Kikwete baba tunakukumbuka na tunazidi kukukumbuka

kakaye

Member
Jul 21, 2016
87
63
Chonde chonde baba yetu sio wote tuliokuona mbaya wengi tunakukumbuka baba. Semasema kidogo tunakufa na hali ngumu ya maisha duu!! Uuwi tunaipata mbaya biashara ndo usiseme haziendi tumenyooka mbaya..

Nachukua nafasi hii kuomba radhi kwa rais mstaafu mh Jakaya Mrisho. Kipindi upo madarakan jamii ilikuwa ikilaumu hali ya uchumi.

Mh kwa sasa nakukumbuka sana. Mh huko ulipo nachukua nafasi hii kukuambia mishahara atujaongezewa july hii. Badala ya kuwa July mwez wa watumishi imegeuka kuwa mwez wa msiba mkubwa.

Mh huku hali sio shwari. Kila nikipita kwenye daraja lako la Kigamboni nazidi kukukumbuka japo haukufanikiwa kulizindua.

Nakumbuka ulipowalisha wahanga wa mabomu ya Gongo la Mboto kwa moyo wa dhati. Sasa hivi tumeambiwa hapewi mtu chakula hapa. Sasa yakitokea ya Gongo la mboto sijui itakuwaje.

Ulikuwa unatupa moyo kuwa nchi ipo shwari. Lakini hivi karibuni tumeambiwa yaliyotokea Rwanda na Burundi yanaweza tokea na hapa. Tunaogopa sana mioyo imejaa hofu!

MUNGU AKUBALIKI KWA MAMBO ULIYOWAH KUFANYIA WANANCHI. JAPO KWA KIPINDI HICHO HAYAKUONEKANA
 
Chonde chonde baba yetu sio wote tuliokuona mbaya wengi tunakukumbuka baba. Semasema kidogo tunakufa na hali ngumu ya maisha duu!! Uuwi tunaipata mbaya biashara ndo usiseme haziendi tumenyooka mbaya....
Hatari sana
 
Kuna hatari ya nahodha na nahodha mstaafu kupigania usukani chombo kikenda mrama.

Kwanini wananchi wanajiona hawawezi kusema wenyewe mpaka awasemee Kikwete?

Watanzania tulio wengi hatuna ujasiri wa kuwakoromea watawala wetu.

Hivi unadhani Watanzania wanaweza wakafanya uasi wa kupinga watawala waliopo madarakani?

Mi bado sijauona huo ujasiri aisee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom