa Mo kuangalia mambo yake mengine anaye Marina katika Babra Gonzalez.
 
Story ya huyu Dada wa Chelsea sidhani kama umeiandika sahihi.
Kwa ninavofahamu wakina Torres, Eden hazard hawa walikuja Chelsea kipindi Emiliano akihusika zaidi na sio huyu Dada.
Pia huyu Dada wa Chelsea kuna mda alimtia hasara Boss alileta wachezaji wa kiwango kidogo sana na wasio endana na chelsea mfano... Miazga,Zapacosta,Drinkwater, Kennedy,kepa ,morata,Bakayoko na hili hata Antonio Conte alilalamika kuwa analetewa wachezaji asio wahitaji.

Kwa upande wa Simba huyu Dada Babra yuko vizuri na pia kwenye maswala ya usali usisahau pia kutoa credit kwa kina Hans pope.
 
Yes niko sahihi mkuu vyanzo vya taarifa vyote ni sahihi wakati wa Drogba anakaribia kuondoka darajani Marina ndo alihusika kutaka aongezewe mkataba hata wakato Michael Emanalo stili Marina ndo alikuwa na sauti kubwa ndiye alikuwa anapokea na kupeleka maagizo na maelekezo toka kwa boss directly
 
Mungu ambariki Muamedi yeye ndiyo anapiga hii pisi.
20210429_222747103038.jpg

Mkuu unateseka?
 
Nyuma ya mafanikio ya Chelsea chini ya Bilionea wa Kirusi Roman Abromovic yupo mwanamke wa shoka na jasiri Marina Granovoskaia,Aliajiriwa katika kampuni ya mafuta ya Mrusi Roman Abromovic ya sibnfet mwaka 1997 kabla ya kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Abromovic kwenye bodi ya Chelsea mwaka 2010,huwezi kukuta akitajwa sana katika vyombo vya habari.

Kwa miaka zaidi ya kumi amebaki kuwa gizani, hajawahi kuonekana katika shughuli za nje ya uwanja.Ana rekodi ya kuwa CEO wa kwanza kutofanya na Interview na chombo chochote cha habari duniani tangu ajiunge na Chelsea mara nyingi kuonekana wakati wa kutambulisha wachezaji wapya au kusaini mikataba mbalimbali,Huyu ndie Marina injini ya mafanikio pale the Blues.

Licha ya kuwa gizani bado amebaki kuwa mtu mwenye kauli kubwa katika mambo ya kiutendaji Marina ndiye aliyeamua kwenda tofauti na uamuzi wa bodi kwa kutaka Didier Drogba aongezewe kandarasi kubakia darajani mwaka 2009.Alihusika pia katika kurejesha mahusiano mazuri kati ya Roman Abromovic na Jose Mourinho hadi kupelekea Mourinho kurejea Chelsea kwa mara ya pili mwaka 2013,

Dili zote za kusajili wachezaji kuanzia Fernando Torres,Eden Hazard, Diego Costa, Kai Havertz Timo Warner, Hakim Ziyech na wengineo wote mpaka deals za kuajiri makocha tofauti zilisimamiwa vilivyo mwanamama huyu mwenye asili ya Kirusi na Canada

Sio mnunuzi mzuri wa wachezaji tu pia ni bingwa mzuri wa kuuza wachezaji kwa faida,ameweza kuingiza faida kubwa kwa mauzo ya Diego Costa, Nemanja Matic,David Luiz kwenda PSG ,Eden Hazard na Alvaro Moratta kwa uchache.

Granovskaia alihusika kwa sehemu kubwa wakati wa makubaliano ya udhamini mpya wa jezi kwa kuingia mkatabaj uliovunja rekodi wa pauni milioni 900 na miamba ya nguo Nike mnamo mwaka 2016, zaidi ya mara mbili ya mkataba wake wa awali na Adidas.

Maamuzi ya Roman hayana tofauti kubwa na ya Mohammed Dewji(Mo)mdhamini na mmiliki wa Club ya Simba baada ya kuondoka kwa Senzo Mbatha, tofauti na matarajio ya wengi alileta jina geni katika soka la Tanzania mwanadada Barbara Jaime Gonzalez ambaye kabla ya hapo amefanya kazi katika kampuni za Mo kwa muda kidogo, licha ya umri mdogo lakini ameonekana kuwa na mafanikio na malengo ya kuifikisha mbali Simba.

Barbara anavunja rekodi ya kuwa CEO mwanamke wa kwanza Tanzania na pengine Africa katika umri mdogo pia huku akihudumu katika club ambayo kwa sasa ni mojawapo ya miamba katika soka la kiafrika, licha ya pressure kubwa na kutokuzoea kwa baadhi ya watu ameweza hadi sasa kuonesha matumaini makubwa, Simba SC ipo katika hatua ya robo fainali ya champions League.

Kuondoka kwa Sven Vandenbroeck katikati ya msimu na michuano ya kimataifa kuliwapa wakati mgumu Simba lakini chini ya utendaji makini wa Barbara Simba walifanikiwa kumpata Didier Gomes ambaye anaonekana bora na kupata mafanikio makubwa zaidi ya mtangulizi wake,hii inathibitisha utendaji makini wa Barbara

Usajili wa Thadeo Lwanga, Larry Bwalya, Chris Mugalu unaonekana pia kuthibisha maono makubwa ya Barbara katika njanja ya ufanyaji biashara nzuri ya usajili kama ilivyo kwa Marina Granavoskaia wa Chelsea.

Nje ya uwanja Barbara amefanikisha deal ya kusaini mkataba wa kwanza mnono wa uzalishajj jezi kwa Tanzania, Simba wakiingia mkataba na kampuni ya Fredi Vunja Bei wa kitita kisichopungua zaidi ya bilioni 2

Wakati kila mtu akizungumza na kuhoji kuhusu mkataba wa Mohammed Hussein Zimbwe Jr ,Barbara hakutetereka alikuwa akifanya kazi kimya kimya, katikati ya mayowe na kuulizana Tshabalala alionekana akisinya Simba ni Kazi ya Barbara mfukuza mwizi kimya kimya

Licha ya muda mfupi akihudumu kama CEO wa Simba lakini mafanikio yake ndani ya uwanja na nje ni makubwa,bado ana mipango mikubwa ya kutengeneza Simba iwe taasisi kubwa kimataifa,kuifanya iwe na timu bora ya vijana na wanawake, kuongeza mapato ya club na kufanya ijiendeshe kwa faida,tayari jina la Barbara linanifanya nimuone Barbara Gonzalez kama Marina Granovoskaia wa Simba, wakati Roman Abromovic yuko zake Urusi akila mvinyo katika Yatch zake ni muda sasa wa Mo kuangalia mambo yake mengine anaye Marina katika Babra Gonzalez.
hakuna kitu wa simba mdangaji tu
 
Write your reply...huyo Babra ni kivuli tu, maamuzi yote yanatoka kwa MO. Marina hatafuti show off kwenye mitandao na vyombo vya habari kama Barbra. Babra kila siku kiguu na njia kupiga selfie na akina etoo, alitakiwa awe Public Relation Offifcer, sio C. E. O
 
Back
Top Bottom